Vurugu za UAMSHO Zanzibar: Polisi auawa kikatili...

Wimana

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
2,449
717
Kufuatia kutoweka kwa Sheikh Farid na wafuasi wake kuvamia na kuharibu Ofisi za CCM jana huko Zanzibar, usiku wa jana, wafuasi wa uamsho wamemuua kikatili PC Said alipokuwa akitoka kazini.

Source: TBC Asubuhi hii

My Take
Haya ndio matokeo ya kufumbia macho hiki kikundi cha Wanaharakati wa Kiislamu. Iliwahi kuhojiwa humu ndani, kwa nini Serikali inashindwa kufuta usajili wa Uamsho Zanzibar?

Je, kuvamiwa na kuharibiwa kwa Maskani za CCM, haonyeshi kuwa kikundi hicho ni cha Kisiasa kinachotumia dini?
 
taarifa nilizopata leo ni kuwa katika vurugu jana askari polisi mwenye cheo cha koplo amechinjwa jana na waandamanaji wa uamsho..
Aliyeko zanzibar anaweza kutupa habar zaid
whaaat!!!!!!!!!!!!!!!! Inasikitisha sana kucheka na nyani sasa wanavuna mabua omg rip coplo
 
Ivi nikweli hili group la uhamsho lina nguvu kuliko heshi la polisi ?Yaani mmilikiwa mbwa anang'atwa na mbwa wake..
 
Bado binafsi sioni kweli kama hili linatosheleza kwa waislam kufikia hatua waliyo fikia. Katika miaka ya 1980s nilikuwa na marafiki majirani na jamaa waislam lakini tulionana hivyo bila kuwa na shaka yeyote hv sasa sipati amani nikiwa karibu ya kundi la waislam wanaozidi wawili hasa wanaovaa kaptula ndefu.

I wonder what happened sasa napata mashaka ikiwa madai kuwa uislam ni dini ya amani kweli. Maana wanayofanya wanaya justify kupitia vitabu vyao this is so bad.
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo,haya ni matokeo yake na utaona sasa Serikali inashughulika na matokeo badala ya chanzo kama kawaida yao.
 
Matunda ya udhaifu wa serikali, wahenga walisema, "mafahali wawili hawakai zizi moja"
 
Makanisa yalichomwa hakuna aliyekamatwa.Sasa hali inazidi kuwa mbaya...lets see kama serikali itafumbia macho na hili pia.
 
.....mambo ya ngoswe aachiwe ngoswe mwenyewe...nachoshauri ni kwamba vurugu zikizidi...tuzuie vyombo vya abiria kuja bara...somo la wakimbizi (wawe wa ndani au nje) tulishalielewa sawia..chambilecho wasemaji wa kiswahili.."hata mbuyu ulianza kama mchicha"..."somalia nyingine hiyooo!! yaja!!
 
Hadi watakapo ua kiongozi mmoja ndo serikali itachukua hatua. We angalia walochoma makanisa znz wamefanywa nini. Hata hapa utasikia tu Tunalaani mauaji ya askari wetu hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika.
 
Back
Top Bottom