Vyama 11 vya upinzani visivyo na uwakilishi katika Bunge la Tanzania, vimetangaza kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
8,498
10,967
Hivi ndio vile UMD, NRA, CCK, SAU ,TADEA, PONA, DP na vingine.

Hivi ndio mikoa ya ccm, wao ndio huibeba ccm kila
CHADEMA inapokataa kushiriki.
Nakumbuka waliitwa diamond jubilee baada ya uchaguzi wa 2015 kukubali matokeo baada ya CHADEMA kuyagomea.

Imetokea tena, leo wanatoa tamko la pamoja kushiriki uchaguzi baada ya CHADEMA kujitoa.

Je, hawa ndio kinga ya ccm kitaifa na kimataifa kuhusu demokrasia ya vyama vingi?!

Tumeona hata vyombo vya habari kama radio na magazeti, kuna magazeti yanatuumiza kuhalalisha ukandamizwaji wa vyombo vya habari.

Kila wanapo banwa mbavu, huyataja yote kwa wingi wao, je hili lipo kwenye siasa za vyama pia?!

Kwanini leo, na siyo kabla ya CHADEMA kujitoa?!

Wanalipwa na serikali ya ccm?!

Hivi vyama hata mikutano ya ndani havifanyi, lakini leo ghafla wamejikusanya kutangaza kushiriki uchaguzi.

Hivi vyama hata uchaguzi wa viongozi wao hawafanyi, lakini leo ghafla hawa.

Karibuni tuwajadili hawa.

======

Screenshot_20191109-051900~2.png

Mwenyekiti wa DP, Abdul Mluya akizungumza na wanahabari

Vyama 11 vya upinzani visivyo na uwakilishi katika Bunge la Tanzania vimetangaza kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 vikieleza kuwa, “anayesusa chakula ameshiba.”

Dar es Salaam. Vyama 11 vya upinzani visivyo na uwakilishi katika Bunge la Tanzania vimetangaza kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 vikieleza kuwa, “anayesusa chakula ameshiba.”

Vimetangaza uamuzi huo leo Ijumaa Novemba 8, 2019 jijini Dar es Salaam siku moja baada ya Chadema kujitoa kushiriki uchaguzi huo kutokana na figisufigisu zilizofanyika katika uchukuaji, urejeshaji wa fomu za kugombea na uteuzi wa wagombea.

Vyama hivyo ni DP, NRA, AFP, Demokrasia Makini, UDP, ADC, Ada- Tadea, Sauti ya Umma (Sau), TLP, CCK na UMB

Vimesema vitashiriki vikiamini Wizara ya Tamisemi inayosimamia uchaguzi huo itatenda haki kwa kuwarejesha wagombea wake walioenguliwa kushiriki uchaguzi huo.

“Tunaamini watarudishwa kwa sababu wamekidhi matakwa. Tunataka tushindane kwa hoja na sera kwenye mikutano ya hadhara,” amesema katibu mkuu wa DP, Abdul Mluya kwa niaba ya viongozi wa vyama hivyo.

Amesema, “tutaendelea na uchaguzi kwa sababu siku zote anayesusa chakula ameshiba. Hatuwezi kususia uchaguzi kwa sababu ni mtaji wa kujiimarisha hasa kwa vyama hivi ambavyo havina diwani wala wabunge tofauti na Chadema.”

“Ili tuondokane na vyama vya mfukoni visivyo na nguvu njia sahihi ya kufanya ni kushiriki uchaguzi. Tushiriki uchaguzi ili kujenga mizizi kwenye Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ndio mtaji wa kupata wabunge,” amesema Mluya.

Chanzo: Mwananchi
 
Wewe ulitaka watoe lini tamko lao?

Kwa nini na wewe unataka kuwachagulia muda wa kutoa matamko yao?
Kama wanashiriki kulikuwa na haja gani ya kutoa tamko la pamoja kwamba wanashiriki?!

Kwani waliambiwa hawatoshiriki au wasishiriki?!

Kwapamoja, wanasimamisha wagombea wa muungano au kila chama kina mgombea wake?

Ikiwa kila chama kinasimamisha mgombea wake kwanini tamko la pamoja?!

Vinavyo jitoa ni sawa vikitangaza, lakini vinavyoshiriki vina haja gani kutangaza, si tutaona wakishiriki kampeni?!

Je, wanatumika na serikali ya ccm?!
 
Hivi ndio vile UMD, NRA, CCK, SAU ,TADEA, PONA, DP na vingine.

Hivi ndio mikoa ya ccm, wao ndio huibeba ccm kila
CHADEMA inapokataa kushiriki.
Nakumbuka waliitwa diamond jubilee baada ya uchaguzi wa 2015 kukubali matokeo baada ya CHADEMA kuyagomea.

Imetokea tena, leo wanatoa tamko la pamoja kushiriki uchaguzi baada ya CHADEMA kujitoa.

Je, hawa ndio kinga ya ccm kitaifa na kimataifa kuhusu demokrasia ya vyama vingi?!

Tumeona hata vyombo vya habari kama radio na magazeti, kuna magazeti yanatuumiza kuhalalisha ukandamizwaji wa vyombo vya habari.

Kila wanapo banwa mbavu, huyataja yote kwa wingi wao, je hili lipo kwenye siasa za vyama pia?!

Kwanini leo, na siyo kabla ya CHADEMA kujitoa?!

Wanalipwa na serikali ya ccm?!

Hivi vyama hata mikutano ya ndani havifanyi, lakini leo ghafla wamejikusanya kutangaza kushiriki uchaguzi.

Hivi vyama hata uchaguzi wa viongozi wao hawafanyi, lakini leo ghafla hawa.

Karibuni tuwajadili hawa.
1.Kwani waliweka wagombea nchi nzima? 2.Je wagombea wao hawakuenguliwa?
3.Je kama hawakuweka wagombea watashiriki vipi uchavuzi?
4.au zoezi LA kurejesha fomu linarudiwa??

Hebu nisaidie kujibu hayo maswali
 
Kama wanashiriki kulikuwa na haja gani ya kutoa tamko la pamoja kwamba wanashiriki?!

Kwani waliambiwa hawashiriki au wasishiriki?!

Kwapamoja, wanasimamisha wagombea wa muungano au kila chama kina mgombea wake?

Ikiwa kila chama kinasimamisha mgombea wake kwanini tamko la pamoja?!

Vinavyo jitoa ni sawa vikitangaza, lakini vinavyoshiriki vina haja gani kutangaza, si tutaona wakishiriki kampeni?!

Je, wanatumika na serikali ya ccm?!
Narudia kukuambia, kwa nini unavichagulia kazi za kufanya na wakati gani?

Wao wameamua kutoa tamko kuwa wanashiriki uchaguzi na wameamua kutoa tamko kwa muda ambao wao wanaona inafaa.

Kwenye hoja yako hii mwingine anaweza pia kusema, kwani kulikuwa na umuhimu gani wa CHADEMA kutoa tamko kwenye vyombo vya habari wakati wangeandika barua kwa watendaji wake au kuwapigia simu na kuwaambia wasishiriki kwenye zoezi la uchaguzi!

CHADEMA wameamua kutoa tamko na vyama vingine pia vimeamua kutoa tamko! Huu ndio uamuzi wao ambao haujavunja sheria za nchi!
 
Wanatangaza kushiriki uchaguzi wakati zoezi ni open kwa kila chama, wanaowatumia wanawapotosha
 
1.Kwani waliweka wagombea nchi nzima? 2.Je wagombea wao hawakuenguliwa?
3.Je kama hawakuweka wagombea watashiriki vipi uchavuzi?
4.au zoezi LA kurejesha fomu linarudiwa??

Hebu nisaidie kujibu hayo maswali
Hawakuweka wagombea popote, na katika report za matokeo ya vyama vilivyoshiriki nilizoziona mitandaoni hakuna wagombea wa hivyo vyama.

Hawakutoa wagombea hivyo hakuna aliyeenguliwa kwa upande wao, lakini nashangaa kuona wanasema watashiriki, kivipi? Au wataongeza majina ya wagombea wao leo na kesho?!

Watarudisha form gani kama hawakuchukua form za kuomba kugombea?!

Wao wanadai uchaguzi huu ni HURU na HAKI, kwani umeshafanyika, hadi watoe tathmini hiyo?!

Tumeona wagombea wa chadema, wakinyimwa form, na waliopewa hawakuteuliwa na wengine kuenguliwa kabisa.

Lakini hawa wao hawakushiriki kabisa tangu mwanzo, hawakuhamasisha wananchi kujiandikisha, na hawakutoa wagombea, hakuna record zao popote watashiriki vipi.

Je, wanatumika na serikali ya ccm?!
 
Narudia kukuambia, kwa nini unavichagulia kazi za kufanya na wakati gani?

Wao wameamua kutoa tamko kuwa wanashiriki uchaguzi na wameamua kutoa tamko kwa muda ambao wao wanaona inafaa.

Kwenye hoja yako hii mwingine anaweza pia kusema, kwani kulikuwa na umuhimu gani wa CHADEMA kutoa tamko kwenye vyombo vya habari wakati wangeandika barua kwa watendaji wake au kuwapigia simu na kuwaambia wasishiriki kwenye zoezi la uchaguzi!

CHADEMA wameamua kutoa tamko na vyama vingine pia vimeamua kutoa tamko! Huu ndio uamuzi wao ambao haujavunja sheria za nchi!
CHADEMA walifanya hivyo kuwataarifu wagombea wao waliokuwa wamekata rufaa na waliojiandaa kukata rufaa wasifanye hivyo tena, na kuwahabarisha wanachama wao kwamba uongozi wameamua kutoshiriki uchaguzi kurosawa na kasoro zilizojionyesha mpaka muda huo. Na huo ndio ulikuwa msingi wa tamko lao.

Hivi vyama havikuwa na sababu ya kutoa tamko, wengeenda kupiga kampeni, na kila chama kina wagombea wake, kama wapo kweli, kwanini tamko la pamoja?!
 
Hawakuweka wagombea popote, na katika report za matokeo ya vyama vilivyoshiriki nilizoziona mitandaoni hakuna wagombea wa hivyo vyama.

Hawakutoa wagombea hivyo hakuna aliyeenguliwa kwa upande wao, lakini nashangaa kuona wanasema watashiriki, kivipi? Au wataongeza majina ya wagombea wao leo na kesho?!

Watarudisha form gani kama hawakuchukua form za kuomba kugombea?!

Wao wanadai uchaguzi huu ni HURU na HAKI, kwani umeshafanyika, hadi watoe tathmini hiyo?!
Tumeona wagombea wa chadema, wakinyimwa form, na waliopewa hawakuteuliwa na wengine kuenguliwa kabisa, wao hawakushiriki kabisa tangu mwanzo, hawakuhamasisha wananchi kujiandikisha, na hawakutoa wagombea, hakuna record zao popote watashiriki vipi.

Je, wanatumika na serikali ya ccm?!
kwa mujibu wao kushiriki sio lazma kuweka wagombea
 
Hebu waulize ikiwa kushiriki uchaguzi ni haki ya kila chama ni chama gani kiliwahi kutangaza kushiriki uchaguzi?

CCM wametangaza kushiriki uchaguzi? ACT nao wametangaza?

Ni mtu mwenye utimamu wa akili tu anayeelewa kushiriki uchaguzi sio habari bali kutokushiriki ndio habari.
 
Anataka vyama vyote viendeshwe na kamati kuu ya chadema.
Hapana, nilitaka kufahamu kama wana wagombea wa muungano au kila chama kina wagombea wake?!

Tamko la nini ikiwa wanashiriki uchaguzi?!

Tunafahamu uchaguzi upo na vyama vyote vitashiriki, isopokuwa CHADEMA waliojitoa, sasa tamko la nini?!
 
Ni haki yao kama wameridhika na mchakato.
Mchakato ulikuwepo tangu mwanzo na haujafutwa. Vyama vyote vinashiriki, wao hawajajitoa na hakuna aliyesema wamejitoa, kwamba ilibidi wakanushe. Sasa msingi wa tamko lao ni upi?!
 
Back
Top Bottom