Vuta nikuvute Kati ya Steven Wassira na Ester Bulayaa: Mmoja atishia kujitoa CCM!

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Haya tena sasa PIGO KUBWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI NA UVCCM. Ni pigo jingine kubwa kwa chama cha mapinduzi na umoja wa vijana wa CCM (UVCCM)baada ya lile la kujiengua kwa makada wao maarufu James Milya , Ally Bananga,Diwani Maarufu Alphonce Mawazo . Sasa pigo hilo limekuwa la kuumiza zaidi baada ya kiongozi maarufu na kada maarufu wa chama hicho Easter Bulaya kutangaza nia ya kujiengua katika chama hicho baada ya kupata mizengwe mingi kutoka kwa kiongozi wa chama na mbunge wa Bunda steven Wassira. Kwa takriban mwaka mzima sasa wawili hao wamekua katika mgogoro mkubwa wa kimaslahi kiasi cha Mh. Easter Bulaya kutaka kujiengua ndani ya chama hicho.

Akiongea na waandishi wa habari leo jioni Easter alikiri kuwepo kwa mgogoro mkubwa kati yake na Steven Wassira baada ya kusema kuwa Wassira anaogopa kutoka madarakani kwa kuwa anajua Easter yuko tayari kulichukua jimbo hilo la Bunda. Pia alisema wananchi wamemchoka Wassira kutokana na ahadi hewa zisizo na utekelezaji, pia matumizi mabaya ya fedha za umma ambapo ametumia takriban Mil 27 kupaka rangi tu katika hospitali ya DDH ya wilayani bunda. Pia Easter aliendelea kusema kuwa fedha zilizotolewa kama msaada kutoka benki ya dunia kwa ujenzi wa shule ya Bunda hazijulikani zilipo.

Easter aliendelea kusema hayo ni machache tu ila kwa leo ameweka wazi nia yake ya kujiengua na chama hicho bila kushurutishwa na mtu yeyote
 
Kama ni kweli bulaya kanena haya adhihirishe kwa matendo,
Maneno matupu hayavunji mfupa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Weka chanzo cha habari mkuu!
Waache wagombane. Lakini huyu mzee hana kitu chochote,ester b akiamua jimbo ana lichukua! Aachane na hao magamba!
 
Majungu hayo ataenda wapi? Ccm ndicho kimemjenga na kumpatia nguvu alizo nazo kwani hao akina mawazo wako wapi si ndio kwisha yao cdm ina wenye hati miliki nyinyi wengine ni wachoma mkaa tu.
 
Kama Esther Bulaya anataka bright future yake politically aachane na huyo mzee pamoja na CCM yao aje CHADEMA kwenye tumaini jipya litakalomwangazia future yake kisiasa. Hakika hawakawii kumkolimba huyu binti akiendelea kujipima nao ubavu. NIMEMALIZA
 
Bulaya hatumtaki CDM abaki huko huko magambani maana huwa anazomea sana wapinzani bungeni.
 
Gambas Wanasiasa wote wanaangalia Maslahi kwanza. iwe CCM iwe upinzani.
 
Last edited by a moderator:
Mh. Rais Steven Wassira wa Tanzania (sorry .. nilikuwa najaribisha tu kama ina'sound' nicely). Maana nimesoma anatajwatajwa na CCM kama mgoombeaje amtarajiwa
 
CCM ni chama madhubuti hii sio asasi ya mageuzi kama vyama vingine milango ipo wazi na aondoke wapo kina Ester wengine watajitokeza; ajiulize ni wangapi walitishia na kujitoa na leo hii wapo wapi? Hao kina James Millya unawasikia?

Chama

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kama Esther Bulaya anataka bright future yake politically aachane na huyo mzee pamoja na CCM yao aje CHADEMA kwenye tumaini jipya litakalomwangazia future yake kisiasa. Hakika hawakawii kumkolimba huyu binti akiendelea kujipima nao ubavu. NIMEMALIZA

Namfahamu Esta Bulaya Tangu anasoma kile chuo cha uandishi wa habari cha DSJ hadi alipopata kazi Uhuru gazeti na kisha kujiingiza UVCCM. Hana sifa hizo kama mnavyodhani, mnamu-over rate!
 
Hivi naomba kuuliza na kutaka kujua! Bado Wassira anataka kuwa Mbunge?duu kazi kweli kweli kumbe ni ajira sasa sio utumishi wa wananchi kwa muda na kupumzika kuachia wenzako?anajimilikisha!!!
 
Hata ajira ina kikomo unless ni ya ujambazi. Majambazi hawastaafu.
Hivi naomba kuuliza na kutaka kujua! Bado Wassira anataka kuwa Mbunge?duu kazi kweli kweli kumbe ni ajira sasa sio utumishi wa wananchi kwa muda na kupumzika kuachia wenzako?anajimilikisha!!!
 
CCM ni chama madhubuti hii sio asasi ya mageuzi kama vyama vingine milango ipo wazi na aondoke wapo kina Ester wengine watajitokeza; ajiulize ni wangapi walitishia na kujitoa na leo hii wapo wapi? Hao kina James Millya unawasikia?

Chama

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
we huwasikii nadhani mkuu, nadhani watu wakiamia kwenu hawasikiki kama akina amani kaburu,hiza tambwe mmeshawazika!
 
Majungu hayo ataenda wapi? Ccm ndicho kimemjenga na kumpatia nguvu alizo nazo kwani hao akina mawazo wako wapi si ndio kwisha yao cdm ina wenye hati miliki nyinyi wengine ni wachoma mkaa tu.

Mbona unaitaja CHADEMA hapa? sijaona katika maelezo akitaja kuwa atahamia CHADEMA, mbona mnakuwa waoga kwa CHADEMA hivyo!? anaweza akajitoa ccm na akaenda chama kingine chochote, akaanzisha chama chake au akaamua kukaa nje ya ulingo wa siasa, any can be her option
 
Back
Top Bottom