Vyakula vya watu wa mikoani vimenivutia sana

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
542
733
Miezi saba iliyopita nilianzisha makazi mapya katika moja ya mikoa ya hapa nchini, nipo eneo la mjini lakini ukienda cafe kupata chakula vyakula kwa sehemu kubwa ni vya asili tena kama wewe ni mtumiaji wa ugali wa sembe utakufa kwa njaa na hauta upata, ukiagiza ugali unaletewa dona tena dona lililofurika chomboni na endapo hautamaliza au kuacha watu wanakushangaa sana tena wanaweza kukupa pole kwani wataamini unaumwa na huku yeyote anayebakiza chakula tena awe ni mwanaume huwa ni mwenye tatizo la afya, yaani mgonjwa.

Nitumie fursa hii kuwapa pole wale wanaume kutoka moja ya majiji makubwa hapa nchini kwani najua wasingeweza kula hata robo ya chakula cha huku mkoani, huku chakula hakiwekwi kwenye poti na ikitokea kikawekwa basi ni cha mtu mmoja sio kwa familia nzima kwani utasababisha watu walale na njaa zao.
 
Dona kambale chukuchuku hebu jaribu kisha tuletee mrejesho !!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom