Vya vya siasa na ukombozi wa pili wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vya vya siasa na ukombozi wa pili wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eiyer, May 10, 2011.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Kwa yeyote mwenye mapenzi ya kweli na nchi hii atakubali kuwa nchi hii inahitaji ukombozi mpya kutoka kwa wakoloni weusi ambao mfumo wao ni wa utawala ni mbaya kuliko hata wakoloni weupe,unapozungumzia ukombozi ni wazi unazungumzia mabadiliko ya maisha ya wananchi yatakayoongozwa na dhamira ya ukweli kutoka moyoni mwao,lakini lazima kuwe na kiongozi wa kuwaongoza watanzania,ndio hapo matatizo na tofauti za kimtazamo ya vyama vya siasa tulivyo navyo,ninaamini ili tuikomboe nchi yetu ni lazima tuwe wakweli na uchungu wa kuboresha maisha yetu kutoka ndani ya mioyo yetu,tuwe kitu kimoja,vyama vya siasa kama vile cuf kubadilika na kuwa pamoja na ccm ni jambo la kusikitisha sana,nchi haitakombolewa kwa style hii,vyama vyote vya upinzani vinatakiwa vitambue kuwa chadema ndio chama kinachokubalika zaidi kwa sasa kutokana na sera yake ya kujitambulisha na wanyonge,hivyo vyama hivyo vinatakiwa kuanzia bungeni mpaka nje ya bunge viwe na sauti moja,ingependeza kama vyama vingine vingekuwa bega kwa bega na chadema kuanzia kwenye maandamano ya kupinga mfumuko wa bei mpaka leo kwani yanayozungumzwa kwenye maandamano ndo kilio kikubwa cha wananchi na ndo mtazamo wa kila mtanzania mwenye nia njema na nchi hii,tukiweza umoja tutakuwa tumemshinda adui kwenye eneo muhimu sana,SAA YA UKOMBOZI IMEFIKA
   
 2. O

  Omr JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo ni mawazo yako wewe kibaraka wa CDM
   
Loading...