Vurugu zaibuka kwenye kikao kati ya LATRA na wamiliki wa magari Mwanza

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Vurugu zaibuka katika kati ya LATRA na wamiliki wa magari, madereva

Vurugu zimeibuka katika kikao cha pamoja kati ya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji pamoja na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kutokana na wamiliki wa vyombo vya usafiri nchini kudai sheria zilizotungwa ni kandamizi kwani nitakuja kuwanyonya.

Kikao hicho, kiliwakutanisha wamiliki wa vyombo vya usafiriji, madereva pamoja na LATRA kwa lengo la kusiliza wadau hao kuhusu sheria mpya zilizotungwa ikiwemo ya madereva kuanza kuomba cheti kutoka LATRA kitakachomruhusu kufanya kazi hiyo.

Wamiliki wa vyombo vya usafiriji ambao wamesusia kikao hicho ni viongozi wa chama cha wamiliki (Taboa) ambao waliwakilisha wenzao kwenye kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza.

"Sheria ambazo mnatueleza hapa tayari zimepitishwa na bunge Sasa mnakuja kutueleza sisi hapa tufanye kitu gani?, hizi sheria tayari zimepitishwa hatuna cha kuzungumza sisi," alisikika mmoja wa wamiliki wa vyombo usafiriji.

Walisema kuwa, kabla ya LATRA haijatunga sheria hizo na kuzipeleka bungeni walipaswa kuwasikiliza wadau hao.

Na CHARLES CHARLES
*******

HABARI ZAIDI

Baadhi ya wadau wa sekta ya usafirishaji wametoka ndani ya mkutano wa kuchukua maoni ya kuboresha rasimu za kanuni mbalimbali zitakazotumika katika sheria ya uendeshaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra).

Kanuni hizo zinalenga kusimamia sheria namba 3 ya mwaka 2019 ya usafirishaji na uchukuzi chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Latra.

Tukio hilo la kususia mkutano huo limetokea leo Jumatatu Agosti 26, 2019 jijini Mwanza nchini Tanzania baada ya kudai kwamba mamlaka haiwasikilizi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wadau hao kutaka baadhi ya mambo yafanyiwe marekebisho kwenye sheria hiyo lakini Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Billiard Ngewe akasema kwamba hayawezi kubadilika kwa sababu tayari ni sheria ambayo imeshasainiwa na Rais John Magufuli wa Tanzania..

Katibu wa wamiliki wa Mabasi Kanda ya Ziwa (Taboa), Anwar Said amesema baadhi ya mambo ambayo wanataka yafanyiwe marekebisho lakini wanapingwa hivyo hawaoni sababu ya kuendelea kujadili na kutoa maoni hao.

"Miongoni mwa mambo ambayo yanaleta mkanganyiko ni pamoja na kuingiliana kwa mamlaka kati ya Latra na traffic, sheria ya usalama barabarani inatoa mamlaka ya kukagua na kuthibitisha ubora wa gari, sheria ya Latra inampa mamlaka Ofisa wa Latra kufanya hivyo," amesemana

"Kifungu cha 16 cha sheria ya usalama barabarani kinatoa jukumu la kuripoti ubadilishwaji wa umiliki wa gari kwa msajili wa magari ndani ya siku saba za kubadili kwa umiliki, lakini sheria ya Latra kinamtaka mmiliki juu ya hitaji hilohilo huu ni mwingiliano wa kimamlaka bila sababu,” amesema

Makamu mwenyekiti wa Taboa kanda ya Ziwa, Elia Ernest amesema sheria inasema lazima kumnunulia sare na kitambulisho kondakta na dereva ila akikamatwa bila kuvaa vitu hivyo anawajibishwa mmiliki jambo ambalo sio sahihi.

Naye mwenyekiti wa chama cha wa usafirishaji wa abiria daladala mkoa wa Mwanza, Ysuph Lupiga amesema Latr hawajajipanga kuwaita wadau kutoa maoni hao hivyo ni vyema wakaahirisha ili wajipange upya na hakuna maana iwapo tayari sheria hiyo imeshapitishwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Ngewe amesema mamlaka hiyo haina uwezo wa kubadilisha sheria ambayo imeshasainiwa na Rais.

Hata hivyo, alipofuatwa kutaka kufafanua zaidi kuhusu jambo hilo alisema hana cha kuongea bali yeye amemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi katika shughuli hiyo hivyo hana cha kufafanua zaidi.

Washiriki wa kikao hicho ni wa usafirishaji wa abiria kwa mabasi makubwa, daladala, bodaboda, bajaji, magari ya mizigo na teksi.
 
wanataka justification bila kuwepo ushirikishwaji_
nb. Bora ukoloni wa mwingereza urudi.
 
Sasa driving license ina certify nn na LATRA driving certificate ita certify nn Ambapo kukipata tu lazma kuna application fee bado Ada ya kila mwaka
 
Back
Top Bottom