Vurugu za Uamsho zanzibar CCM kutoa msimamo wake tarehe 09/06/12 saa sita mchana

KOMBAJR

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
5,827
1,271
Heshima kwenu Wanabadi, Asubuhi ya leo wakati nieleke kujitafutia riziki nimekutana na hilo bandiko hapo juu katika makutano ya bara bara za jiji.

Nimeona ni Vizuri tukalijadili sababu baada ya kulisoma nikawa na maswali mengi ambayo sikuwa na majibu!

Jadili mapungufu au mashiko ya Bango hili
 
Nimeliona pale Ubungo mataa, sijaona sababu ya kuweka mabango kwa ajili ya tamko tu. Halafu ni bango lenye mapungufu, mbona halijasema wanatoa tamko kupitia chombo gani cha habari?
 
Yani wamefikiria weee wakaona hio ndio itakua kivutio cha mkutano???!!!!!!!!!! pumbaf zao kabisa
 
Nadhani kama kawaida yake m/kiti alikuwa anasubiri ridhaa ya Kamati Kuu!
 
He! Kweli hii kali, jingine liko Mwenge. Limeandikwa hivi: UZURI WA KANGA MANYOYA, UZURI WA CCM SERA ZAKE. Ha ha haaa! Naona Nape kaanza kutoa silaha za maangamizi.
 
Mungu mpe busara nape maana jana amesema haina haja kwa wazanzibar kihoji juu ya muungano kwani asili yake ni nyerere na karume je leo tutoe nchi kwa mtu aliyekufa nape usije ukammkanyanganyoka mkiani utapotea sisi tuna mungu wewe una nini mwenzetu.
 
Binafsi sioni tatizo hapo labda baada ya kulisikia hilo tamko litakalo tolewa, na CCM kama chama chenye wanachama wake kule Z'bar hawana budi kutoa msimamo wao ili kujiweka kwenye safe side ikiwa ni pamoja na kuwatoa shaka wanachama wake"

Hebu tulisikie hilo tamko ili tujadili kwa mapana zaidi.
 
Nimeliona pale Ubungo mataa, sijaona sababu ya kuweka mabango kwa ajili ya tamko tu. Halafu ni bango lenye mapungufu, mbona halijasema wanatoa tamko kupitia chombo gani cha habari?

Lipo pia Mapipa ila halizungumzi hilo tamko litatolewa wapi na nani
 
Watuamabie kauli ya mwenyekiti wao kukataza watu kujadili muungano ilichangia kiasi gani vurugu Zanzibar...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom