Vurumai, Mabomu ya machozi vya rindima Singida kufuatia ajali iliondoa uhai wa mwanafunzi

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
6,276
12,335
Mwanafunzi moja wa shule ya msingi Kibaoni Manispaa ya Singida amefariki dunia jioni ya Leo baada ya kugongwa na Gari iliosemekana ni ya kusafirishia hela za benki.

Mwanafunzi huyo aligongwa akiwa sehemu salama kabisa inayoruhusu waenda kwa miguu kuvuka barabara yani zebra, lakini kwa kutojali kwake Dereva wa Gari Hilo alimpitia na kumvuruta kwa umbali wa mita 50 hali iliyosababisha kutokutambulika kwa maiti hiyo kiurahisi kwani kichwa hakionekani

Baada ya hayo wananchi walifuata gari Hilo kwa hasira na kuanza kulipiga mawe,hali iliyosababisha Polisi kuingilia Kati na kutandika Mabomu ya machozi na maji ya washa washa

Kuna kiongozi moja ambae chanzo Cha habari hakikufanikiwa kumtambua either ni RC or DC lakini alishindwa kutuliza hali ya Mambo

RIP mwanafunzi
 
wale jamaa wanapaswa kurudi tena darasani, na mifumo ya ulinzi au usafirishaji hela unadirike sasa kuliko kutumia mbinu za kizamani.

Wanaendesha magari wakitanua kushoto na kulia bila kuzingatia maeneo wanayofanya hivyo, unakuta eneo lina korongo kushoto na kulia wao wanatanua huku wakijua wewe huna pwakweda ssasa sijui uende kolongoni au mtaloni?, Zebra crossing wao wananyoosha tu.

Hata kama unasafirisha hela au mgonjwa hupaswi kuacha madhara mengine nyuma... Dereva akamatwe apewe kesi ya kuua kwa kukusudia na hukumu iwe kunyongwa mpaka afe tena kesi iende haraka ndani ya miezi miwili na kunyongwa anyongwe haraka...ni PUMBAVU huyo amefanya kabisa, wengine watajifunza.

Hii misafara na usafirishaji wa hela vikome kwenye hizi highways vichochoro, barabara zenyewe nyembamba halafu bado tunalazimisha ujinga huu.

Hela zisafirishwe na Cargo plane mpaka mkoa husika au hellicopter za jeshi tena wawe wanalipia kuliko kuleta usumbufu, ajali na vifo visivyo vya lazima.
 
Apumzike kwa amani. Lakini pia tuwafundishe na watoto namna sahihi ya kuvuka kwenye alama.

Pia watambue sehemu hizo za uvukaji bado zinazingatia kanuni za kutazama pande zote na kufanya maamuzi.

Uvukaji pia uwe wa haraka katika maeneo hayo,sio kutembea kama mgonjwa.

Eneo la wavuka kwa miguu bado halikupiki haki zote mtembeaji,maana kuna dharura za vyombo vya moto ambavyo vinaweza kukuondolea haki hiyo.

Pole kwa familia, ndugu,jamaa na marafiki kwa kumpoteza kijana.
 
Hata hawa wa Ambulance na Zimamoto waambiwe pia...unaweza kutaka kuokoa kifo cha mtu mmoja halafu ukaacha vifo kumi nyuma....unaweza kuwahi kuzima moto nyumba moja huku haina watu halafu nyuma ukaacha vifo 100...
 
wale jamaa wanapaswa kurudi tena darasani, na mifumo ya ulinzi au usafirishaji hela unadirike sasa kuliko kutumia mbinu za kizamani...
Kunq zile zebra crossing zinawekwa jirani kabisa na taa za barabarani.

Unakuta taa zimeruhusu lakin kuna watu wanaamua kupita tu kisa wapo kwenye zebra. Hii sio sawa.

Sisi wazee wa TZ 11 tujitahidi sana kuchukua tahadhari,maana likikukuta hakuna fidia itoshayo mwili ama uhai wako.
 
Back
Top Bottom