Vurugu zatokea CCM Tabora. Ni baada ya Jina la Lucas Seleli kurudishwa kugombea NEC kinyemela, Mpogolo ahusishwa

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,395
Fujo kubwa sana zimetokea leo katika kikao cha wajumbe wa Kamati ya siasa mkoa wa Tabora baada ya jina la mgombea wa 4 kurejeshwa leo wakati vikao vya mchujo vilimalizika wiki jana Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu Mpogolo anasemekana ndio mratibu wa hili jambo huku akitumia jina la Rais Magufuli kuwa ndio kamtuma arejeshe jina la Lucas Seleli kuwa moja wa mgombea wa nafasi ya NEC

Awali katika vikao vilivyomalizika wiki jana, wagombea wote walipitiwa na vikao vya juu husika, na katika kupitisha majina Ndg. Seleli alikatwa katika vikao hivyo. Ila cha kushangaza leo Naibu Katibu Mkuu kavunja kanuni, sheria na taratibu za chama kwa kuingiza jina la Seleli kinyemela..

Tayari wajumbe wote wametoa msimamo kuwa hawataingia katika chumba cha kupiga kura, kwani huu ni uhuni, na kumtaka Naibu Katibu Mkuu kuacha kumchafua Rais kwa kutumia jina lake..
 
Huu ni unafiki wa kupitiliza wa mashetani... eti aache kumchafua Rais hivi huyo mpogolo ana ubavu gani wa kujiamulia hayo yeye mwenyewe?

Huyo mwenyekiti anaenunua wapinzani ndo eti asichafuliwe? Kichefuchefu!!@
 
Hivi bado kuna haja kweli ya kuwa na wajumbe wa nec kwenye hii ccm mpya, mimi nadhani ni muda muafaka sasa kwa wajumbe wote kujiuzuru ili kuunga mkono jitahidi za mwenyekiti za kuleta maendeleo ya viwanda na kuwakomboa wanyonge. Anyways, acha wafu wazikane wenyewe, mhudumu ongeza glass...
 
Wajumbe wengi wanaopiga hizo kura njaa sana matishet yalishaanza kubadilika rangi wana haki ya kumpinga seleli wa anko magu
 
mtifuano ndani ya chama ni afya hatuhami wala hatukimbii chama, mwisho wa siku tutakaa chini tutakubaliana na kufikia muafaka licha ya kuwa na makovu mwili mzima,na baada ya hapo nguvu zetu tutazihamishia kwa wale wanaojiita wapinzani wetu maana tutakua ni nguvu moja tena.
 
Back
Top Bottom