Vurumai kwenye Uchaguzi wa Mitaa, Ukimya wa JPM, Je huku si kupotoka kwa Serikali kwenye dhamana ya Umma?

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Najaribu kuuliza hilo swali. Natafakari dhamana ya serikali na viongozi wetu kwenye hii vurumai na najaribu kuiangalia wajibu wa kuwajibika(Responsibility) naona giza.

Yaani kwamba zoezi la maandalizi ya uchaguzi kwa hatua za awali kabisa serikali kufanya figisu ya kutoa tarehe kwamba ilikuwa ni bure na hakukuwa na hujuma?

Kwamba figisu za kutunga kanuni kukosa uwazi na kuwekwa mitego mingi kiasi cha wadau kulalamika katika hatua za aswali kwamba hakukuwa na nia ovu?

Kwamba Mh Rais kuzungumza na watendaji wa kata na mitaa nchi nzima hakukuwa na azma fulani?

Kwamba zoezi la kuchukuwa fomu, kujaza na kurejesha na mizengwe iliyotokea kwa wapinzani iwe ni bure na hakukuwa na azma ya vurumai?

Kwamba Kutumika kwa watendaji wa kata na mitaa kuvuruga hilo zoezi bila kuchukuliwa hatua yoyote ni bure na serikali kuu haihusiki?

KUWAJIBIKA KWA SERIKALI.

Yani kwamba serikali kwenye hili haiwajibiki kwa umma? haikereki na sintofahamu hii ya vurumai na wala inahisi haiwajibiki kwa yaliyotokea? Nani anawajibika bas?

Eti wanatumika viongozi wa Dini kubeba msalaba wa dhambi hii kusafisha na kumbe wanatumika kuchonganisha watanzania?

Nani awawajibishe watendaji wa kata, halmashauri, wilaya, mikoa, Waziri wa TAMISEMI ? Nani amuwajibishe mwenzake ?

Kwamba juu ya yote , makelele, kujimwambafai kwa serikali juu ya Wanyonge kote kule haioni namna WANYONGE NA MASIKINI HUKO VIJIJINI WALIVYONYANGANYWA HAKi ZAO ZA KUCHAGUA?

UKIMYA WA RAIS MAGUFULI.

Yaani Rais yuko kimya hadi sasa ? Anajaribiwa nani kwenye waJIBU HUU WA SERIKALI KWA UMMA?

Rais anasubiri nini ili awawajibishe wavurugaji au huu ukimya utafsiriwe vipi?

Hivi series yote hiyo ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka 2019 kutoka hatua za awali hadi sasa , serikali ya JPM itakwepa vipi kuwajibika kwa umma kwa matokeo ya uchaguzi huu?

Endeleeni kunyamaza.

Kishada.
 
Ukiandika kitu lazima ujue mwelekeo wa sasa wa nchi, na si kujifanya unaishi nje.
 
Tusimuingize Rais kwenye mambo asiyohusika
Hana jinsi ya kukwepa haya, bila baraka zake katika uchafu huu angewawajibisha wahusika. Sifa zake za tumbua tumbua TAMISEMI yote ingepigwa chini na akajizidishia umaarufu na kimya chake(kana kwamba nothing went wrong kwenye ufutwaji wa wagombea) kinaashiria blessings zake kwa yote yaliyotokea.
 
Sio kila kitu ni mpaka rais Magufuli, maadam rais ana wasaidizi, na hoja zote ziko ndani ya uwezo wao, hakuna haja ya rais Magufuli kuingilia kila kitu, unless things got off hand.

Saa hizi watu tunasubiria tuu kukamilishwa tuu kwa taratibu, ndipo tusherehekee ushindi wa kishindo.

P
 
Sio kila kitu ni mpaka rais Magufuli.
P
Raisi ni Nani? Kwa mujibu wa katiba ni Head of state(Mkuu wa Nchi),
Kila litendwalo iwe kwa kujua/kutokujua/Kushiriki moja kwa moja au kutendwa na Wasaidizi wake,
Eg:mawaziri, wakuu wa mikoa,wilaya na N.k,
Ni moja kwa moja lazima kiwe na Baraka zake kwa sababu Katiba pia inawatambua hao kama Wasaidizi wake,na Kauli zao ni kauli ya aliewateua.
Pasipo yeye hakuna wao.

Cc Zero iq
 
Sio kila kitu ni mpaka rais Magufuli, maadam rais ana wasaidizi, na hoja zote ziko ndani ya uwezo wao, hakuna haja ya rais Magufuli kuingilia kila kitu, unless things got off hand.

Saa hizi watu tunasubiria tuu kukamilishwa tuu kwa taratibu, ndipo tusherehekee ushindi wa kishindo.

P
TAMISEMI iko chini ya nani?
 
Mkuu siamini kwamba unaweza kuingia kwenye kapu la watu wa aina hii. Yaani jambo ambalo ni la Kitaifa na linaviashiria vyote vya kutia doa Serikali nzima useme Rais ana wasaidizi?

Ama kweli peremende haijawahi kumuacha mtu salama.
 
Hana jinsi ya kukwepa haya, bila baraka zake katika uchafu huu angewawajibisha wahusika. Sifa zake za tumbua tumbua TAMISEMI yote ingepigwa chini na akajizidishia umaarufu na kimya chake(kana kwamba nothing went wrong kwenye ufutwaji wa wagombea) kinaashiria blessings zake kwa yote yaliyotokea.
Wengine wanajificha kwenye kivuli cha Wasaidizi. Aibu imevuka hata ubinadamu na imeizingra mishipa ya ufahamu.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Raisi ni Nani? Kwa mujibu wa katiba ni Head of state(Mkuu wa Nchi),
Kila litendwalo iwe kwa kujua/kutokujua/Kushiriki moja kwa moja au kutendwa na Wasaidizi wake,
Eg:mawaziri, wakuu wa mikoa,wilaya na N.k,
Ni moja kwa moja lazima kiwe na Baraka zake kwa sababu Katiba pia inawatambua hao kama Wasaidizi wake,na Kauli zao ni kauli ya aliewateua.
Pasipo yeye hakuna wao.

Cc Zero iq
Kwenye huu uchafu watakwambia ana wasaidizi lakini kwenye kusifia mema watakwambia pongezi kwa Rais.
 
Najaribu kuuliza hilo swali. Natafakari dhamana ya serikali na viongozi wetu kwenye hii vurumai na najaribu kuiangalia wajibu wa kuwajibika(Responsibility) naona giza.

Yaani kwamba zoezi la maandalizi ya uchaguzi kwa hatua za awali kabisa serikali kufanya figisu ya kutoa tarehe kwamba ilikuwa ni bure na hakukuwa na hujuma?

Kwamba figisu za kutunga kanuni kukosa uwazi na kuwekwa mitego mingi kiasi cha wadau kulalamika katika hatua za aswali kwamba hakukuwa na nia ovu?

Kwamba Mh Rais kuzungumza na watendaji wa kata na mitaa nchi nzima hakukuwa na azma fulani?

Kwamba zoezi la kuchukuwa fomu, kujaza na kurejesha na mizengwe iliyotokea kwa wapinzani iwe ni bure na hakukuwa na azma ya vurumai?

Kwamba Kutumika kwa watendaji wa kata na mitaa kuvuruga hilo zoezi bila kuchukuliwa hatua yoyote ni bure na serikali kuu haihusiki?

KUWAJIBIKA KWA SERIKALI.

Yani kwamba serikali kwenye hili haiwajibiki kwa umma? haikereki na sintofahamu hii ya vurumai na wala inahisi haiwajibiki kwa yaliyotokea? Nani anawajibika bas?

Eti wanatumika viongozi wa Dini kubeba msalaba wa dhambi hii kusafisha na kumbe wanatumika kuchonganisha watanzania?

Nani awawajibishe watendaji wa kata, halmashauri, wilaya, mikoa, Waziri wa TAMISEMI ? Nani amuwajibishe mwenzake ?

Kwamba juu ya yote , makelele, kujimwambafai kwa serikali juu ya Wanyonge kote kule haioni namna WANYONGE NA MASIKINI HUKO VIJIJINI WALIVYONYANGANYWA HAKi ZAO ZA KUCHAGUA?

UKIMYA WA RAIS MAGUFULI.

Yaani Rais yuko kimya hadi sasa ? Anajaribiwa nani kwenye waJIBU HUU WA SERIKALI KWA UMMA?

Rais anasubiri nini ili awawajibishe wavurugaji au huu ukimya utafsiriwe vipi?

Hivi series yote hiyo ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka 2019 kutoka hatua za awali hadi sasa , serikali ya JPM itakwepa vipi kuwajibika kwa umma kwa matokeo ya uchaguzi huu?

Endeleeni kunyamaza.

Kishada.
JPM inaonekana wazi kaagiza au kubariki ujinga unaoendelea.

Halafu unategemea afanye nini? Akemee?
 
Back
Top Bottom