VUVUZELA na Ari zaidi, Kasi Zaidi na Nguvui zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VUVUZELA na Ari zaidi, Kasi Zaidi na Nguvui zaidi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bigirita, Jun 22, 2010.

 1. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Nikiwa mdogo, mjomba wangu aliwahi kuniuliza, ninapenda kifaa gani kizuri cha muziki? mimi kwa kuwa nilipenda filimbi nikasema filimbi ndo kifaa kizuri, akaniuliza kwa nini? nikasema kwakuwa kinatoa milio tofauti kwa nyimbo tofauti.

  Mjomba akaniangalia usoni, akaniambia, hiyo ni milio tofauti au mlio ule ule katika ala tofauti?

  Akasema, kama ni mlio tofauti, basi filimbi ingeweza kutoa mlio wa ngoma. Nikagundua busara ya mjomba. Nikanyamaza.

  Haya ya JK na milio ule ule kutoka kwenye VUVUZELA linalotoa mlio wa kati yanakubalika kwa wananchi? Kama VUVUZELA alilotumia 2005 halikuweza kuwaburudisha watanzania, anauhakika gani kwamba, wimbo ule ule kwa kuongeza neno zaidi kutoka katika VUVUZELA lile lile, utawaburudisha watanzania wasio na maji, uhakika wa chakula, uhakika wa matibabu, elimu bora, barabara, pembejeo za kilimo n.k.??

  Tutafakari!!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Bigirita,..Kama wasomi wa vyuo vikuu ndio wanaopita kumtafutia wadhamini nchi nzima, unategemea ni nani atasimama kidete kumkosoa huyu mtu?...Mentors wa nchi wanaacha taaluma zao na kugombea ubunge huku wakiimba na kucheza vuvuzela hili la KASI MPYA...Unategemea nini?...Habari kamili tutaiona safari kwenye 2nd phase ya awamu yake!
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hii nchi sijui wanatupeleka wapi. Wengi wetu hatutaki kuona kuwa hakuna jipya ndani ya hawa jamaa. Tukipewa kanga, kofia au t-shirts tunawapigia kura hafu tunaumia miaka mkitano. Endeleeni kuwachagua tu!
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu!! inasikitisha sana! Ninashangaa CCM kusema imejenga shule za sekondari, wakati mama yangu alinipigia simu siku moja akaniambia anatakiwa kwenda kukusanya mawe, asipokwenda inabidi alipe fine, hivyo alikuwa ananiomba nimpe hela alipe ili asiende kubeba mawe kwani afya yake sio nzuri.
  SASA CCM ndo imejenga au wananchi wamejenga?
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba watanzania hawachagui kwa kusikiliza sera za mgombea na kumpima kama anayoyasema ana uwezo nayo. Nimesikiliza kwa makini na kusoma kwenye magazeti leo mipango na malengo ya CCM 2010-2015, kwa kweli ni nzuri na kama ikitekelezwa ipasavyo Tanzania itakuwa kama Botswana.

  TATIZO kubwa ni kwamba HAITATEKELEZWA, mtu akiniambia ile ya 2005-2010 imetekelezwa (hata kwa angalau 50%) nitajua kwamba Tanzania ni nchi pekee ambayo unaweza kuleta maigizo kwenye siasa na ukafanikiwa. Ukadanganya na usishitakiwe!
  Kwangu mimi maendeleo ninayoyaona wazi ni uhuru wa vyombo vya habari, ingawaje hii si kwa sababu ya serikali ya CCM, ni wakati wake ninajua hawataki kusemwa tunavyowasema lakini hawawezi kwa sababu teknolojia imewaacha nyuma.
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kama unakumbuka Jenista Mhagama, alimbwatukia waziri wa TAMISEMI kuwa hajui anachokifanya na hajafanya chochote ndani ya miaka mitano, lakini, huyo huyo akiulizwa CCM imefanya nini atasema imefanya mambo kibao..........atajisahaulisha kabisa kuwa kuna wafanyakazi ambao wanahitaji likizo miaka mitano hawajapata, walimu wapya wanatakiwa kulipwa kwa wakati hawalipwi na matakataka mengine kibao!!
   
 7. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2010
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mie nilipoiona slogan yake ya mwaka huu nilisikitika kwa mambo makubwa mawili.
  1.kitendo cha ccm kushindwa kuona kiuwaziwazi kwamba slogan yao imeprove failure hivyo kupitwa na wakati.Yaani kamati yake ya kampeni imeshindwa kuja na slogan mpya.Hii imeonesha uvivu wa kufikiri na uwezo mdogo wa kutathmini alama za nyakati

  2.Dharau waliyoinesha kwetu watanzania,pamoja na upupu wote uliofanyika katika kipindi hiki cha miaka mitano bado wanaamini slogan hii itawapatia ushindi.Haya ni matusi tena ya nguoni.
   
 8. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yaani jamaa bado anathuibutu kuimba tena wimbo wa ARI, KASI na NGUVU?! Mbona yalishamshinda siku nyingi na sikuwahi kuusikia tena huo wimbo?
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  anajua mbayu wayu wapo tu!! ambao akili za kuambiwa na ccm, hawa-mix na zao!
   
 10. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ninavyoelewa slogan ya CCM mwaka huu ni "2010 Ushindi kwa CCM Lazima". Hiyo tu, inatosha kuwajua hawa watu sasa wameishiwa uongo, kilichobaki walazimishe mambo.
   
Loading...