Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 10,335
- 17,850
Vitendo vinavyofanywa na raia wa Afrika Kusini dhidi ya maisha na mali za Wahamiaji ni vitendo viovu ambavyo vinapaswa kulaaniwa na Waafrika wote.
Bara la Afrika ni moja na mipaka iliwekwa mwishoni mwa karne ya 18 na Wakoloni ili waweze kututawala kiurahisi na kupora mali asili yetu.
Pamoja na hizo vurugu zinazofanywa dhidi ya wahamiaji kuna mambo kama 6 yanayopelekea vurugu hizo zitokee;
1. Wahamiaji kutoka Zimbabwe wanakimbia uchumi mbovu ambao umeharibiwa na viongozi wao (Robert Mugabe 1980-17 na sasa Mnanhagwa). Laiti Robert Muhabe asingeleta sera ya kugawa ardhi ya Masetla kwa Maveterani wa vita vya ukombozi wa Zimbabwe mwaka 2000, uchumi wa Zimnabwe usingevurugika na Wazimbabwe wasingekimbikia South Africa kutafuta vibarua.
2. Wahamiaji wanaoshambuliwa ni haramu (undocumented). Wameingia kwa njia za panya. Wameroroka nchini kwao na kutopita kwenye mifumo ya Uhamiaji. Kwa mfano vijana wa Tanzania wengi hawana hata uwezo wa kuishi nyumba za kupanga. Aidha wanalala kwenye korido za majumba makubwa au kwenye magari mabovu maeneo ya garage. Wengine hulala kwenye meli mbovu katika majiji yaliyoko pembezoni mwa bahari.
3. Wahamiaji haramu hawana sifa (skills) za kuwawezesha kufanya kazi za kitaalamu kule hivyo huishia kufanya biashara haramu kama ; kuuza mihadarati, kufanya ukahaba, kuuza silaha na ujambazi wa kutumia silaha.
Watanzania hufanya biashara za uganga wa kienyeji, kuuza karanga na nyanya, kuuza kete za bangi nk
4. Katika kitovu cha Johannesburg maarufu kama Hilbrough, Wanaigeria ndiyo wamiliki wa majumba makubwa baada ya Wazungu kukimbia uharamia unaofanyika. Katika eneo hili ndiyo biashara ya silaha, mihadarati na ukahaba umekithiri
5. Wahamiaji haramu wako tayari kufanya kazi yeyote kwa mshahara wowote watakaopewa na Kaburu. Kitendo hiki kinawakwaza Wenyeji kwa vile wanataka kulipwa kadri ya bei ya soko. Wenyeji wana vyama vya wafanyakazi vilivyo imara, hivyo basi mara nyingi hufanya mgomo. Wakati wa mgomo Kaburu huwaajiri Wahamiaji, na hapo ndipo chuki kutoka kwa Wenyeji inapoanzia.
Wito Wangu;
Nchi zote zilizo kaskazini mwa Afrika ya Kusini ziweke mazingira wezeshi kwa vijana kupata ajira ikiwa ni pamoja na matumizi ya Raslimali zao za asili vizuri. Botswana iko karibu sana na South Africa lakini tatizo la wahamiaji si kubwa kama Tanzania Mozambique na Malawi