Vuteni subira Katiba mpya- Msekwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vuteni subira Katiba mpya- Msekwa

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 4, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,012
  Trophy Points: 280
  Vuteni subira Katiba mpya- Msekwa


  Na Gladness Mboma

  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Bw. Pius Msekwa amewataka mwananchi mwenye mawazo Katiba kuwa na subira hadi
  pale Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume yake ndipo wayapeleke na si vinginevyo.

  Bw. Msekwa aliyasema hayo jana wakati alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka mjini Arusha baada ya kuombwa kutoa maoni yake kuhusu Katiba hiyo akiwa mmoja watu walioshiriki kuandika Katiba ya sasa.

  "Rais ameshazungumza yote kuhusiana na Katiba mimi siwezi kuzungumza lolote mawazo yangu na ya kwako pamoja na watu wengine yanayohusu Katiba tuyapeleke katika tume itakayoundwa na Rais na siyo kuhoji mtu mmoja mmoja,"alisema na kuongeza;

  "Sasa hivi tusubiri tume na siyo kusubiri maoni ya mtu mmoja mmoja, kwani haitawezekana kusikiliza maoni ya mamilioni ya watu wote kwa kuhoji mtu mmoja mmoja. Haitawezekana, ila tume itakwenda kila wilaya na kijiji kuchukua maoni ya wananchi," alisisitiza.

  Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Kikwete alitangaza mchakato wa katiba mpya katika hotuba yake ya kufunga mwaka 2010 na kukaribisha 2011, ambapo alieleza kuunda tume maalumu itakayoratibu maoni ya wananchi ili waamue jinsi wanavyotaka katiba hiyo iwe.

  Katika hotuba hiyo, Rais Kikwete aliwataka Watanzania kutokuwa na jazba katika madai mbalimbali ya katiba na kuweka wazi kuwa tume atakayounda haitabagua chama, rangi, dini na kwamba itaunganisha makundi yote ya jamii.

  Rais Kikwete alisema kuwa ameamua kuunda tume hiyo itakayoongozwa na mwanasheria aliyebobea, itakayokuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii kutoka pande mbili za muungano.

  Hata hivyo pamoja na Rais Kikwete kuvunja ukimya kuhusu mjadala huo wa Katiba ambao uliwakuna Watanzania, baadhi yao walimeshauri kuhusu utaratibu unaofaa kwa utekelezaji.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,012
  Trophy Points: 280
  Tatizo letu ni moja tu...............JK hana mamlaka ya kisheria ya kuunda tume ya kuandika katiba mpya.......kwa kufanya hivyo ni kuwa anataka kutuandikia katiba yake aitakayo mwenyewe halafu aibandike sifa ya kuwa imetokana na wadau................................

  Sisi tunataka Bunge lisimamie mchakato wote kwa kuutungia sheria itakayotuongoza njia ya kupita.............Hii tume ya JK haina nguvu ya kisheria lakini inavikwa majukumu ya kuongelea sheria .........................How absurd......................

  Labda Msekwa atueleze ni kwa nini JK anatudharau hivyo? Hajui ya kuwa tunajua utaratibu sahihi wa kupata katiba mpya ambayo itakidhi si mahitaji yake binafsi na Ridhiwani wake bali itakidhi mahitaji ya nchi nzima?
   
Loading...