Vyakula vya ajabu nilivyowahi kula

kuna kijiji nimekaa kina wawindaji haramu wao huwinda nchi jirani
huko nimekula twiga&punda,punda milia ngiri, sana tu
 
1. "Kombucha tea"(fungus tea) nilishawahi kunywa sana ina kauchachu flani siku hizi haipatikani sana.

2. "Mbesi" samaki alieoza au kuchina analiwa sehemu za Ifakara

3."Dadii" pombe ya kienyeji ya sehemu za Arusha.Unakunywa unalewa na unashiba.
Dadii Ni pombe ya kwetu uchagani,inatengenezwa na mahindi ipo Kama uji
unashiba kabisa
 
"Hata Nguruwe huwa ana swih mbele ya njaa ya kufa"

Hii kauli niliwahi kumsikia Fid Q kwenye moja ya nyimbo zake, kitambo kidogo.

Muda huo nakula ugali wa kengele, yani dereva wa sahani break mkeka.

Nilipo kuwa nausikia mstari huu, kila siku nilikua najisea kua hata iwe vipi sintokuja kula nguruwe, sababu jamii yangu, dini yangu hairuhusu kula nguruwe.

Miaka mingi imepita, ule ugali wa kengele umeota mbawa, nasasa ni mwendo wa asie fanya kazi na asile, yani ni Jitegemee sio makongo tena.

Katika kujitafutia mwenyewe riziki ndipo sasa nakubaliana na msemo wa fid q " hata nguruwe huwa anaswih mbele ya njaa ya kufa" baada ya kukutana na nyakati ngumu za utafutaji riziki (hususan chakula)

Leo nataka niwashirikishe, ama niwahabarishe vyakula vya ajabu nilivyo wahi kula, ambavyo sikutegemea kama nitakuja kula kwenye maisha yangu.

1- PANYA
Ebwana eh, Mndengereko ukitaka akunyime maji basi atambue kua wewe ni mla panya.

Kwetu panya aliwi kabisaa tena ni kinyaa, lakini mimi nimekula.

Nakumbuka ilikua mwaka 2018, nikiwa nachimba poli la Nacoja (inasomeka nakocha)

Kulikua kuna nyumba moja hivi, ya bibi yangu wa kimakua, huyu alikua mganga, nilikua nikitoka Nanhupo (ninapo ishi) lazima nipite hapo kijijini (Nacoja) kwa huyu bibi, nioge dawa ndio niingie polini (mgodini)

Mazoe hayo yalipelekea pale nyumbani kwa yule bibi nichukuliwe kama mwana ndugu, kwani nilipo kua nafika hapo nyumbani lazima nibebe vijizawadi.

Siku moja, nimetoka zangu polini mida ya jioni, jua lishazama, nikaona kwa muda huu siwezi kupata piki piki ya Nanhupo, nikaamua kulala pale kijijini kwa yule bibi yangu.

Hii si mara yangu ya kwanza kulala hapa. Ni nyumba kubwa yenye wanafamilia wengi, pia kuna mtoto mmoja wapo wa yule bibi ni lika langu, hivyo huyu bibi alikua anani chukulia kama mwanae tu.

Niliingia pele, nikamkuta dada mkubwa yuko jikoni anaandaa ugali, nikamsalimia, nikaingia chumbani kubadili nguo za kazi.

Mara haukupita muda mrefu, nikaitwa kwa ajili ya kula. Sahani yetu ilikua ya watu kama wanne hivi, akiwemo yule mtoto wa kiume wa yule mama na watu walio nizidi umri kama wawili hivi.

Kabla ya kuanza kula yule mshikaji wangu, akaniuliza "unaaliya mavala?" akimaanisha kua ninakula panya, nikamjibu ndio.

Neno mavala mimi nikahisi kaniuliza kama nina kula mbawala, hivyo nikamjibu ndio. Nikawanawa maji na show ikaanza.

Matonge kama manne matano, mara, mmoja wa wale wazee akazama ndani ya bakuli nakutoa kitoeo na kukiweka kwenye sahani, amadi nakuta panya katula, mkia huo.

Kidogo nitapike lakini nikajikaza kisabuni, kwanza nijiuliza kama nitanawa maji, wenyeji wangu wangenichukulia vipi? tena ukizingatia walisha niuliza. Nikaona sio poa, na mimi nika kamata wakwangu nikaweka pembeni. Kwa kweli nilijilazimisha mpaka nikammaliza.

Miaka miwili sasa tangu tukio hilo kupita, cha ajabu nimekua nawapenda panya kufikia mpaka nawalipaga watoto waende wakanichimbie huko mapolini.

Panya ananoga ukimkaanga na Mafuta kisha ukapata kachumbari na pili pili nyingi, mbele yako upo ugali wa muhogo.

Kwa hapa Tete panya anauzwa kwenye sahani kama samaki wa kukaanga, haiwezi pita week bila kula panya. Kiufupi panya ni mtamu na najuta kuchelewa kumjua.

2- CHURA
Hii ilikua huko huko polini Nacoja, tafauti ni kua huku sio kijijini bali ni porini.

Polini kula vitu vya ajabu haishangazi lkn si wote wanaokula vitu vya hovyo.

Binafs nilikua nina kinyaa sana kula vitu vya hovyo lkn kubanwa na njaa usiombe.

Kuna nyakati ufanyaji wetu wa kazi hupitiaga nyakati ngumu sana , hasa kiangazi, tena zaidi ni kuanzia mwezi wa kumi, kumi na moja na mwanzoni mwa mwezi wa kumi na mbili.

Narudi muda si mrefu
Kwahyo mkuu panya unapiga fresh kabsa saizi na kuwasifia juu yaani
 
😂😂 eti panya mtamu na najuta kuchelewa kumjua..🤣🤣Yani wewe..khaa
 
Njoo umalizie ndugu
 
Niliwahi kula nyoka asiejulikana bila kujua kwa kumchanganya na samaki ucku tulipokua kwenye shughuli za uvuvi tulikuja kugutushwa na mshkaji mmoja aliekuja asubuhi na kutaka tumwachie amalizie ile supu sasa alipokua amefika mwisho mwisho c akanyanyua na sufuria ili apige ile supu tarumbeta ndipo akaona ngozi ngozi na kichwa dah jamaa alimaind kishenzi akizani tumemtegeshea dah
 
Back
Top Bottom