Sitachoka
JF-Expert Member
- Nov 17, 2011
- 3,030
- 1,303
Haya tena sasa PIGO KUBWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI NA UVCCM. Ni pigo jingine kubwa kwa chama cha mapinduzi na umoja wa vijana wa CCM (UVCCM)baada ya lile la kujiengua kwa makada wao maarufu James Milya , Ally Bananga,Diwani Maarufu Alphonce Mawazo . Sasa pigo hilo limekuwa la kuumiza zaidi baada ya kiongozi maarufu na kada maarufu wa chama hicho Easter Bulaya kutangaza nia ya kujiengua katika chama hicho baada ya kupata mizengwe mingi kutoka kwa kiongozi wa chama na mbunge wa Bunda steven Wassira. Kwa takriban mwaka mzima sasa wawili hao wamekua katika mgogoro mkubwa wa kimaslahi kiasi cha Mh. Easter Bulaya kutaka kujiengua ndani ya chama hicho.
Akiongea na waandishi wa habari leo jioni Easter alikiri kuwepo kwa mgogoro mkubwa kati yake na Steven Wassira baada ya kusema kuwa Wassira anaogopa kutoka madarakani kwa kuwa anajua Easter yuko tayari kulichukua jimbo hilo la Bunda. Pia alisema wananchi wamemchoka Wassira kutokana na ahadi hewa zisizo na utekelezaji, pia matumizi mabaya ya fedha za umma ambapo ametumia takriban Mil 27 kupaka rangi tu katika hospitali ya DDH ya wilayani bunda. Pia Easter aliendelea kusema kuwa fedha zilizotolewa kama msaada kutoka benki ya dunia kwa ujenzi wa shule ya Bunda hazijulikani zilipo.
Easter aliendelea kusema hayo ni machache tu ila kwa leo ameweka wazi nia yake ya kujiengua na chama hicho bila kushurutishwa na mtu yeyote