Vurugu zatokea Mahakamani Arusha kwenye kesi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA

Mahakama haiwezi kamwe kuhukumu kwa kufuata shinikizo la wingi wa watu waliopo nje!!!!
 
Kwani Rais haoni kuwa watu wake maskini wanateseka kwa yeye kuwepo madarakani madaraka amepata sasa kwanini asiwaachie watu wasio na makosa hao?
Kwa hiyo raisi ndio aliwatuma kufanya makosa?
Au huyu raisi ndo wa Kwanza kuingia madarakani Kisha watu wakapata kesi?
Fateni Sheria uone Kama utakutana na hayo Mambo.

Ukimsaka Simba ndani ya kichaka lazima uwe tayari kupambana nae.
Hata hao huenda walijiandaa yanayotokea.
Mshawishi mkubwa yupo ubelgiji anakunywa mvinyo na nyama choma na watoto wake wako shule ila hao wapi sero.
 
Kwa hiyo raisi ndio aliwatuma kufanya makosa?
Au huyu raisi ndo wa Kwanza kuingia madarakani Kisha watu wakapata kesi?
Fateni Sheria uone Kama utakutana na hayo Mambo.

Ukimsaka Simba ndani ya kichaka lazima uwe tayari kupambana nae.
Hata hao huenda walijiandaa yanayotokea.
Mshawishi mkubwa yupo ubelgiji anakunywa mvinyo na nyama choma na watoto wake wako shule ila hao wapi sero.
Nani kakwambia wana makosa?
Style mpya ya kutesa wapinzani kisheria imepatikana!
*Unawabbikizia kesi,hata kama zina dhamana unazuia dhamana zao na wanasota rumande!
*Unapiga danadana kesi kwa kusema uchunguzi haujakamilika huku kiuhalisia hakuna uchunguzi wowote unaofanyika maana ni kesi ya kubambikizia!
*Wanasota rumande mpaka pale serikali itakapoona imetosheka na adhabu.
*DPP anakuja kusema hana nia ya kuendelea na kesi na kesi inafungwa rasmi!
Hapo mtu umesota miezi kadhaa jela halafu anatokea mpuuzi mmoja amasa hana nia ya kuendelea na kesi na wakati huo huo kesi ilikuwa ya kubambikiziwa!

Wallah ikitokea kwangu halafu nikatoka nitazaa na DPP!
 
Sehemu nilipopigia mimi kura yaani hakukuwa na shida yoyote na wapinzani walishindwa kihalali kabisa!

Sina tatizo lolote la wapinzani kushindwa kihalali, tatizo langu lipo kwenye ushindi usio wa halali.
 
Sheria ipi inaruhusu wahanga wa siasa za upinzani kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi?
Swala la kusema kuwa wapinzani ndo wahanga zaidi,ni swala la hisia zako tu mkuu.Sasa kama ni kweli wamehusika,unataka wasihukumiwe kwakua ni wapinzani?
 
Halafu kuna wapuuzi walikuwa wanasema cdm waende mahakamani wakafungue mashtaka kama wameibiwa kura, kisha mahakama ndio hizo zinaagizwa na wahuni wachache wa serekali jinsi ya kuendesha kesi.
Naona kama hata kule kujizuia wasionekane kuwa 'extreme' sasa kumeondoka.
Hivi kuna nini hasa kinachosababisha 'desperation' yote hii?

Mbona ni kama watu wamekwishakubali na wamejisalimisha tayari, kwa nini wakati huu ndio wazidishe huu ukandamizi? Wananuia kufanikiwa kwa kiasi gani zaidi ya walivyofanikiwa tayari?

Watu wamekwishaogopa vya kutosha na kujisalimisha, ya nini kuendelea kuwatia hofu?
 
Tanzania hamna mahakama huru tena. Ndiyo maana hakuna hata mtu mmoja wa upinzani amefungua kesi kuoinga matokeonya uchaguzi mwaka huu.
Mkishinda kesi mnasifia kuwa mahakama zipo huru na imetenda haki lakini ukiona mmebanwa mnasema Tanzania hakuna mahama iliyo huru ni ajabu kabisa.
 
Mambo kama haya ya kijinga tanayofanywa na serekali ya chama changu, ndiyo yanayo wapa sababu serekali za kutukebehi na hii ya Arusha ITAMSAIDIA SANA LEMA KUWEZA KUPEWA UKIMBIZI WA KISIASA.
 
Mkishinda kesi mnasifia kuwa mahakama zipo huru na imetenda haki lakini ukiona mmebanwa mnasema Tanzania hakuna mahama iliyo huru ni ajabu kabisa.

Kwa taarifa yako watu huwa hawasifii kwamba mahakama ziko huru, bali hushangaa mahakama zinapothubutu kutenda haki dhidi ya maagizo ya watawala wenye viburi vya madaraka.
 
Katika hali ya kushangaza Dunia, mahakama ya hakimu mkazi Arusha,imesema haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa Washtakiwa 20 ambao ni wanachama na viongozi wa CHADEMA wanaokabiliwa na Kesi no 72,75 na 76 zote za Uhujumu Uchumi zinazokabili wanachama 20 wa Arusha Mjini na Arumeru Magharibi

Hakimu Mfawidhi Bi.Mahumbugwa alikuwa anawasiliana na wakili wa serikali kabla ya kusoma hukumu hii ambayo imefanya ndugu wa washtakiwa kubaki midomo wazi, kabla ya hukumu ya leo Hakimu huyu huyu na mahakama hii ilitoa uamuzi Novemba 9 kuwa ina mamlaka ya kutoa dhamana kwa kuwa shtaka lenyewe halina zaidi ya 10mil.Ni mara ya kwanza kwa hakimu wa mahakama kutoa hukumu mbili tofauti kwenye shauri moja

Kisheria baada ya hukumu ya kwanza upande wa Jamhuri ulipaswa kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama lakini badala yake hakimu amewekewa shinikizo na Serikali kufuta hukumu ya awali

Baada ya ndugu kusikia hivo walizingira mahakama wakitaka haki itendeke kwa ndugu zao ambao ndio watafuta mkate wa kila siku wa familia,baadhi ya washtakiwa wana watoto wachanga!

Mawakili wa upande wa Wafuasi wameeleza kuwa wataenda mahakama kuu kuomba dhamana kwa ajili ya wateja wao! Jopo hili linaongozwa na Wakili maarufu Jijini Arusha Sheck Mfinanga,pamoja na wakili Jebra Kambole na Winnie

Ndugu wa washtakiwa walionekana mahakamani hapa wakiwa na jaziba kali kiasi cha kutishia usalama wa mahakama,na wamesema siku ya shauri watakuja kwa wingi kuonyesha mshikamano,aidha wametaka Mahakama itende haki kwa kuwa ndugu zao wamebambikiziwa kesi za kisiasa

My take,
Mahakama inapaswa kutoa haki mapema maana haki iliyocheleweshwa ni haki iliyonyimwa.
Huyu hakimu aache ubabaishaji atende haki maana kuna siku uvumilivu utawashinda watu

Duh! Martha Martha Martha, kweli unakubali mashinikizo ya kisiasa?
 
Tatizo lina hao ndugu Yani wanaendelea kudhani nchi ina mahakama? Yani moja ya upumbavu ni kufikiri nchi bado ina vyombo vya kutetea wananchi. Wao walitakiwa kuwatoa ndugu zao Basi na sio kusubiri upuuzi wa hakimu
 
Back
Top Bottom