Vyama vinakosea kuwaruhusu vijana wa siku hizi kuwa wasemaji

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Vijana wa siku hizi wana uelewa mdogo, washabiki na wapenda sifa. Vijana naongelea hapa ni chini ya miaka 35 ambao wapo kwenye kundi hizi za umoja wa vijana. Je ni wangapi wamewahi kukupa ushauri wa maana!. Siwasemi kwani ni tatizo la kidunia kwa sasa.

Inasikitisha kuona vijana wa miaka 20's na 30's eti wanajaribu kumkosoa Mtaka au Diallo na tunawapa uzito. Cha ajabu badala ya kuangalia hoja muhimu wanatafuta vijimaneno vya ili tu watu waendelee kuwa wanafiki na kuongopwa kufukuzwa kwa kutoa yaliyo moyoni. Kama ni kweli waelewa wangekuwa wanakosoa kwa hoja kwasababu siyo yote waliosema hawa viongozi ni kasfa.

Mtaka kusema kwamba viongozi wengi hawajui machungu ya wananchi wa kawaida ni hoja, Mtaka kusema watoto wa wakubwa wanaishi maisha tofauti na watoto wa wakulima ni hoja. Diallo kusema serikali iliyopita ilikuwa inaonea watu ni hoja, Diallo kusema kwamba biashara zilikimbia ni hoja. Sasa hawa vijana ambao hawana kazi tungefikiria wangeunga mkono hoja ya Diallo ambaye ni mfanyabiashara mkubwa kuhusu kazi na ajira badala yake vijana wanaongelea maneno machache ya kumkashifu hayati!. Diallo kusema kwamba katiba mpya isitengezwe na wanasiasa bali wataalamu kama kenya ni hoja muhimu lakini badala yake hawa vijana hawajui hata kwamba katiba nzuri itawasaidia wenyewe.

Tatizo hii miaka ya mitandao tumekuwa na vijana washabiki sana na kuchukulia vitu kirahisi rahisi tu. Hivi ukifikiria Dr Diallo biashara ambazo kafanya pale mwanza kuanzia miaka 1980 kwa mazingira yale leo hii badala ya kujifunza ni kumfanya kama vile tu ni mtu poa kana kwamba hawa vijana wamefanya kitu chochote. Ukiwa na miaka 22 unafikiria unajua kila kitu! lakini ukifika miaka 40 unagundua ukiwa miaka 22 ulikuwa hujui kitu kwasababau kikubwa sio kusoma kwenye magazeti na mitandao bali uzoefu. Hawa vijana hawana uzoefu wa maisha lakini tunawaruhusu watuendeshe hoja kama wanajua wanachokifanya. Ujuaji huu ambao unatokana na mitandao sio ujuaji wa ukweli maana kujua kitu unahitaji uzoefu.

Hata mimi ni kijana wa miaka 40's lakini tuseme ukweli hawa madogo zetu mitandao imewaaribu ni walalamishi kila siku, hawataki kujituma na wajuaji wa kila kitu. Hivyo nawashauri tuwapuuze na topic hapa za kijinga tusiziendekeze ili huu mtandao usiwe mtandao wa uzushi badala yake tuwe na hoja na tuache utoto
 
Back
Top Bottom