Vuta picha vyama vyote vya upinzani vifutwe ibaki CCM pekee

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,598
3,644
Anaandika #GODBLESS_LEMA (MB) Arusha

Vuta Picha Vyama vyote vikafutwa katika kipindi hiki kikabaki CCM tu chama ulichonacho wewe.

Then hao uliokua unawaona hawafai akina Mbowe, Mdee, Heche, Nassary, Lema n.k wakaona ni UJINGA KUFA unatetea watu wasiojua kujisaidia wenyewe. Wakajiuliza Kwani tunakwama wapi? Acha na sisi tukaungane na CCM mtesi wao na sisi tuishi vizuri tu.

Then Wabunge wote katika Majimbo yote wakatokea CCM kila kitu kikaamuliwa ndani ya Chama.

Mbowe akasaidiwa kujenga Bilcanas mpya maisha yakaendelea kama tunavyoona watu wanasamehewa kubomolewa nyumba zao wakijiunga na CCM.

Mbowe, Mnyika, Lijualikali tayari wanatambulika na system ya Uongozi hapa nchini. Kama DC wa Dodoma anaejitambua kama karai amepata vipi hawa wenye makarai yao watakosa?

Then fikiria wewe Mtanzania wa kawaida utaishije na atakusaidia nani tena kuhoja kuhusu pesa yako?

Kama walipokuwepo watu wa kuhoji pesa yako bado walikua watu wanakula kwa kujificha japo kweli zinaliwa. Vipi wakikosekana?

Hivi mshawahi kufikiria madhara ya hizi Juhudi za Kudhoofisha Upinzani au huwa mnashangilia tu?

Mtaishi kama "Mbwa Koko" na hutatambulika tena kama mfuasi wa CCM watatambuana viongozi kwa viongozi. Who is going to deal with you?

Leo Viongozi wa CCM wanawanyenyekea kidogo wananchi ni kwa sababu wanajua kuna Uchaguzi awamu ijayo.... Na Pengine Jimbo likaenda Upinzani. Ikibaki CCM pekeake nani atakunyenyekea wewe? Nani atakuja kujua hata unaishije?

Mshafikiria?

Hamtamuona Polepole tena! Anakuja kueneza nini? Watakua ofisini tu wakilipana mishahara. Watawachagulia kila kitu na hakuna cha kuwafanya.

Mshafikiria?

Ni ngumu kuelewa kwa kuwa haijatokea na mnaangalia leo tu.

Huwa natamani hii hali itokee hata kwa muda wa mwezi mmoja tu.

Mtakopwa hadi mishahara mtasema wapi? Nani atawapigania kipindi hicho hata kina Lissu wanakula mema ya nchi tu.

Hicho ndo kipindi hata ajira mpya kuna zingine itabidi wapate kwanza watoto wa viongozi na wengine mtapata zitakazobakia.

Hicho ndo kipindi mtapigwa hadi fimbo makazini, nadhani Dalili za Makofi zimeanza na hakuna wa kuwatetea.... Ukienda kushtaki makahamani unawakuta wale wale. Unapeleka kesi na unafungwa wewe. Wa kupiga kelele itakua ni familia yako tu wengine wote wanaogopa.

Akina Mbowe kipindi hicho watakua wanakula kuku kwa mirija tu.

Mtawaita na hawataitika tena. Ipo sababu kubwa sana ya Kuilinda Demokrasia na vyama Vya Upinzani. Walioianzisha na Kuitetea kwa Damu hawakua wajinga they focused on their future.

Hatubembelezani hapa kuilinda demokrasia ya kweli maana kesho ni yetu sote.

Kila Unachotaka kukishabikia kipime kwanza madhara yake ya baadae.

Watu mnatamani vyama vya Upinzani vyote vife au vifutwe ila ipo siku mtavililia na hamtavipata.

Tafakari

Siku njema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani chadema ndo mungu tunayemuomba msaada hiyo in kufuru mbona pia kesho yetu in kaburini wote hapa duniani mi leo usijidanganye bro binafsi naitaji kiongozi muadilifu au mwenye khofu ya Allah sio DEMOKRASIA kwani ni mfumo hatari na wa kijinga kwa watu maskini hivyo km kula KUKU kwa mirija mlishakula sn na wanyonge wapo na chadema wapo ebu msituaminishe ujinga wenu huku wote ni walewale wanafiki wa kisiasa kubwa na zuri duniani tupo kwa muda mfupi na kila nafsi itaonja umauti hapo ndo mtakiona nyie wanaharakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kabla ya upinzani Nchi ilikuwaje?
Huko China kuna vyama vya upinzani?

Ni heri upinzani huu wa kutetea matumbo yao,kujimilikisha Ardhi,kutetea ufisadi ,kussuport ushoga na utegemezi wa misaada ...Ni bora ufe kabisa ili tupate vyama mbadala vyenye Sera zinazoeleweka.
 
Na sivuti picha Bali nitavuta pumzi ya mungu bure bila ubaguzi kwa muda huu mchache nitakaokuwa duniani acheni siasa za uongo mnawakejeli watu na watu wanaumia huku nyie mkineemeka kwan unaoneaha wazi unachuki kwan mbunge wa chadema halipwi mshahara au uliwai MPA nani zaid ya familia yako kuona mmebanwa kelele au ulitaka awekwe nani ndani vyovyote iwavyo dhuluma haidumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wamekufa,wameumia au madhira mangapi wanyonge yamewakuta ktk mfumo huu wa demokrasia huku wakiamini wabunge watawaletea maendeleo hatmaye wabunge wao wakaamia chama pendwa wala hawakujali wangap waliumia kwaajili yao bhas ifikie hatua tuseme hata uchaguzi unawagharimu watu kwa kuiga demokrasia ambayo asili yk ni unyonyaji tu hkn jipya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom