Vyakula vinavyoongeza uwezo katika tendo la ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyakula vinavyoongeza uwezo katika tendo la ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Felixonfellix, Mar 25, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Aina 10 ya vyakula vinavyoongeza uwezo katika tendo la ndoa

  Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.

  Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:

  PILIPILI
  Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.

  PARACHICHI
  Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.

  NDIZI
  Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.

  CHOKOLETI
  Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake, jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa mawazo.

  CHAZA NA PWEZA
  Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.

  POMEGRANATE
  Ni aina fulani ya matunda mekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.

  MVINYO MWEKUNDU
  Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo.

  MBEGU ZA MATUNDA
  Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.

  VANILLA
  Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni TIKITI MAJI ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa.
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  naona umetaja zaidi mboga na matunda; vyakula sijaviona hapa ama ni mimi tu ndio sielewagi?
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Umesahau Mhogo na karanga hapo.
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Asali na mayai ya kuchemsha je?

  Fidel mwana upo; nilijua tropiki hii itakugusa tuu!
   
 5. Sydney

  Sydney Senior Member

  #5
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kweli? Na kama ni kweli kuna ulazima wowote? jamani mh!
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  M barikiwe sana watu wa mungu, daktari sio lazima uwe na PHD (pure head damage) bali hata akina sie tunaunganisha ma miti tunayo ijua na matunda maisha yanaendelea. Kwani zamani babu zetu waliishije? ofukozi waliugua na walijua miti ya kuwatoa kwenye matatizo waliokuwemo.
   
 7. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Kuhusu nini? ; nimeshindwa kuelewa nikusaidieje kujibu!
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, upo sahihi kabisa.
  Lakini amesahau na vinywaji pia....sio mboga na matunda pekee!
  Muulize Fidel hapo kwenye kinywaji!
   
 9. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,016
  Trophy Points: 280
  Asali ni muhimu sana
   
 10. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,016
  Trophy Points: 280
  Swali ni kwa wanaume tu au na wanawake pia?
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  kwani wanawake wanahitaji nguvu?.jamaa amesema uwezo, sasa uwezo si mpaka jogoo aweze kupanda mtungi?

  wanawake wanahitaji nini ili bibi afunguke?
   
 12. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Fidel kwa idhini niliyopewa na kamanda bigirita naomba utupangie safu ya vinywaji:D
   
 13. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,016
  Trophy Points: 280
  Kama hawahitaji nguvu basi wana raha sana, kweli mwanaume mateso
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Asali inahusika; ICU wewe unaitumiaje hii?
   
 15. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,016
  Trophy Points: 280
  Bibi ndio nini au nani? Mayelo
   
 16. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,016
  Trophy Points: 280
  Unakunywa kijiko kimoja asubuhi na kingine usiku. Unaweza pia kutumia kwenye chai asubuhi
   
 17. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Ni ile tropic tuliyoisoma kwenye jiografia,yaani tropic ya kansa au?
   
 18. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Sasa hii ukiichanganya na vitunguu swaumu mambo yanakuwa swadakta!!
   
 19. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Matumizi ya asali na kiini cha yai!

  Unachemsha yai na uondoa lile ganda jeupe unabakiwa na kiini chake tu;

  Saga kiini cha yai kwenye kisosi kwa kutumia kijiko ama kisu cha mkate; pima asali yako vjiko vinne vya chakula weka ktk kikombe

  miminia kiini kilichosagwa kwenye hicho kikombe na ukoroge upate ute mzito; kama uanwasi wasi waweza kupaka hii kwnye mkate lakini yapendea ukiila jinsi ilivyo!

  Ni sextiser ya kumfa mtu hiyo!
   
 20. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #20
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Niliweka makusudi kumnasa fidel; n wei si unajua darasani kwetu wanafunzi 120 mwalimu mmoja asa akitamka topic unasikia kama tropic na akitamka beep inasikika kama dip!:D
   
Loading...