Vurugu Zanzibar, makanisa yachomwa moto!

picha za kanisa la kariakoo znz lilivyochomwa. Hawa jamaa nia yao siyo siasa tu, kuna chuki na udini nyuma yake.
Hawawezi kukaa bila migogoro hawa, hata wakiacha muungano watazua jingine tu

Lengo ni Taifa la kiislam Zanzibar na inshaallah tutafika.
 
Kama slovakia,serbia,kossovo n.k wameweza wazenji mtashindwaje?

Songa mbele ndugu maendeleo ni matokeo ya presha popote pale duniani
 
wanasiasa na viongozi watumie hekima na busara kuepusha mambo makubwa kutokea.
 
Kwa hiyo hicho mnachokidai kimenyimwa na Kanisa mpk mlichome moto?

Hii ndio busara yenu mliorithi kwa waarabu. Utaitakaje haki usiyoweza kuwapa wengine? Hili linadhihirisha jinsi mlivyo wa hatari kama mkiachwa muendelee na huu ujinga wenu
 
something need to be done in Znz....haiwezi kuwa kimya katika suala hili...
 
Hayo yote sawa lakini kuchoma kanisa hapana, hiyo haikubaliki hata kidogo!kanisa linahusiana vipi na siasa au muungano?hivi wakristu wakijibu kwa kuchoma misikiti itakuwaje??siasa zifanywe kama siasa na dini ziachwe kama dini!!
 
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR
Tarehe 27MAY2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.
Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.
Jumuia inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.
Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.
Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.
Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.
WABILLLAH TAWFIQ
 
picha za kanisa la kariakoo znz lilivyochomwa. Hawa jamaa nia yao siyo siasa tu, kuna chuki na udini nyuma yake.
Hawawezi kukaa bila migogoro hawa, hata wakiacha muungano watazua jingine tu

Hawa wanatakiwa jeshi la wananchi litumwe kule litembeze mbano kwa miezi kama mitatu hivi ili wawe na discpline! nimechukizwa mno na kitendo cha kuchoma kanisa! kwa nini wasiende kuchoma ofisi za magamba! au vituo vya polisi wanachoma nyumba ya mungu? hii laana haitwaacha salama hata muungano ukivunjika watabaki wanauana wao wenyewe!!
 
Hofu sio Kanisa, ni upotofu !Mara Mungu alikuwa mtu, mara alipigwa, mara kafa, mara kafufuka, mara ana baba'ke, mara ana mama'ke ! Sasa huyo mungu anatofauti gani na Mwingira au Kakobe ?

Ushauri wa bure, chambua imani yako ndipo utaeleweka; lakini kuchambua imani za watu wengine unajidharirisha tu!! Rudi kajipange upya.
 
Kuna Vikanisa uchwara vingi sana siku hizi.. vyenye wachungaji waendesha hummer na V8s! siku wakichoma KKKT au RC ndio ntawashangaa ila hivi vikanisa uchwara hivi kwanza ni bughudha tupu
 
Kwa hiyo hicho mnachokidai kimenyimwa na Kanisa mpk mlichome moto?

Hii ndio busara yenu mliorithi kwa waarabu. Utaitakaje haki usiyoweza kuwapa wengine? Hili linadhihirisha jinsi mlivyo wa hatari kama mkiachwa muendelee na huu ujinga wenu

Mkuu, naona kipovu kinakutoka. Punguza ghadhabu.
 
Muungano huu usio na tija kwa pande zote ndio utakuwa chanzo cha machafuko Tanzania.

Uvunjwe na Zanzibar iwe huru kujifanyia maamuzi yake. Una faida gani. Wabara hawautaki, Wavisiwani hawautaki. Huu Muungano unatakiwa na kanisa tu,

Punguza Udini japo mara moja tu katika maisha yako! Too much we mwanamke
 
Muungano huu usio na tija kwa pande zote ndio utakuwa chanzo cha machafuko Tanzania.

Uvunjwe na Zanzibar iwe huru kujifanyia maamuzi yake. Una faida gani. Wabara hawautaki, Wavisiwani hawautaki. Huu Muungano unatakiwa na kanisa tu,

Kanisa lipi mkuu? Maana yapo mengi sana.
 
Wa ZANZIBAR wanahofia sana wakisia jina la YESU linatajwa maeneo ya makazi yao,bse baadhi yao wanaishi na majini au wanategemea majini ili mambo yao yaende,na mabo mengine yasiyompendeza Mungu,sasa makanisa yanapozidi kuongezeka ZANZIBAR ina wapa hofu sana,lkn maandiko yanasema hayo yoote yatapita na mwisho wa siku JINA LA YESU litasimama na wote wataitambua kweli na itawaweka huru,ndo sababu wakichoma kanisa moja yanajenwa mengine matano,wanabaki kushangaa inakuwaje tunayachoma lkn bado yanazidi kuongezeka kwa kasi? hiyo ndo nguvu ya Injili.
 
Wanataka kukarubisha al-shabab wapeni nchi yao....,,, bara tutaanza kupokea wakimbizi toka zanzibar
 
Haya sasa, polisi kazi kwenu maana yake ni kuwa jamaa wa UAMSHO wamewakana waliokamatwa jana usiku sio wanachama wao, kwa kuwa UAMSHO imesema haihusiki na vurugu za kuanzia jana hadi leo. Sasa wakamateni, wateseni hadi watajane, wawe wamepatikana wengi wa kutosha ndio wafunguliwe mashtaka. Hawa uamsho wasije kurudi tena kudai waliokamatwa ni wanachama wao!
 
Mimi si Mzanzibari ni Mtanganyika tena ni Mtanganyika haswa, nilizaliwa wakati nchii hii haijabadilishwa jina na Nyerere na kupewa jina alilotoa Mhindi wa Tanga.

Moja katika makosa makubwa sana aliyoyafanya Nyerere ni huu Muungano, wakati alikuwa anashadidia Biafra itengane na Nigeria kwa masuala ya kidini alikuwa analazimisha Zanzibar iungane na Tanganyika, haya ndio matokeo ya maamuzi na utawala mbovu wa Nyerere.

Maslahi ya nchi hii hayapatikani na huu muungano usio na maridhiano. Mbona tuliweza kuivunja East African Community kwa kuwa haikuwa na maslahi kwetu kwa wakati huo? na sasa tunaingia katika kuziunganisha Afrika Mashariki kwa mazungumzo na njia zinazokubalika na wote.

Ili kuudumisha huu Muungano na ushirikiano wa ukweli, ni muhimu uvunjwe na zifanyike njia zinazokubalika na wote kuunda upya kama ilivyo kwa Afrika Mashariki.

Kikwete ukitaka muungano uwe imara kuuvunja ndio njia sahihi na kuanza mazungumzo upya ni vipi uwe muungano wa uhakika.

Hata madaktari wanapoirekebisha mifupa iliyoungika vibaya, huivunja kwanza na kuitengeneza vizuri. Kuuvunja Muungano ndio tiba ya huu Muungano si vingine.
Hivi hujui kuwa JK akiuvunja muungano na yeye anapoteza uhalali wa kuwa rais kwa katiba ya sasa? Tunahitaji kubadili katiba ambayo itatambua Tanganyika na Zanzibar huru na rais wa Tanganyika na rais wa Zanzibar wataratibu mapendekezo ya kuunda upya muungano.
 
Back
Top Bottom