Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 54,784
- 27,562
Kikwete ashtushwa kifo cha Ballali
*Safari yake yaishia makaburi mbali na kwao
Na MWANAHALISI JR
RAIS Jakaya Kikwete ametoa rambirambi kwa familia ya marehemu Dkt. Daudi Ballali, ambaye alitarajiwa kuzikwa jana mjini Washington DC Marekani na kueleza kushtushwa na kifo hicho.
Kwa mujibu wa taarifa yake iliyotolewa na Ofisi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alielezea kupokea taarifa za kifo cha gavana huyo wa zamani wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) kwa masikitiko makubwa.
"Wakati huu mkijiandaa kwa mazishi yake baadaye leo (jana), napenda kutumia nafasi hii kutoa mkono wa rambirambi kwenu na kwa ndugu zenu wote," alieleza Rais Kikwete katika taarifa hiyo na kuwatakia faraja katika wakati huu mgumu.
"Naungana nanyi katika wakati huu mgumu wa majonzi makubwa kutokana na msiba mkubwa uliowakuta," alisema.
Rais Kikwete, alisema Tanzania inaelewa familia hiyo imepata uchungu mkubwa kutokana na kuondokewa na mpendwa wao na kiongozi wa familia.
"Ni Kazi ya Mungu haina makosa, tunawatakia mazishi mema, tuzidi kumuombea marehemu, apate mapumziko mema," alisema Rais Kikwete katika taarifa hiyo.
Wakati huo huo baadhi ya ndugu wa marehemu Ballali jana waliendelea kushikilia msimamo wao wa kutaka mwili wa ndugu yao urejeshwe kuzikwa nchini.
Taarifa ambazo Majira ilipata jana jioni zilieleza kuwa ndugu hao walisisitiza ndugu yao arejeshwe na kuzikwa kijiji kwake Lunganga , Mufindi mkoani Iringa.
Hata hivyo utashi wa ndugu hao waliobaki nyumbani, inaelekea ulizidiwa nguvu na kile kilichoelezwa, wosia wa Dkt. Ballali aliouacha wakati wa uhai wake ambapo alisema akifa azikwe Marekani kwa kile alichoeleza kuchafuliwa jina lake kutokana na kashfa ya EPA.
Dkt. Ballali alikaririwa akiweleza baadhi ya ndugu zake kwamba alilitumikia Taifa kwa uadilifu mkubwa na hakuwahi kuiba hata senti moja na kwamba kashfa hiyo imemchafua kwa kiasi kikubwa.
Katika hali iliyoonesha kuwa mazishi ya gavana huyo jana yalifanyika katika mazingira ya faragha kubwa, mawasiliano ya vyanzo vyetu mjini Washington DC hayakupatikana kirahisi na simu zote zilikuwa zinatumika wakati wote.
Hata hivyo wakati tukienda mitamboni chanzo hicho kimoja kilithibitisha kwamba maandalizi ya maziko hayo yalikwisha kamilika zikiwemo taratibu za kufanyika misa kwa ajili ya kuombea mwili wa marehemu na utoaji wa heshima za mwisho katika kanisa Kuu la Mtakatifu Stephen Martyr 2436 Pennsylvania Ave, NW Washington DC 20037.
Kilidokeza kwamba mazingira ya awali yalionesha kuwa wanaotakiwa kuhudhuria mazishi hayo ni watu wachache wakiwemo ndugu, wafanyakazi wenzake na marehemu Ballali waliowahi kufanya kazi alipokuwa Shirika na Fedha Duniani (IMF),Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Bw.Ombeni Sefue na Watanzania wachache wanaishi mjini Washington DC.
Chanzo hicho kilisema kwa mujibu wa saa za Marekani, ratiba ya mazishi hayo ilitarajiwa kuanza saa nne kamili asubuhi na baada ya hapo ndipo mwili huo ungepelekwa kwenye makaburi ya Wakatoliki ya Get of Heaven, eneo la Silver Spring, MD kwa mazishi.
Hadi tunakwenda mitamboni ilikuwa haijafamika kwamba mwili wa Dkt. Ballali utachomwa moto au utazikwa kiafrika kwa kuteremshwa kaburini kwasababu huduma zote mbili zinakubalika katika makaburi hayo.
Ikiwa Dkt. Ballali atachomwa moto majivu yake hayataruhusiwa kugawanywa bali yatateremshwa kaburini kwa mujibu wa taratibu za kikatoliki