gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,274
- 20,673
Nimatumaini yangu kwamba nyote mu wazima wa afya, lakin pia napenda kutoa pole zangu nyingi sana kwa mpendwa wetu mtangazaji wa ITV ufoo Saro kwa dhahama iliyomkuta. Pole sana na Mungu akuafu mpendwa.
Kwa muda mrefu kidogo mkoloni wangu amekuwa akinutuma kwenda kukaa kijiwen kuhesabu magari, nimekuwa nahangaika toka kijiwe kimoja kwenda kingine ili tu niweze pata data anazo taka huyu mkoloni.
Katika peke peke zangu hizo nimegundua jambo moja kubwa ambalo nafikiri labda halijakuwa addressed vyema, ama liko addressed lakini utekelezaji wake ni mbovu na hauna ufuatiliaji.
Sote tunajua vyema kwamba harakati za kumkinga mtoto na maabukizi ya VVU toka akwa mama ziliaza miaka ya 2005 hivi kwa hapa kwetu. Nyuma ya hapo ilikuwa kwamba mama akiwa muathirika basi atamzaa mtoto muathirika na wala haikupewa kipaumbele kwamba mtoto huathirika kivipi ama wakati gani, ingawa pia ilikuwa inajulikana wazi kwamba hakuna mahusiano yeyote kati ya damu inayozunguka mwilini kwa mama na ile inazunguka kwa kijusi. Hali hii ya kutojua mtoto akingwe vipi ilipelekea watoto wengi wanaozaliwa na mama wenye VVU Wazaliwe wakiwa tayari ni waathirika wa VVU.
Hata hivyo kampeni nyingi sana zilijitokeza za kukinga maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto na hivyo kupunguza chances za mtoto kuzaliwa na VVU hata kama mama ni muathirika ingawa pia hii hai-garantee kwamba mtoto huyu aliyesalimika akiwa tumboni hadi kuzaliwa, hata weza kuambukizwa na mama yake wakati wa makuzi hasa kipindi cha kumyonyesha. Elimu juu ya unyonyeshaji wa mtoto anayezaliwa na mama mwenye VVU hutolewa bure kwa wamama ili tu kupunguza ile mianya michache iliyobaki inayoweza kumsababisha mtoto kupata maambukizi. Harta hivyo huu sio msingi wa mada yangu hii kwa leo.
Leo ninataka kujadili kidogo ama kwa upana juu ya utunzwaji wa watoto ambao tayari wana VVU. Kwanza kabisa naomba wazazi tuelewe kwamba watoto hawa hawana makosa na wala wewe mzazi pia haikuwa nia yako kumuambukiza huyu mtoto VVU hivyo usijilaumu kabisa kwa hali hii na kuamua kuificha.
Mathalan kwa hapa DSM siku ya ijumaa ndio siku ambayo imewekwa na CTC kwaajili ya kliniki ya watoto wenye VVU. Jambo la kushangaza kabisa ni kwamba siku hii ukienda kwenye vituo utakuta wazazi wanaoleta watoto wao kliniki ni wachache sana kuliko hata ilivyotegemewa.
Jambo la kushangaza zaidi siku ya Kliniki za watu wazima utakuta folen hadi unakosa pa kukanyaga. Sisemi kwamba idadi ya watoto wenye VVU ni sawa na ya watu wazima la hasah lkn namaanisha kwamba wale wachache wenye VVu huwa hawaletwi klinik wala hawaanzishiwi dawa mapema.
Hali ni mbaya zaid kwa wale ambao wana miaka kuanzia 7-hawa wazazi wao walishawakatia tamaa kabisa na huwa wanawatibu kienyeji (sina maana ya ugaga) yaani mtoto akiumwa mama atasema ni malaria atampeleka zahanati atapimwa malaria akikutwa nayo bas atapewa dawa za malaria basi, kesho akiumwa tena mama ataona uvivu atampa dawa anazojua last time alitumia mchezo umeisha.
kwa hali hii hupelekea watoto hawa kuripotiwa kuwa HIV+ wakiwa tayari wana hali mbaya sana. nimeshuhudia mwenyewe watoto wengi wakipelekwa hosp tayari wakiwa na MENINGO ama Toxo na tena hawa unakuta toka siku wanapata TB mpaka inaadvance inakuja kuwa relapse TB bado wazazi wanakuwa wagumu kukubali kuwapima HIV. hii haitoshi wazazi hawa hushuhudia watoto wao wakipoteza maisha kwa ajili ya uoga usiokuwa na tija.
Sababu kubwa ambayo niliipata kwamba kwann wazazi huogopa kumpima mtoto niliambiwa ni AIBU kwamba wazazi huona aibu lkn nikajiuliza hivi aibu hii haitawapata pindi mtoto atakapougua kiasi cha kumletea umauti??
Dr mmoja aliniambia wazi kwamba baadi ya wazazi hasa wamama hudiriki hadi kuongopa history ya ugonjwa wa mtoto hivyo kum-mislead Dr. sasa je hapa unampoteza Dr ama mtoto??
lakini pia nimegudua sheria zetu nazo zinahitaj marekebisho kwamba Dr aruhusiwe wakati fulan kuwa na maamuzi ambayo hata kama mzazi hayakubali lkn yanalenga kuokoa uhai wa mtoto basi ampime huyu mtoto.sion kama kuna faida kufuata msimamo wa mzazi wakati mwili unaoumizwa ni wa mtoto asiye weza kujisemea kwa kipindi hicho na pengine angepewa nafasi ya kujisemea basi angeweza kusema tofauti na mzazi anavyotaka.
Hebu basi wazazi waache ubinafsi waone ukweli watoto wao nao wanahitaj kufurahia maisha kama wao. wakubali matokeo jaman wawapeleke watoto Kliniki wakapimwe na wawe tayari kuwapa dawa. Naumia sana nionapo msururu mrefuuu wa watu wazima wakichukua dawa huku wakiwa wamewafunga watoto ndani eti wanakwepa aibu.
Wasalaam