Vurugu zatawala Pretoria, vijana wa ANC wagomea uteuzi wa Meya mpya

Sele Mkonje

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
643
845
jiji la pretoria limeingia tena katika machafuko kwa siku ya pili mfululizo baada ya vijana wa ANC kuingia mtaani na kufanya uharibifu wa hali ya juu wakishinikiza kuongeze muda wa muhula mwingine kwa meya wa jiji hilo na kuponga utenguzi wa mgombea mwingine kwa ajili ya nafasi hiyo.

Vijana hao WAMECHOMA MOTO maduka ya wageni na kuvunja vioo vya magari yaliyokuwa yakikatiza eneo hilo.

Hata hivyo meya wa sasa wa Pretoria amelaani tukio hilo na kusema kuwa yeye amejitenga na vurugu hizo na ameridhika na chama chake kumchagua mgombea mwingine..

Baadhi ya shule zimewatumia wazazi ujumbe wa simu kutowaruhusu watoto wao kuhudhuria masomo mpaka pale hali itapokuw shwari.

My take: Wale watanzania na wanaafrika mashariki mliopo maeneo ya karibu na pretoria muwe makini katika shughuli zenu za kila siku mpaka pale vurugu zitapotulia.
 
Wapumbavu sana hawa, bora hata mzungu angeendelea kuwakalia, kazi yao kuchoma maduka ya wageni kila wakikurupuka.
 
Wapumbavu sana hawa, bora hata mzungu angeendelea kuwakalia, kazi yao kuchoma maduka ya wageni kila wakikurupuka.
Sijui kama wanaeleweshwa kuwa walisaidiwa na waafrika hao wageni kukabiliana na kaburu mweupe akubali haki sawa kwa wote, sasa wa-South Afrika eusi wamekuwa makaburu-weusi
 
Sijui kama wanaeleweshwa kuwa walisaidiwa na waafrika hao wageni kukabiliana na kaburu mweupe akubali haki sawa kwa wote, sasa wa-South Afrika eusi wamekuwa makaburu-weusi
yani hasira zao huwa wanamalizia kwetu waafrika wenzao.
 
JACOBO ZUMA is a disgrace to south africans, he must go.
 
Hawa wapuuzi weusi wa Africa kusini ni zaidi ya makaburu, ngoja watawaliwe jumla part two.
 
Back
Top Bottom