Vurugu za Z’bar zimeacha maswali pasipo majibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vurugu za Z’bar zimeacha maswali pasipo majibu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, Jun 19, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"][​IMG][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 18 June 2012 21:16 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  TUMESIKITISHWA sana na vurugu zinazotokea Zanzibar mara kwa mara na kutoa picha kwamba pengine visiwa hivyo vinaelekea kule vilikotoka. Baada ya takribani miaka miwili ya utulivu, utengamano na maridhiano miongoni mwa Wazanzibari kutokana na kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, inasikitisha kuona vurugu na uvunjifu wa amani vinarejea tena katika visiwa hivyo, ingawa mara hii vikiwa na sura tofauti.

  Itakumbukwa kwamba wiki kadhaa baada ya Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (Jumuki) kufanya mihadhara iliyosababisha vurugu, umwagaji damu na uharibifu wa mali katika visiwa hivyo na kuilazimu polisi kutumia nguvu za ziada kuwatawanya wafuasi wa jumuiya hiyo, hali kama hiyo ilitokea tena juzi na kusababisha hali ya sintofahamu.

  Tunaambiwa Polisi walitumia mabomu kuwatawanya wafuasi hao waliokuwa wakielekea katika moja ya misikiti katika Jimbo la Dole kwa lengo la kufanya mhadhara, ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yao ya kutaka Zanzibar ijitoe katika Muungano. Polisi wanasema wafuasi hao wa jumuiya hiyo walikuwa wakitokea Mkoa wa Mjini Magharibi na kuelekea Mkoa wa Kaskazini Unguja kabla ya kuzuiwa na kutakiwa kurudi walikotoka.

  Inasemekana kwamba polisi walipokea barua kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ya kuzuia jumuiya hiyo kufanya mhadhara katika mkoa huo kutokana na wananchi wa mkoa huo kupinga kutumiwa kwa misikiti kwa shughuli za kisiasa kama jumuiya hiyo ilivyokuwa ikidaiwa kufanya. Pamoja na jeshi hilo la Polisi kuzuia mhadhara huo, viongozi wa jumuiya hiyo walikaidi amri hiyo na kuwaamuru wafuasi wao kuandamana kuelekea katika eneo walikopanga kufanya mhadhara huo.

  Ndipo Polisi walipolazimika kulipua mabomu ya machozi yaliyowasambaratisha wafuasi hao, wakiwamo wanawake na watoto, huku wafuasi wengine wakikimbilia katika misikiti ya jirani ambako walifuatwa na kutiwa mbaroni. Zipo taarifa kwamba baadhi ya wafuasi hao walipata majeraha kutokana na purukushani hizo na kupelekwa hospitalini kwa matibabu.

  Tumelazimika kutoa mlolongo wa sakata zima la juzi kutokana na unyeti wa mgogoro wenyewe. Kwa upande mmoja, lazima tukubali ukweli kwamba Polisi kupambana na kutumia nguvu kuwasambaratisha wafuasi wa kikundi cha dini kilichosajiliwa kisheria siyo jambo la kawaida na pengine ndiyo sababu hata viongozi wa jumuiya hiyo wamekiri kwamba walikaidi amri ya Polisi ya kuwataka watawanyike. Lakini kwa upande wa pili, viongozi hao walipaswa kutambua kuwa, pamoja na kuwa na haki kikatiba kukusanyika na kufanya mihadhara, walikiuka sheria za nchi kwani Serikali ya Zanzibar tayari ilikuwa imepiga marufuku maandamano na mihadhara kwa muda kufuatia vurugu zilizotokana na mihadhara hiyo wiki kadhaa zilizopita.

  Vurugu hizo lazima zitufumbue macho na kuona umuhimu wa wananchi, wakiwamo viongozi wa madhehebu ya dini kuheshimu sheria za nchi. Kama Polisi walizuia maandamano na mihadhara kutokana na Serikali kuipiga marufuku, tungetegemea viongozi wa jumuiya hiyo waende mahakamani kupinga hatua hiyo ya Serikali badala ya kupambana na Polisi waliokuwa wanatekeleza amri halali ya Serikali.

  Kwa muda mrefu sasa umekuwapo utamaduni wa baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini hapa nchini kujenga dhana potofu kwamba unyeti wa madhehebu ya dini wanazoziongoza unawafanya viongozi hao wawe juu ya sheria na katiba ya nchi. Wanashindwa kutambua kuwa, pamoja na haki ya kuabudu na haki nyingine nyingi, haki hizo za kikatiba zinazo taratibu zake zinazopaswa kufuatwa na kuheshimiwa. Haki hizo zina chimbuko na misingi yake na asitokee mtu yeyote kujaribu kutushawishi kwamba haki hizo zinaelea tu angani.

  Sisi tunadhani kwamba mwelekeo wa Zanzibar hivi sasa hauleti matumaini kimaendeleo na kiustawi na kwamba vurugu zinazoendelea visiwani humo zinaibua maswali mengi yasiyo na majibu. Tunazishauri mamlaka husika zichunguze kiini cha vurugu hizo kwani dalili zote zinaonyesha kwamba nyuma ya vurugu hizo ipo ajenda ya siri.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wenyekuleta Fujo na vurugu Zanzibar ni hawa Amiri Jesh Mkuu Kikwete na Huyu Ndugu yake Wa Kitanganyika Waziri wa mambo ya Ndani Mjimbi.

  Mambo hupikwa Tanganyika yakapakuliwa Zanzibar kwa kisingizio kuwa Ulinzi ni swala la Muungano ok, lakini Jee huo Muungano wenyewe ni kwa nini usijadiliwe na baadae Polisi kuamriswa kutumia nguvu zidi ya raia na Wananchi wa Zanzibar.

  Ikiwa Muungano ni ridhaa ya watu wa Pande mbili husika jee una siri gani hata uekewe hadidu Rejea katika Katiba kuwa Muungano usijadiliwe na Mjumbe wenye kuchukuwa maoni ya Muungano atafukuzwa na kupewa azabu ,Jee kuna urudhaa gani hapa.

  Ndio tukasema Wazanzibar hatuko huru baada ya kufanya mapinduzi ya kumuondosha Muarabu ili tuwe huru mara tumenyakwa na Mkoloni Mweusi Tanganyika, jee hii ni haki mutufanyiayo?.

  Hivi sasa viongozi wetu wa Smz kimya kuhusu vitimbi hivi mutufanyiavyo na ukiwauliza husema amri hutolewa kutoka Tanganyika sio sisi swala la ulinzi ni la Muungano japo kuwa sisi linatuma lakini tuko pamoja.

  Sasa hii ni ile ya Tanzania Nyerere kutetea Ubaguzi na kupewa uhuru wake Southafrika na Biafra lakini kumbe ni ndumi la kuwili kwa Wazanzibar.

  Ishallah kila mukifanya hivi ndio kutuchonga ukali na kufanya tuwashukie zaidi katika jamii yetu ya kizanzibar na kuwafundisha watoto wetu nyiyi ni watu wa aina gani.

  Mungu ibariki Zanzibar na watu wake.
   
 3. j

  john paulo masanger New Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vurugu za Zanzibar ni kudharauliwa kiliyo cha Wazanzibari wlio wengi, kwa kunyimwa fursa ya kutoa maoni yao kuhusu suala la Muungano, inasikitisha kuona serikali zote mbili [SMT na SMZ] kuogopa kuwapa fursa wananchi wao kutoa maoni yao kuhusu huu Muungano, tusiwalamu jumuiya ya Uwamsho kwani wao wanawasemea wananchi wote wa Zanzibar, msimamo wa uwamsho ni msimamo kwani hata Wawakilishi wote ktk baraza walikuwa na msimamo kama wa Uwamsho, serikali zote mbili zinapaswa kulichukulia uzito matakwa ya wazanzibar ya kuitisha kura ya maoni, kabla mambo hayajaharibika . waulizwe wananchi wangapi wanataka muungano, nawangapi hawautaki mungano, hizi vurugu zote zitakwisha. la asiyesikia la mkuu ......, zumari likipulizawa Zanzibar basi watu maziwa makuuu ngoma...
   
 4. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  mzee
  1 na 2 hapo inaonyesha unatoa povu la lugha ya kiswazi
  no 3 bi kwamba SMZ ipo ndani ya SMT so uozo wa serikali ni mmoja si bara wala visiwani.
  hapa ni kuwatoa ccm tu. pia kama ni kujadili muungano kijadiliwe nini wakati inaeleweka waunguja hamtaki muungano? hapa mjue kwamba wanaowabania muungano usivunjike ni viongozi wa ccm tu na si mwananchi mwingine maana hata mimi siutaki muungano, upuuzi tu.
   
 5. Imam Yussuf Shamsi

  Imam Yussuf Shamsi Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wachangiaji wa bajeti ya Zanzibar karibuni wote, hawakuacha kuzungumzia suala la muungano, kuna wanaoupinga kabisa na hata wale wasaka tonge wa magamba, wameelezea kutokuridhishwa kwao juu ya mfumo tulionao sasa, wakieleza kuwa ni mbovu na ingependeza ukabadilishwa.
   
Loading...