Vyama imara vya siasa ndivyo vilivyosaidia Magufuli kupata urais

mbikagani

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
3,107
1,782
Ukiangalia mchakato mzima wa uteuzi wa wagombea ndani ya CCM utakubaliana nami kuwa bila ya kuwa na vyama tishio kwa CCM, Magufuli urais kwake ulikuwa ndoto.Pale ndani ya CCM na wajumbe wa halmashauri kuu, ni wachache sana walikuwa na mtazamo wa kumpitisha Magufuli ku contest nafasi ya urais.

Magufuli anapaswa kufahamu hili kwamba, mchango wa vyama vya siasa katika maendeleo ya nchi hii ni tofauti sana na vile yeye anavyozani.Kimsingi yule aliyeikubali ile 20% ya wale waliopendekeza kuwepo kwa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 aliona mbali sana.Si vyema kwa rais wetu kubeza vyama vya siasa na kuviona vinamcheleweshea ahadi zake kwa wananchi.

Ni vyema atambue hili kwamba ili kuwa na maendeleo endelevu ni vyema jamii ishirikiane katika kuyaleta hayo maendeleo pamoja na kuyasimamia.Unaweza kuwa na maendeleo lakini bila kuwa na maelewano maana nzima ya maendeleo haipo, kwani ikifika wakati wa kunyang'anyiana fito, hayo maendeleo hupotea kama upepo.Ni vyema atambue kuwa vyama hivi ndivyo vimemfanya leo hii awe raisi, ni bora avisikilize na ashirikiane navyo ili kuleta maendeleo endelevu.

By mpenda maendeleo.
 
Does Mr. President Magufuli refuse to cooperate with the opposite political alliance in bringing Tanzania development?
 
Mungu huwa anatenda miujiza kama ile ya Mussa akiwa Misri. Madhari tushampata aliye wa kweli, hizo zingine zitabaki porojo. Usisahau na historia zingine zilizopita 1985/1995
 
Back
Top Bottom