Vyakula vinavyosababisha kitambi

Won mawila

Member
Mar 7, 2019
83
56
Habar wakuu

Hivi ni vyakula vya aina gani nivitumie nipate kitambi kidogo hata cha kuzugia msaada tafadhari.

==========

Kitambi (kilibatumbo) ni tumbo kubwa ambalo linachomoza kwa mbele na wakati mwingi kuning'inia isivyo kawaida. Ni ugonjwa kama magonjwa mengineyo na huweza kuwakumba watoto, vijana, watu wazima na hata wazee wa jinsia zote!

Kwa baadhi ya watu, hukichukulia kitambi kama ishara ya ufanisi au mafanikio kwa mhusika katika nyanda nyingi za kijamii. Ni imani ambayo kwa namna moja ama nyingine inachekesha kwakuwa kilibetumbo ni ugonjwa kama magonjwa mengine.

Mwili wa binadamu una seli bilioni 50-200 za mafuta zilizogawanyika kwenye mwili wa binadamu. Kwa wanawake zipo sana maeneo ya matiti, nyonga, kiunoni na kwenye makalio. Kwa wanaume seli zipo sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio.

Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili, ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi na ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

Sababu za kupata kitambi

Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori), mtu kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

Vyakula vinavyochangia uongezekaji wa kilibetumbo ni pamoja na nyama (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga (chips), pizza, vyakula vyenye wanga mwingi kama ugali wa mahindi, mihogo, wali, mikate myeupe na pia viazi vya mviringo. Ndizi pia huchangia!

Sababu nyingine ni kuwa na chembe za urithi za unene kutoka kwa wazazi, pia kuna sababu za kimazingira. Ila pia kuna sababu nyingine zisizojulikana.

Jinsi ya kujua kama una kitambi

Kitambi kinaweza kuonekana kwa kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno(waist) na nyonga (hips). Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au 40 in kwa wanaume na >88 cm au 35 in kwa wanawake, na uwiano wa kiuno na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake.

BMI ya 30 au zaidi inaashiria 'Obese' uzito kuzidi kiasi. Kuwa na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki, kuliko hata cha BMI.

Kipimo kingine cha kitambi ambacho kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu.

Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.

Njia za kuondoa kitambi
  • Mlo mzuri kiafya ndio ufunguo wa kupunguza uzito na kutoa kitambi. Kuacha kula vyakula vinavyotia nguvu sana, vyenye mafuta na sukari nyingi ndio msingi wa kuondoa kitambi. Hii husaidia mwili kutumia mafuta yaliyo mwilini kutengeneza nguvu hivyo kupunguza mafuta na kuondoa kitambi. Aidha, punguza matumizi ya vinywaji vyenye sukari kwa wingi na tumia samaki badala ya nyama.
  • Kufanya mazoezi ya mwili kila siku kwa dakika 30-60 walau siku 3 ndani ya juma (week) moja (Mfano kuendesha baiskeli na kukimbia).
  • Dawa ni muhimu tu kama una matatizo mengine kama kisukari, mfano dawa fulani za kisukari zinaweza kukusaidia kupunguza mafuta yanayozunguka ogani muhimu kama ini na kongosho.
  • Kufanya upasuaji mkubwa ili kupunguza mafuta, hii hufanyika kwenye nchi zenye teknolojia kubwa na hii hushauriwa endapo mafuta yaliyomwilini yamesababishwa na magonjwa yameshindwa kupungua kwa njia ya rahisi ya kawaida.
Imedhihirika pia kudhibiti 'Stress' inaweza kusaidia kwenye kupambana na kitambi.

Michango ya wadau
Tafuta pesa mkuu, automatically kitakuja.

Anyway jenga mazoea ya kinywa supu tena ile yenye mafuta na nyama zenye mafuta na vinywaji baridi kila mara. (Vyenye sukari nyingi)
----
Baba la baba Kula Carbohydrates za kushato, Fats , Protein .

Yaani kunywa bia ikiwezekana Ungana na Nguruwe/Noah/Mbuzi katoliki kula yale makapi ya Bia/Shayiri iliyochacha (Fermented) Kula Ugali nyama choma,Shushia na serengeti 5 kila siku mchana, .

Nenda kwa nka massaweeew kunywa mbege kula mbege mnama, within 2 months

Kitambi utakuwa nacho
----
Fanya hivi. Kula ugali mkubwa sana na nyama choma au samaki wa kukaanga wa kulumangia na kachumbari. Jioni kula wali mwingi, hakikisha kipimo chako cha chakula kinaongezeka kidogo.

Asubuhi kula vizuri. Piga supu na vyapati vingi na hakikisha unakunywa maji ya kutosha. Hakikisha hujisikii njaa wakati wote.

Kama ni mkristo kula nguruwena bia atleast bia 2 nzito. Yaani zenye ule uzito wa yale maji....kama vile Castle Milk Stout.

Njoo hapa baada ya mwezi.
----
Mmh! nakuheshimu ila kwa hili Umenichosha best?

Sipend Men mwenye kitambi?
Yan kaz hawawez kabisa.
Nina Experience nao for a while ( I had meet various men with Kitambis from different Angles/location and I found Mostly have poor performance on Bed while Financialy fit)

Napendelea Man awe simple Portability na siyo Mtambi/Obesity hivyo plz naomba ufanye mazoez na uachane na hiyo tamaa ya kuwa na kitambi.

Mostly Vitambis/Obesity(Body max Index) people has tendence of high cholestral,Diabetes,Pressure,Lack of Exercise

"SAMAHAN LAKIN"
 
Habar wakuu

Hivi ni vyakula vya aina gani nivitumie nipate kitambi kidogo hata cha kuzugia msaada tafadhari.
Hahahaahh unataka kitambi cha kufutia kioo cha smartphone au sio??? Tahadhari inadaiwa vinapunguza ufanisi wa tendo

Kula wanga kwa wingi,,, unaeza kujifunza zaidi kupitia insta, fb, YouTube channel Dr Boaz Mkumbo MD
 
Fukia ugali na wali kwa wingi bila kusahau products za ngano kama bia, vyapati, maandazi na gonga sana chai na soda halafu baada ya mwezi leta majibu.
 
Baba la baba Kula Carbohydrates za kushato, Fats , Protein .

Yaani kunywa bia ikiwezekana Ungana na Nguruwe/Noah/Mbuzi katoliki kula yale makapi ya Bia/Shayiri iliyochacha (Fermented) Kula Ugali nyama choma,Shushia na serengeti 5 kila siku mchana, .

Nenda kwa nka massaweeew kunywa mbege kula mbege mnama, within 2 months

Kitambi utakuwa nacho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta pesa mkuu, automatically kitakuja.
Anyway jenga mazoea ya kinywa supu tena ile yenye mafuta na nyama zenye mafuta na vinywaji baridi kila mara. (Vyenye sukari nyingi)
Asante mkuu napenda sana vinywaj baridi ila hapo kwenye sukari kali ndo shida sasa
 
Back
Top Bottom