Vurugu zazua balaa mpakani Tanzania na Zambia

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112








Mahanga%285%29.jpg

Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Milton Mahanga



Mapango makali yaliyozuka jana nchini Zambia, katika eneo lisilo la mwenyewe (No man's Land), jirani na mpaka wa Tanzania katika mji mdogo wa Tunduma, yalisababisha shughuli za mpaka huo kusimama kwa muda.
Kadhalika, hali hiyo ilisababisha kuwepo kwa msongamano mkubwa wa magari ya mizigo na abiria mpakani hapo, hali iliyoukumba pia msafara wa Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Milton Mahanga aliyekuwa na ziara ya kikazi katika eneo hilo.
Akizungumza na Nipashe, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, alisema vurugu hizo zilizotokea upande wa Zambia, pia ziliathiri shughuli za kawaida upande wa Tanzania.
Alisema chanzo cha vurugu hizo ni watendaji wa Halmashauri wa Nakonde nchini Zambia kufanya msako wa wazururaji bila kushirikiana na Polisi wa Zambia wala wa Tanzania na kuingia katika eneo lisilo na mwenyewe mahali walipo wamachinga wengi.
Alisema wamachinga walipobaini kuwa hakuna Polisi kwenye msako huo, walianza kuwashambulia kwa mawe viongozi hao na kusababisha vurugu za aina yake.
Alisema watendaji wa Halmashauri ya Nakonde walilazimika kuomba msaada wa Polisi wa Zambia, ambao walifika eneo hilo na kuanza kulipua mabomu ya machozi kwa lengo la kuwaokoa watendaji hao ambao kwa wakati huo walikuwa wakiendelea kushambuliwa na wamachinga.
Kamanda Nyombi alisema Polisi walipopata taarifa hizo walikwenda mpakani hapo na kujiweka tayari tayari kwa lolote, ikiwa kama vurugu hizo zingeingia hadi upande wa Tanzania.
Askari kutoka ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mbozi aliyekuwa akisindikiza msafara wa naibu Waziri, alilazimika kufanya kazi ya ziada kuondoa magari yaliyokuwa yameegeshwa pembezoni mwa barabara ili kuruhusu msafara wa Dk. Mahanga kupita.
Hata hivyo, baada ya muda vurugu hizo zilidhibitiwa na askari na shughuli za mpakani kuendelea kama kawaida.



CHANZO: NIPASHE
 
napenda sana hilo jina la no mans land utakuta watu wamekaa wanafanya wanachotka hapo wazi wazi magendo, bangi kila aina ya uhuni na askari wanaangalia tu du sikuelewa na bado sijaelewa
 
Back
Top Bottom