Vurugu zavunja kikao cha Halmashauri ya jiji la Tanga

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Tanga chavunjika baada ya madiwani wa CUF kutomtambua Meya Suleiman Mustapha kwa madai hakushinda kihalali.

==================

tanga+jiji.jpg

Tanga. Halmashauri ya Jiji la Tanga ipo hatarini kuvunjwa kufuatia madiwani wake kushindwa kuelewana katika kikao kilichositishwa leo na Mkurugenzi mtendaji.

Kikao hicho cha baraza la madiwani wa Halmashairi ya Jiji la Tanga kwa mujibu wa barua za mwaliko walizopewa madiwani hao kilikuwa ni cha mwendelezo wa mkutano wa desemba 19 mwaka jana ambacho pia kilivunjika baada ya kutokea vurugu.

Chanzo cha kuvunjika kikao cha leo ni baada ya diwani wa kata ya Tangasisi (CUF) ambaye pia ni Naibu Meya, Mohamed Haniu kuchukua kipaza sauti na kutangaza kwamba kama wanataka kikao hicho kiendelee ni lazima ufanyike uchaguzi wa Meya.

“Kwenye wito wa barua za kikao hiki hakuna ajenda ya uchaguzi kwa hivyo tukubaliane kwanza kwamba tunaanza na uchaguzi wa Meya ndipo tuendelee kwa sababu hatuna meya hadi sasa”alisema Haniu.

Tangazo hilo lilisababisha madiwani wa kutoka chama cha wananchi (CUF) kushangilia jambo lililomlazimu Meya wa Jiji, Mohamed Mustapha (Selebosi) kutamka kwamba kikao anakiahirisha.

Tamko la Selebosi lilisababisha madiwani wa CUF kushangilia kwa mara ya pili huku wakiimba nyimbo za kukisifu chama hicho.

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho,Meya wa Jiji hilo, Mohamed Selebosi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdullah Lutavi, Mbunge wa Jimbo la Tanga, Mussa Mbarouk na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Dk Wedson Sichalwe waliingia katika ofisi ya Mkurugenzi kufanya kikao chao cha ndani.

Akizungumza na waandishi wa habari,Kaimu Mkurugenzi , Sichalwe alisema ajenda ambazo zilikuwa zijadiliwe ni kuunda kamati za kudumu za halmashauri, kupanga ratiba za vikao vya halmashauri, kupokea taarifa ya utendaji wa halmashauri katika kipindi ambacho madiwani hawakuwepo na kupokea taarifa ya Serikali.

“Kama mlivyoshuhudia kikao kimevunjika,inapotokea vurugu kama vile hakuna sababu ya kuendelea na kikao, sheria inamruhusu Meya kukivunja” alisema Dk Sichalwe na kusisitiza kuwa taarifa zaidi atatoa baadaye.

Diwani wa Kata ya Duga (CUF), Halid Rashid alisema watakuwa tayari kuendelea na kikao iwapo madiwani wa CCM watakubali uchaguzi wa nafasi ya meya ufanyike upya kwa sababu hawamtambui Mohamed Mustafa kama Meya.

“Ni bora Halmashauri ya jiji ivunjwe kama Serikali inalazimisha tumtambue Selebosi kuwa ni Meya, sisi hatutakubali akae mbele kuongoza kikao aje huku ndiyo kikao kiendelee” alisema Halid.

Mohamed Haniu (CUF) alisema anaamini Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela anaweza kumaliza mgogoro wa nafasi ya Meya wa Tanga kwa kutumia busara ya kuamuru uchaguzi wa meya ufanyike upya.

Diwani wa kata ya Chumbageni (CCM) Saida Gaddafi aliwataka madiwani kutoka chama cha CUF kukubali matokeo yaliyomtangaza Selebosi kuwa Meya kwa sababu hata wao walimkubali Mohamed Haniu kuwa Naibu Meya.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga aliwahimiza madiwani wa Jiji kukubaliana ili vikao vya kupitisha miradi ya maendeleo ya wananchi viweze kuendelea.

Dalili za kutokea vurugu katika kikao hicho zilijitokeza mapema kufuatia jeshi la polisi kumshikilia Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Tanga na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Meya wa jiji la Tanga, Rashid Jumbe asubuhi kabla ya kuanza kikao hicho.

Taarifa za kushikiliwa na jeshi la Polisi diwani huyo zilienea na hata kikao kilipoanza hakuwepo ukumbini ambapo madiwani wenzake walisema alikamatwa kwa madai ya kuratibu shughuli za matangazo kuhusiana na kikao hicho kwa kutumia gari lililopita mitaani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Leonard Paul alithibitisha kukamatwa kwa diwani Rashid Jumbe na kwamba alikuwa akituhumiwa kutangaza mitaani kwa kutumia gari kuhusu kikao hicho.

Chanzo: Mwananchi
 
Safi, democracy must take its course.....................................
 
Kama sikosei tulisikia uchaguzi wa Meya utarudiwa ...hilo limekaaje huko?
 
Baraza limevunjika au kikao kimevunjika, kwa maeleze yako inabidi warudi kwenye uchaguzi wa madiwani.

Mleta mada toa ufafanuzi wa kutosha.
 
Chama kisichotaka kushindwa katika ubora wake,hawakawii kumwita Jecha hapo Tanga afute uchaguzi wa mbunge na madiwani,akamtangaza meya wa kichina kashinda kwa 92.876.
 
Ulifikiri mimi ni kanjanja mwenzako? Siyo najita ndio kazi yangu usichokielewa hapo ni nini au kwasababu tayari kimebuma?

Kama kweli wewe ni mwanahabari na haujaona kosa kwenye habari yako basi wewe ni Kubenea type mwenye elimu ya hapa na pale.
 
Halafu wewe mtoa mada kuwa na nidhamu, unaulizwa baraza limevunjika au ni kikao bado unajifanya mjuaji tena eti kazi yangu ndio hiyo, kuvunjika kwa baraza maana yake watu wanaenda kwenye uchaguzi na kama kikao kimevunjika bado baraza la madiwani ni hai, sasa watu wanauliza wewe unajifanya kila anayeuliza anatetea huo ujinga wa meya wa Tanga, kwa kifupi Sele Boss hajashinda umeya kihalali na hili ccm wanatakiwa wajue kwa hali ilivyokuwepo hakukuwa na uwezekano wa diwani yoyote wa chama cha upinzan angejaribu kumpigia mtuhumiwa yoyote wa ccm. Madiwani wa CUF wanatakiwa wagome mpaka mwisho kuonyesha kupinga ubakaji wa demokrasia.
 
Umeanza kutoa puvu naona serekali ya Tv na Magazeti imekuaribu sana mpaka mkitia sadaka kanisani mnaita wandishi wa habari
Unasema? hata kwenye sadaka nako?
Anyway tuache hayo, hivi Tanga nako wanasubiri jamaa aseme neno moja tuu na Uchaguzi wa kweli wa meya ndio ufanyike?
 
Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Tanga chavunjika baada ya madiwani wa CUF kutomtambua Meya Suleiman Mustapha kwa madai hakushinda kihalali.

Chanzo: Mwanahabari Huru Jijini Tanga

Bahati mbaya bila madiwani wa Ukawa kuwepo akidi haitatosha hata siku moja.
 
Back
Top Bottom