Vurugu za Kisiasa Tanzania, turudishe chama kimoja

Nilikuwa sahihi kusema umesoma kichwa cha habari tu, na ukahitimisha kwa hisia. Lunyungu nakushauri uchukue tabia ya kiume ambayo haiongozwi na hisia. Isije ikawa unaozeefu unaoongelea ni wa hisia hisia. Sasa acha mawazo yako mgando ya hisia, soma habari yote kisha toa hoja zinazoambatana na matukio halisi acha hisia.

Watu wajuvu walio jibu hapa nimesoma mawazo wakiwa wamesoma ujumbe majibu yao hayana tofauti na yangu ambaye sikusoma . Again mkiwa mnatumwa kuja JF waambieni kwamba kule si mahali kusema hovyo . Yaani NEC nzima ya CCM akiwamo JK kumsikiliza kihiyo Guninita kwamba Sitta abwage kadi na afukuzwe kisa ulaji . Kaka si hapa .Sikuhitaji kupoteza muda na wale walio amua kua sacrifice muda wamesema kama mimi bado wataka nikasome utumbo ?
 
1.
1. Vurugu za kisiasa...... zinatoa fundisho moja kubwa kuwa vyama vingi havijengi umoja wa kitaifa.

2. umuhimu wa kurudisha mfumo wa chama kimoja ili kudumisha umoja wa Watanzania.

3. Kuna mlolongo wa matukio ya kutoweka kwa amani .. huko Zanzibar sambamba na uandikishaji wa wapiga kura ni mifano inayoonyesha kuwa mfumo wa vyama vingi hautufai Tanzania.

4. Kwa maoni yangu mfumo wa chama kimoja utarejesha umoja unaotoweka kati yetu Watanzania.

- Mkuu hebu soma tena mwenyewe hoja zako, hapo juu the main theme yako ni kwamba mfumo wa chama kimoja ndio solution ya vurugu ya siasa nchini kwetu, na kwamba sasa hivi tuna vurugu za kisiasa ambazo chanzo chake ni vyama vingi vya siasa.

- Halafu soma hapa chini hoja zako mwenyewe, unavyojichanganya kwamba tatizo sio vyama vingi vya siasa, ila mishahara na marupu rupu ya wanasiasa ndio chanzo cha vurugu unayoiita ya kisiasa nchini:-

5. Vinginevyo ili kokomesha vurugu za kisiasa ....hatuna budi kuishinikiza serikali ipunguze mishahara na marupurupua ya wanasiasa ili Watanzania wasikimbilie kwenye siasa na hivyo kusababisha kutoweka amani katika nchi yetu.

6. Kama kipato katika sekta mbalimbali za maisha katika nchi yetu kitakuwa na usawa, vurugu za kisiasa hazitakuwepo

7. haitatatua vurugu za kisiasa mpaka sekta zote ziwe na uwiano sawa wa kipato cha fedha.

8. , Watanzania tudai kwa nguvu nchini kote kupunguzwa kwa mishahara na marupurupu ya wanasiasa na kuongezwa katika sekta nyingine ili amani idumu Tanzania.

8. Vinginevyo tukishindwa hili turudishe mfumo wa chama kimoja.

- Huku chini wewe tena unasema tatizo la vurugu za siasa nchini mwetu sio vyama vingi, ila ni mishahara na marupu rupu ya wanasiasa, sasa mkuu naomba uchague exactly unataka nini hasa kati ya chama kimoja na mishahara ya wanasiasa?

- Isipokuwa mawazo ya chama kimoja ni out of the line, hayana nafasi tena katika taifa letu, tatizo tulilonalo ni elimu ndogo sana ya siasa kwa wananchi wetu, ndio maana wenye elimu kubwa kidogo yaani baadhi ya viongozi wetu wanaweza kuwatumia hawa wananchi wa chini na wapiga kura wenye elimu ndogo ya siasa na kuleta hizi vurugu ambazo ni very isolated tena kwa small scale,

- Hoja yako ya vurugu za siasa nchini haina nguvu kabisa kwa sababu mkuu Tanzania ni taifa kubwa sana lenye wananchi karibu millioni 40, sasa eti unasema kupotea maisha kwa wananchi wake 27, miaka kadhaa iliyopita iwe ni sababu ya ku-reverse a progressive political multparties idea kwa wananchi wake waliobaki? Are you serious au unatania mkuu?

- Mkuu hivi unajua katika maamuzi ya kitaifa huwa kuna risk factors ambazo lazima ziwe weighed na viongozi wa juu hasa Usalama wa Taifa na Rais mwenyewe kabla ya ku-introduce any new law kwa taifa? Sasa nenda huko serikalini watakusaidia kuelewa kwamba walipokuwa wanapitisha huu mswaada wa vyama vingi, kulikuwepo na studies ambazo ziliweka wazi the risk zake ambazo lazima iwe pamoja na vifo vya wananchi wachache, sasa ukihesabu vizuri katika wananchi millioni 40, ukipoteza 27 tu as a sacrifice basi hilo zoezi limefanikiwa tena bigtime, kwa sababu the end justifies the means mkuu,

- Mkuu mawazo yako ya kutaka kurudi nyuma kweusi kwa sababu ya vifo 27, kati ya wananchi millioni 40, ni misguided na very mis-informed, na inasikitisha sana hata kukubaliwa kuwekwa hapa JF, tena hapa kwenye uwanja wa siasa.

Respect.

Field Marshall Es!
 
Vurugu za kisiasa zinazotokea Zanzibar kwa sasa na sehemu zingine wakati wa uchaguzi Tanzania bara zinatoa fundisho moja kubwa kuwa vyama vingi havijengi umoja wa kitaifa. Ingawa inaweza kuonekana kama wendawazimu lakini tukubali, tusikubali kuna umuhimu wa kurudisha mfumo wa chama kimoja ili kudumisha umoja wa Watanzania.

Kuna mlolongo wa matukio ya kutoweka kwa amani ambayo yametokea ndani ya vyama vingi. Matukio ya mauaji ya watu wasiopungua 27 huko Zanzibar wakati wa utawala wa Mkapa, uchomaji moto wa nyumba unaoendelea huko Zanzibar sambamba na uandikishaji wa wapiga kura ni mifano inayoonyesha kuwa mfumo wa vyama vingi hautufai Tanzania. Si hayo tu, kule Tarime wakati wa uchaguzi mdogo wa mbunge baada ya kifo cha Mh. Wangwe zilichochewa na kuwepo kwa mfumo wa chama kimoja. Si hayo tu, vurugu zilizotokea kule Kiteto pia wakati wa uchaguzi mdogo zinatufanya Watanzania tufikirie upya demokrasia ya vyama vingi ambayo tumenakili kutoka ulaya. Hata kura za maoni kuhusu kuanzisha vyama vingi zilionyesha asilimia 90% kutaka kuendelea na mfumo wa chama kimoja. Hili linaweza bishaniwa kuwa kura ya maoni haikuwa huru. Lakini haiondoi ukweli wa kutoweka kwa amani tunakoona sasa nchi kwetu.

Ingawa wengine wanaweza kusema kuwa mfumo wa vyama vingi unasaidia kumeza utengano wa aina nyingine kama ukabila, udini, ukanda n.k. lakini siasa za Tanzania zimesaidia sana kumomonyoa umoja wa Watanzania. Ukabila na udini unatumika kama mtaji wa kisiasa. Kwa maoni yangu mfumo wa chama kimoja utarejesha umoja unaotoweka kati yetu Watanzania.

Vinginevyo ili kokomesha vurugu za kisiasa yatupasa sasa kupanua wigo wa Mapambano nchini petu. Wana harakati, wafanyakazi wa sekta binafsi naya umma, wafanyabiashara na wakulima hatuna budi kuishinikiza serikali ipunguze mishahara na marupurupua ya wanasiasa ili Watanzania wasikimbilie kwenye siasa na hivyo kusababisha kutoweka amani katika nchi yetu. Kwa mfano kodi kwa wafanya biashara na wafanyakazi zinatakiwa ziwe za haki. Kama kipato katika sekta mbalimbali za maisha katika nchi yetu kitakuwa na usawa, vurugu za kisiasa hazitakuwepo kwa sababu kila mtu atachagua pa kufanya kazi na kipato hakita pishana. Madaktari watabaki mahospitalini, pia manesi na wafamasia, walimu wataendelea kufundisha shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Pia wakulima wataendelea na kilimo na hawatadanganyika kununuliwa Tshirt na kufia. Pia wafanya biashara watabaki kwenye biashara. Sheria inayosemwa na JK ya kutenganisha biashara na uongozi haitatatua vurugu za kisiasa mpaka sekta zote ziwe na uwiano sawa wa kipato cha fedha. Hiki ndicho kipaumbele kinachotakiwa kwenda sambamba na vita dhidi ya ufisadi, Watanzania tudai kwa nguvu nchini kote kupunguzwa kwa mishahara na marupurupu ya wanasiasa na kuongezwa katika sekta nyingine ili amani idumu Tanzania. Vinginevyo tukishindwa hili turudishe mfumo wa chama kimoja.

Kwa sababu internet inaunganisha na websites zinazoonyesha mambo ya porno, basi cha muhimu ni kutumia computers zisizo kwenye mtandao.

Kwa sababu magari yanasababisha ajari mbaya, basi tuache kusafiri.

Perfection haiji kwa kurudi kwenye ujima.
 
Watu wajuvu walio jibu hapa nimesoma mawazo wakiwa wamesoma ujumbe majibu yao hayana tofauti na yangu ambaye sikusoma . Again mkiwa mnatumwa kuja JF waambieni kwamba kule si mahali kusema hovyo . Yaani NEC nzima ya CCM akiwamo JK kumsikiliza kihiyo Guninita kwamba Sitta abwage kadi na afukuzwe kisa ulaji . Kaka si hapa .Sikuhitaji kupoteza muda na wale walio amua kua sacrifice muda wamesema kama mimi bado wataka nikasome utumbo ?

Ninasikitika sana kuwa unapenda sana kutanguliza hisia, hili sina cha kukusaidia. Ila japo leo vunja mwiko usome angalau aya ya mwisho uelewa ninasisitiza nini. Kimsingi tusingekuwa na tofauti kubwa kiasi hiki. Ukisoma pale utaelewa kuwa ki-msingi msisitizo ni kutatua vurugu za kisiasa katika mfumo wa vyama vingi. Soma mara moja aya hiyo, na irudie tena. HIvi kama mkulima maisha yake yangewezeshwa angedanyika na rushwa za T shirt na kofia za kijani na njano? Nani atadanganyika kwa chumvi kama maisha yake ni mazuri? Changamoto hapa ni kuwalazimisha wanasiasa wa CCM, kupunguza maslahi ya wanasiasa. Na utakumbuka hata Slaa alikataa sana kuongezwa maslahi ya wanasiasa huku watanzania wengine wanabaki hohehahe. Ninakuomba soma hiyo aya ya mwisho, unganisha na haya ninayoeleza hapa. Suala la Guninita linatoka wapi, kwanza ndiyo mdudu gani huyu aitwaye Guninita?
 
1.

- Huku chini wewe tena unasema tatizo la vurugu za siasa nchini mwetu sio vyama vingi, ila ni mishahara na marupu rupu ya wanasiasa, sasa mkuu naomba uchague exactly unataka nini hasa kati ya chama kimoja na mishahara ya wanasiasa?

-- Mkuu mawazo yako ya kutaka kurudi nyuma kweusi kwa sababu ya vifo 27, kati ya wananchi millioni 40, ni misguided na very mis-informed, na inasikitisha sana hata kukubaliwa kuwekwa hapa JF, tena hapa kwenye uwanja wa siasa.

Respect.

Field Marshall Es!

Naomba nikushukuru kuwa umeona wazo la msingi nililosisitiza. Ki msingi tatizo ni mishahara, pension, na hata katika biashara watu hutozwa kodi kubwa. Suala la chama kimoja na vyama vingi ni mlinganisho niliotoa ili kuonesha kuwa pamoja na kuwa katika mfumo wa vyama vingi tuna tatizo la kutatua. NImemjibu Lunyungu na kumshauri asome aya ya mwisho, nawe pia soma ile aya. Pale nimesema kuwa suala la wanasiasa kurundikiwa maslahi ni chanzo kikuu cha vurugu katika vyama vingi. HIli limepigiwa kelele sana na Dr. Slaa wa Chadema, bahati mbaya sana wanaharakati hata wa JF hawajaona kuwa hili ni tatizo. CCM haitang'ang'ania madaraka ikiwa kila sekta maisha ni mazuri. Hawa CCM wanaua wafuasi wa vyama vya siasa kwa sababu ya kukimbilia maslahi ya kisiasa.

Suala la kusema kuwa watu 27 ni sawa tu kufa siyo sahihi kwa sababu kila mtu anahaki ya msingi ya kuishi. Hatuwezi kuhalalisha CCM kuua eti ni watu wachache. Habari ya kuchagua JF ni uhuru ambao wewe na mimi tunautumia katika kuhamasisha maendeleo ya nchi yetu. Mwisho soma majibu yangu kwa Lunyungu, unganisha na haya hapa na soma aya ya mwisho utaona kuwa ujumbe mkuu niliokusudia ni KULETA USAWA WA MASLAHI KATI YA WANASIASA- MAWAZIRI, RAIS, WABUNGE, n.k ILI MFUMO HUU WA VYAMA VINGI USIWE SABABU YA NDUGU ZETU KUUAWA.

Nashukuru kwa mchango wako.
 
1. Naomba nikushukuru kuwa umeona wazo la msingi nililosisitiza.

2. Ki msingi tatizo ni mishahara, pension, na hata katika biashara watu hutozwa kodi kubwa.

3. Suala la chama kimoja na vyama vingi ni mlinganisho niliotoa ili kuonesha kuwa pamoja na kuwa katika mfumo wa vyama vingi tuna tatizo la kutatua.

4. Pale nimesema kuwa suala la wanasiasa kurundikiwa maslahi ni chanzo kikuu cha vurugu katika vyama vingi.

5. HIli limepigiwa kelele sana na Dr. Slaa wa Chadema, bahati mbaya sana wanaharakati hata wa JF hawajaona kuwa hili ni tatizo.

6. CCM haitang'ang'ania madaraka ikiwa kila sekta maisha ni mazuri. Hawa CCM wanaua wafuasi wa vyama vya siasa kwa sababu ya kukimbilia maslahi ya kisiasa.

7. Suala la kusema kuwa watu 27 ni sawa tu kufa siyo sahihi kwa sababu kila mtu anahaki ya msingi ya kuishi. Hatuwezi kuhalalisha CCM kuua eti ni watu wachache. .

- Mkuu kama ninakuelewa, basi kichwa cha mada yako na maelezo hayafanani kabisaa, unaanza na kusema Tanzania tuna vurugu za kisiasa, ukweli ni kwamba hatuna,

- Unaongelea vifo vya wananchi 27, waliouliwa Visiwani under utawala wa Mkapa, kwamba ndio iwe sababu ya kurudi miaka 15 nyuma kwenye utawala wa chama kimoja, another myth kwa sababu kama wananchi 27, wamepoteza maisha kwa the good of the 40 Million people waliobaki, hakuna ubaya wowote mkuu, unless unasema tuwaite wakoloni warudi kwa sababu kwenye vita vita vya maji maji na Mkwawa, tulipoteza wananchi zaidi ya 27, that is absurd mkuu!

- kwanza umeshindwa sana kuonyesha kwamba Tanzania tuna vurugu politically ambayo ni large scale kwamba tunahitaji kutafuta solution nationally, halafu pia umeshindwa kuonyesha how vyama vingi ni tatizo kisiasa nchini, na sio progress kama wengi tunavyoona na kuamini,

- Mkuu we are better off na vyama vingi kuliko chama kimoja, hiyo sio siri wala ishu for debate, kwamba leo Tanzania tuko way juu na siasa kuliko wakati wowote wa maisha ya uhuru wetu, na ninaomba kurudia tena kwamba vifo vya wananchi 27, kwa ajili ya the good of the future of our nation politically ni okay kwanza ni wachache sana, na inakubalika na hata international community, kama huamini tizama Rwanda, hivi wamekufa wananchi wangapi kufikia walipo sasa, sasa kwa mantiki yako Rwanda warudishe yale mambo yao ya Bagaza kwa sababu wananchi waliokufa kufikia walipo ni wengi sana?

- Mkuu vipi nenda usome history, maendeleo ya China leo wananchi wangapi walikufa as a sacrifice, ni miananchi mioga ndiyo siku zote inatumiwa na viongozi wetu uchwara kuturudisha nyuma kwa visingizio kama vyako, eti kwa sababu wamekufa wanachi 27, basi wananchi waliobaki Millioni 40, wote turudi kwenye ujima, pole sana mkuu it does not make a sense! na sina sababu ya kusoma aya yoyote kati ya ulizoandika kuelewa kwamba huna hoja, kwa sababu maelezo yako hayafanani na kichwa cha mada yako,

- Na besides the idea tu ya kwamba turudi kwenye chama kimoja ni batili sana, yaani unasema Dr. Slaa arudi CCM?

Respect.

FMEs!
 
Tatizo hapa sio mfumo bali ni chama tawala kushikiliwa na viongozi wabinafsi na ving'ang'anizi wa madaraka. Hawataki kuweka uwanja sawa wa siasa kwa hofu ya kuong'olewa.
 
-
- Na besides the idea tu ya kwamba turudi kwenye chama kimoja ni batili sana, yaani unasema Dr. Slaa arudi CCM?

Respect.

FMEs!

Nilifikiri kuwa ni Lunyungu tu anaongozwa kwa hisia, kumbe hata wewe! hii ni hatari. Nadhani ni busara kujenga utamaduni wa kujadili kwa vitu halisi kuliko vya kufikirika. Mfano uliotoa wa China nina kupa alama kuwa umetoa hoja ya maana. Lakini kwa Tanzania sina kumbukumbu ya mauaji ya kisiasa kabla ya mfumo wa vyama vingi. Na bahati mbaya mauaji yanafanywa na CCM dhidi ya vyama vingine. Kama unaona mauaji wa watu 27 au vurugu zingine ambazo jeshi la polisi hutolea ngeu watanzania wasio na hatika ni kidu kidogo yakupasa kufikiri mara mbili kama kati ya hao 27 angekuwemo wewe au mimi, au baba yako ay baba yangu kuliko kushabikia mauaji ya kisiasa. Bado nasisitiza kuwa tuna tatizo la vurugu katika mfumo huu wa vyama vingi la kutatua na suluhisho ni kufyeka maslahi ya wanasiasa ili kuinua hali za maisha ya watanzania katika sekta nyingine. Vinginevyo ninakubali kutokukubaliana na wewe. Kwa vile hatukukubaliana siwezi kukulazimisha ukubali hoja ninazotoa na pia siwezi kukubali hoja yako kuwa watu waendelee kuuawa kisiasa kama unavyopendekeza. Kila mtanzania anahaki ya msingi ya kuishi na ni juu ya kila Mtanzania kutetea uhai. Kama unatetea mauaji mie sipo huko.
 
Tatizo hapa sio mfumo bali ni chama tawala kushikiliwa na viongozi wabinafsi na ving'ang'anizi wa madaraka. Hawataki kuweka uwanja sawa wa siasa kwa hofu ya kuong'olewa.

N kweli CCM inaviongoci wabinafsi. Lakini ubinafsi hapa unakolezwa kutokana na wao kujihalalishia maslahi makubwa mno kupita watanzania wengine. Kama Maprofesa vyuo vikuu wangekuwa wanalipwa vizuri au madaktari, leo hii tusingekuwa na wasomi wengi kukimbilia siasa. Kama Daktari angekuwa anapata milioni 50 baada ya miaka 5 kama bonasi ya kuhudumia watanzania au Profesa anapata milioni 50 kwa kazi nzuri ya kufundisha wimbi la wataalam hawa kukimbilia kwenye siasa lisingekuwepo au lingepungua na vurugu zingepungua pia.
 
Nilifikiri kuwa ni Lunyungu tu anaongozwa kwa hisia, kumbe hata wewe! hii ni hatari. Nadhani ni busara kujenga utamaduni wa kujadili kwa vitu halisi kuliko vya kufikirika.

- Mkuu ninaongozwa na hoja humu JF, na hasa masilahi ya taifa hisia sio masialhi ya taifa na haipo hapa JF, nowhere! Kinachokushinda ni kujenga hoja on uhalisi wa vurugu za kisiasa Tanzania ambazo hazipo, unachozungumzia ni small scale isolated political ishus, ambazo ni based na ukabila na udini, ambalo sio tatizo la taifa letu in general, hii sio hisia ni a true political analysis inayojali facts on the ground, haiwezi kuwa hisia.

Mfano uliotoa wa China nina kupa alama kuwa umetoa hoja ya maana. Lakini kwa Tanzania sina kumbukumbu ya mauaji ya kisiasa kabla ya mfumo wa vyama vingi.

- Ndio maana tunakukumbusha kwamba ili kupata uhuru wetu kuna kina Mkwawa na Maji maji ya Kinjekitile waliopoteza maisha yao kwa sababu ya kutaka kuwa huru, sasa kwa mantiki ya hoja yako, tuwaombe wakoloni warudi kwa sababu kuna damu ilimwagika, sasa kipi hapa usichoelewa?

- Hoja yako ni kwamba kwa sababu wananchi 27, waliuliwa under Mkapa, some few years ago, basi turudishe utawala wa chama kimoja, ninasema hivi hii hoja ni mufilisi na ni empty!

Na bahati mbaya mauaji yanafanywa na CCM dhidi ya vyama vingine. Kama unaona mauaji wa watu 27 au vurugu zingine ambazo jeshi la polisi hutolea ngeu watanzania wasio na hatika ni kidu kidogo yakupasa kufikiri mara mbili kama kati ya hao 27 angekuwemo wewe au mimi, au baba yako ay baba yangu kuliko kushabikia mauaji ya kisiasa.

- Mkuu JF, pamoja na kutoa ushauri mwingi wa kisiasa kwa watawala na vyama vyetu vya siasa, pia tunayarisha viongozi hapa mkuu, watu ambao wakipewa madaraka, hawatasita kutoa maamuzi magumu kwa ajili ya the best interest of our nation, hata kama maamuzi hayo yatapelekea kupoteza maisha ya baadhi ya wananchi wetu, na kwa maneno yako mwenyewe ni clear kwamba huwezi kushika nafasi kubwa ya uongozi kwa taifa, maana unaogopa kufa kwa wananchi, unaogopa kifo ndio maana maviongozi magoi goi wanatumia hiyo fear ya kukutisha kwamba kwa sababu kulitokesa vifo 27 miaka ya nyuma basi turudi kwenye chama kimoja, na wewe unaamini kwamba ni a good idea mpaka unaileta hapa JF, amuka mkuu!

Bado nasisitiza kuwa tuna tatizo la vurugu katika mfumo huu wa vyama vingi la kutatua na suluhisho ni kufyeka maslahi ya wanasiasa ili kuinua hali za maisha ya watanzania katika sekta nyingine. Vinginevyo ninakubali kutokukubaliana na wewe. Kwa vile hatukukubaliana siwezi kukulazimisha ukubali hoja ninazotoa na pia siwezi kukubali hoja yako kuwa watu waendelee kuuawa kisiasa kama unavyopendekeza. Kila mtanzania anahaki ya msingi ya kuishi na ni juu ya kila Mtanzania kutetea uhai. Kama unatetea mauaji mie sipo huko.

- Mkuu sitetei mauaji ila ninatetea kwa nguvu zangu zote the means necessary za kutufikisha taifa kwenye next level, kama vinahitajika some few vifo vya wananchi for the good of my nation, sijali kuwa mmojawapo wa hao watakaochaguliwa kutangulia kwenye haki, ninaiipinga hoja yako ya msingi, ya kurudia matapishi yetu ya utawala wa chama kimoja kwa sababu tu ya vifo 27, over wananchi Millioni 40, hiyo ninasema ni hoja hafifu sana na ni batili.

Respect.

FMEs!
 
Mkuu Watanzania,

Unajichanganya sana katika hoja yako, suala la mgawanyo wa keki halihusiani kabisa na mfumo wa siasa. Mnaweza kuwa katika mfumo wa chama kimoja na kusiwepo na usawa katika mgawanyo wa keki ya taifa hivyo watu kudidimia zaidi kwenye umasikini, na mnaweza kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi lakini wananchi wakaondoka kwenye umasikini.

Nani kakwambia kwamba wakati wa siasa za Chama kimoja hakukuwa na mauaji ya raia wasio hatia, uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa uliendana na ukandamizaji wa kupindukia pengine zaidi ya huo unaouzungumzia leo.

Suala la marupurupu ya viongozi ni tatizo linalotokana na viongozi tilionao kulelewa katika siasa zisizotaka mabadiliko, siasa za ubinafsi, zinazotumia kila hila kuhakikisha wanaendelea kutawala kulinda maslahi yao.

Cha msingi hapa ni kama walivyofanya Wakatoliki kutoa elimu kwa umma ili wafahamu mamlaka waliyonayo katika kuwaweka viongozi madarakani.

Vurugu za kisiasa zinazotokea Zanzibar kwa sasa na sehemu zingine wakati wa uchaguzi Tanzania bara zinatoa fundisho moja kubwa kuwa vyama vingi havijengi umoja wa kitaifa. Ingawa inaweza kuonekana kama wendawazimu lakini tukubali, tusikubali kuna umuhimu wa kurudisha mfumo wa chama kimoja ili kudumisha umoja wa Watanzania.

Kuna mlolongo wa matukio ya kutoweka kwa amani ambayo yametokea ndani ya vyama vingi. Matukio ya mauaji ya watu wasiopungua 27 huko Zanzibar wakati wa utawala wa Mkapa, uchomaji moto wa nyumba unaoendelea huko Zanzibar sambamba na uandikishaji wa wapiga kura ni mifano inayoonyesha kuwa mfumo wa vyama vingi hautufai Tanzania. Si hayo tu, kule Tarime wakati wa uchaguzi mdogo wa mbunge baada ya kifo cha Mh. Wangwe zilichochewa na kuwepo kwa mfumo wa chama kimoja. Si hayo tu, vurugu zilizotokea kule Kiteto pia wakati wa uchaguzi mdogo zinatufanya Watanzania tufikirie upya demokrasia ya vyama vingi ambayo tumenakili kutoka ulaya. Hata kura za maoni kuhusu kuanzisha vyama vingi zilionyesha asilimia 90% kutaka kuendelea na mfumo wa chama kimoja. Hili linaweza bishaniwa kuwa kura ya maoni haikuwa huru. Lakini haiondoi ukweli wa kutoweka kwa amani tunakoona sasa nchi kwetu.

Ingawa wengine wanaweza kusema kuwa mfumo wa vyama vingi unasaidia kumeza utengano wa aina nyingine kama ukabila, udini, ukanda n.k. lakini siasa za Tanzania zimesaidia sana kumomonyoa umoja wa Watanzania. Ukabila na udini unatumika kama mtaji wa kisiasa. Kwa maoni yangu mfumo wa chama kimoja utarejesha umoja unaotoweka kati yetu Watanzania.

Vinginevyo ili kokomesha vurugu za kisiasa yatupasa sasa kupanua wigo wa Mapambano nchini petu. Wana harakati, wafanyakazi wa sekta binafsi naya umma, wafanyabiashara na wakulima hatuna budi kuishinikiza serikali ipunguze mishahara na marupurupua ya wanasiasa ili Watanzania wasikimbilie kwenye siasa na hivyo kusababisha kutoweka amani katika nchi yetu. Kwa mfano kodi kwa wafanya biashara na wafanyakazi zinatakiwa ziwe za haki. Kama kipato katika sekta mbalimbali za maisha katika nchi yetu kitakuwa na usawa, vurugu za kisiasa hazitakuwepo kwa sababu kila mtu atachagua pa kufanya kazi na kipato hakita pishana. Madaktari watabaki mahospitalini, pia manesi na wafamasia, walimu wataendelea kufundisha shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Pia wakulima wataendelea na kilimo na hawatadanganyika kununuliwa Tshirt na kufia. Pia wafanya biashara watabaki kwenye biashara. Sheria inayosemwa na JK ya kutenganisha biashara na uongozi haitatatua vurugu za kisiasa mpaka sekta zote ziwe na uwiano sawa wa kipato cha fedha. Hiki ndicho kipaumbele kinachotakiwa kwenda sambamba na vita dhidi ya ufisadi, Watanzania tudai kwa nguvu nchini kote kupunguzwa kwa mishahara na marupurupu ya wanasiasa na kuongezwa katika sekta nyingine ili amani idumu Tanzania. Vinginevyo tukishindwa hili turudishe mfumo wa chama kimoja.
 
- Mkuu ninaongozwa na hoja humu JF, na hasa masilahi ya taifa hisia sio masialhi ya taifa na haipo hapa JF, nowhere! Kinachokushinda ni kujenga hoja on uhalisi wa vurugu za kisiasa Tanzania ambazo hazipo, unachozungumzia ni small scale isolated political ishus, ambazo ni based na ukabila na udini, ambalo sio tatizo la taifa letu in general, hii sio hisia ni a true political analysis inayojali facts on the ground, haiwezi kuwa hisia.

- Hoja yako ni kwamba kwa sababu wananchi 27, waliuliwa under Mkapa, some few years ago, basi turudishe utawala wa chama kimoja, ninasema hivi hii hoja ni mufilisi na ni empty!

- Mkuu JF, pamoja na kutoa ushauri mwingi wa kisiasa kwa watawala na vyama vyetu vya siasa, pia tunayarisha viongozi hapa mkuu, watu ambao wakipewa madaraka, hawatasita kutoa maamuzi magumu kwa ajili ya the best interest of our nation, hata kama maamuzi hayo yatapelekea kupoteza maisha ya baadhi ya wananchi wetu, na kwa maneno yako mwenyewe ni clear kwamba huwezi kushika nafasi kubwa ya uongozi kwa taifa, maana unaogopa kufa kwa wananchi, unaogopa kifo ndio maana maviongozi magoi goi wanatumia hiyo fear ya kukutisha kwamba kwa sababu kulitokesa vifo 27 miaka ya nyuma basi turudi kwenye chama kimoja, na wewe unaamini kwamba ni a good idea mpaka unaileta hapa JF, amuka mkuu!

- Mkuu sitetei mauaji ila ninatetea kwa nguvu zangu zote the means necessary za kutufikisha taifa kwenye next level, kama vinahitajika some few vifo vya wananchi for the good of my nation, sijali kuwa mmojawapo wa hao watakaochaguliwa kutangulia kwenye haki, ninaiipinga hoja yako ya msingi, ya kurudia matapishi yetu ya utawala wa chama kimoja kwa sababu tu ya vifo 27, over wananchi Millioni 40, hiyo ninasema ni hoja hafifu sana na ni batili.

Respect.

FMEs!

FMES Ninapenda kukufunda leo kuwa harakati zozote za maendeleo za kisasa lazima zijikite kwenye msingi mkuu wa haki za binadamu hasa hasa haki ya kuishi. Hata kama ungekuwa umeshuka kutoka mbinguni leo hii katu sitakubaliana na mawazo yako ya kiibilisi ya kushabikia kusiginwa kwa maisha ya mtu eti kwa sababu ya kutoka sadaka. Ninaweza kukubaliana na wewe kwa mambo mengine lakini siyo hili. Utu wa mtu ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu ambayo watu wote wenye akili timamu wanatakiwa kutetea. Eti kwa sababu ni watu 27 unashabikia, mbona tunatetea uhai wa watu wachache Albino. Msingi mkuu wa kutetea haki za binadamu lazima ujikite katika kutetea maisha siyo kushangilia mauaji kama wewe ulivyopendekeza awali. Ndiyo maana hadi leo tunalaani kitendo cha serikali ya JK kumfungulia haraka haraka marehemu Ukiwaona (Mungu ailaze roho yake peponi) eti kwa kuwa aliyeuawa alikuwa mmoja. Fumbuka FMES, hakuna uchache katika kutoa roho ya mtu. Kwa hiyo kiongozi yeyote wa nchi yetu lazima atetee uhai wa binadamu na kwa kigezo hiki wewe hufai kuwa kiongozi wa nchi. Hata vita dhidi ya ufisadi nyuma yake ni kutetea maisha ya watanzania ambayo yanapotea kwa sababu watu wachache wanakwapua mali za taifa.

FMES Watanzania lazima tuzibe ufa tusije tukajenga ukuta. Unasema vurugu zilizotokea Tarime, hata Kagera na Kiteto ilikuwa za kidini na kikabila? hapa umepotoka. Nasisitiza lazima maslahi ya wanasiasa yafyekwe na kuinuia maisha ya sekta zingine pia ili mbio kuelekea kwenye siasa zisiendelee kuchochea vurugu kwa kugombea maslahi.
 
- Mkuu kwa hiyo kama ninakuelewa this is your case kwa Tanzania kurudi kwenye utawala wa chama kimoja?

- Ninaona juhudi zako unajaribu kuzihamishia kwenye PR, badala ya ku-stick kwenye hoja yako ya msingi kwamba mauaji ya wananchi 27, under Mkapa yawe ndio sababu ya kurudi kwetu kwenye utawala wa chama kimoja, kwa nini unashindwa kujenga hoja on that? Badala yake unaakimbilia kwenye masilahi ya viongozi ambayo hayana anything to do na anything,

- Wananchi 27, walipouawa hakukuwa na marupu rupu ya kutisha kwa viongozi, na infact hata uongozi haukuwa wa kupiganiwa kama sasa, na kama ulivyoambiwa hapo juu ni kwamba hata chini ya utawala wa chama kimoja yamefanyika mauaji, tena mengi sana licha ya wananchi waliokufa kwenye kuhamishwa vijijini kuna waliokufa kule Shinyanga, mpaka kumpelekea waziri wa ndani Mwinyi kujiuzulu na wanazidi hao 27,

- Mfano wako wa Maalbino, napo pia ni nje ya mstari kwa sababu hao hawauliwi kwa sababu za kisiasa, au kwa sababu tuna vyama vingi vya siasa kwa hiyo tukurudi kwenye chama kimoja hawatauliwa tena, is that what you are saying?

- Hata hao tunaojaribu kuwaiga sana kimaendeleo huko ughaibuni, wamepitia mauaji mengi sana katika kupitisha agenda zao za kimaendeleo, kule US unajua ni wananchi wangapi wamekufa katika kupigania muungano wao, Nigeria wamekufa wananchi wangapi kulinda muungano, Europe wamekufa wananchi wangapi mpaka kufikia maendeleo waliyonayo sasa, hatuko hapa JF ku-promote mauaji, lakini kama yanahitajika kwa ajili ya maendeleo yetu hatuwezi kuwa na viongozi kama wewe ambao watakuwa ni waoga na kuanza kulilia kurudi Egypt, badala ya kumsikiliza Moses na kusonga mbele wavuke bahari,

- Mkuu ninarudia tena vifo vya wananchi wachache kwa ajili ya maendeleo ya taifa, ni sawa sawa sana na wala sio ukiukaji wa haki za binadam, hao mabingwa wa haki za binadamu duniani wanajua kwa sababu na wao wamepitia hiyo njia.

Respect.

FMEs!
 
Mkuu Watanzania,

Unajichanganya sana katika hoja yako, suala la mgawanyo wa keki halihusiani kabisa na mfumo wa siasa. Mnaweza kuwa katika mfumo wa chama kimoja na kusiwepo na usawa katika mgawanyo wa keki ya taifa hivyo watu kudidimia zaidi kwenye umasikini, na mnaweza kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi lakini wananchi wakaondoka kwenye umasikini.

Nani kakwambia kwamba wakati wa siasa za Chama kimoja hakukuwa na mauaji ya raia wasio hatia, uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa uliendana na ukandamizaji wa kupindukia pengine zaidi ya huo unaouzungumzia leo.

Suala la marupurupu ya viongozi ni tatizo linalotokana na viongozi tilionao kulelewa katika siasa zisizotaka mabadiliko, siasa za ubinafsi, zinazotumia kila hila kuhakikisha wanaendelea kutawala kulinda maslahi yao.

Cha msingi hapa ni kama walivyofanya Wakatoliki kutoa elimu kwa umma ili wafahamu mamlaka waliyonayo katika kuwaweka viongozi madarakani.

Ninakupa tano kwa hoja zako zenye akili NSESI. Lakini nasisitiza kuwa mwenendo wa sasa wa uonevu wa CCM unaelekezwa kwa vyama vya upinzani suluhisho lake ni pamoja na mgawanyo sawa wa keki ya Taifa. Uchache wa watu waliokufa katika vurugu za kisiasa hauhalalishi mauaji hata kama ni ya mtu mmoja. Umesema vema kuhusu siasa za ubinafsi na ndizo hizo zinazochochea vurugu. Kwa maoni yangu sijui kama wewe upo kwenye siasa utanisamehe, Watanzania tukifanikiwa kuiminya serikali yetu kupunguza maslahi ya wanasiasa wote kuanzia rais, mawaziri, wabunge na wenye vyeo vya kunyoshewa vidole tutakuwa tumetatua huu mwendelezo wa vurugu za kisiasa kukimbilia maslahi huku sekta zingine zikiwa hohehahe.

Kuhusu Waraka wa Wakatoriki ninakubaliana na wewe na harakati za akina Kigunge, na serikali ya CCM ili kukwamisha elimu ya uraia kusambaa nchi nzima lazima zikemewe kwa nguvu zote kama Pengo alivyosema. Kazi ya maaskofu ni ya Kimungu na kuwa ufisadi ambao mkuu wake ni ibilisi lazima upigwe vita makanisani, kwenye misikiti, kwenye matambiko, n.k. Kwa hivo wale wanaoupinga Waraka wa Katoliki ni mawakala wa ibilisi na siku zote Mungu atashinda. Hata pendekezo langu la Watanzania kuanzisha vita vipya vya kupunguzwa kwa maslahi ya wanasiasa sambamba na vita dhidi ya ufisadi ni sehemu ya kuchochea maendeleo ya nchi yetu, huku msingi mkuu ukiwa ni kulinda uhai wa kila Mtanzani. Awe mmoja, wawili au wachache Albino, watu 27 wote wana haki ya kuishi. Tusipoziba ufa tutajenga ukuta.
 
Wakati tukiendelea na mjadala, ni vema kukumbyuka kuwa ni asilimia 20 tu ya watanzania ndio walitaka kuwepo kwa vyama vingi. Nini kilitokea baada ya hapo naamini ni msingi mzuri sana wa kupima performance ya vyama vya siasa leo hii.
Anyway, hivi ushindi wa JK wa asilimia 80 dhidi ya 20 ya vyama vingine ilikua ni coincidence tu?
 
- Labda Mkuu Mpita Njia, tungeangalia pia ushindi wa Mkapa, ambao ulikuwa ni only 60%, sasa kwa hoja ya percentage ina maana gani?

- JF ni uwanja mkubwa sana, sasa tunaposhauri kurudi nyuma kitaifa ni lazima tuwe na hoja nzito, vurugu ndogo za majimbo matatu ya uchaguzi bado hata kama ni kweli hazihalalishi kurudi kwenye utawala wa chama kimoja, ambao mpaka leo wa-Tanzania tunahangaika kujitoa nao maana bado tuna grips zake kila kona ya maisha yetu ya kila siku kitaifa,

- Wanasiasa wengi wa sasa hawakimbilii huko kwenye siasa kwa sababu ya kutafuta marupu rupu, that is not true, Karamagi hakuenda kwenye siasa kutafuta marupu rupu, ukweli ni kwamba wanakwenda huko kutafuta kinga ya mali nyingi walizonazo ambazo hazina maelezo ya kutosha kuhusu uhalali wake,

- Look Mkapa aliacha kabisa kujihusisha na siasa, mpaka recently makelele yalipozidi kuhusu uhalali wa mali zake, ndio ameshituka kwamba akikaa nje ya siasa atarundikwa Segerea, sasa na yeye yupo tena kwenye siasa infull, ingawa at onetime tuliambiwa ameamua kupumzika na aachwe apumzike pia, ndio siasa zetu kutafuta kinga ya ufisadi kwa walio wengi, ingawa pia kuna percentage ndogo sana wanaokimbilia huko kutafuta mlo, usio halali.

- Serikali yetu haina marupu rupu ya uongozi wa kuwalipa wagombea ubunge hela nyingi sana wanazotumia kupata ubunge, ambao sio guarantee kwamba watapata uwaziri ili kurudisha hela zao, kwa hiyo wengi wa wanasiasa wetu ni crooks, wanaoenda huko kutafuta kinga tu za ufisadi wao!

Respect.

FMEs!
 
- Yaani huu ufa unaodai upo, ili kuzibwa ni lazima turudi kwenye utawala wa chama kimoja tu?

Respect.

FMEs!

FMES Mbona haueleweki? Mara unasema hakuna vurugu za kisiasa Tanzania, halafu unasema zilizopo ni kidogo tena ni za kidini na ukabila. Baadaye unakubali kuwa kuna ufa wa vurugu za kisiasa Tanzania. Hivi umesahau jinsi mrema na wafuasi wake walivyokuwa wanafanyiwa vitimbi na jeshi la polisi? Je pia umesahau hivi majuzi jinsi Kubenea alivyomwagiwa tindikali huku Tegambwage akitolewa ngeu? Umesahau pia jinsi ofisi ya Kubenea ilivyovamiwa na kubebwa tarakishi zake na watu waliosemakana eti ni usalama wa Taifa kumbe usalama wa wanasiasa wauvo na ubinafsi wao?. Kwako hii si kitu? Hivi ukimpoteza mpiganaji mmoja kama Kubenea kwako si kitu?
Lakini tatizo lako kubwa la msingi ambalo pia nimeliona kwa Lunyungu ni kuongozwa kwa hisia kuliko uhalisia ambao kwa maneno yako mwenyewe unavunja kanuni zinazoongoza majadiliano JF. Na mnatia aibu pale mnapojitapa kuwa wazoefu JF huku mnatanguliza na kusukumwa na mihemko ya hisia, hii inakera sana. Pia fikra zako FMES kuhusu maendeleo zimepinda sana na kupotoka kuhusu tunu na thamani ya pekee ya uhai wa binadamu awaye yeyote.
Majibu ya namna ya kuziba ufa wa vurugu za kidini utajaza wewe mwenyewe. Nimeyapanga hapa chini kulingana na umuhimu wake kama wewe na mimi tulivyoyapa uzito. Kanuni yangu ya msingi na mtambuka katika kuleta maendeleo ya nchi ni kulinda na kutunza uhai wa Watanzania, mmoja au wengi huku wewe ukisisitiza umuhimu wa kuua ili kufikia malengo ya maendeo katika mfumo wa vyama vingi.
Majibu ya Watanzania namna ya kuziba ufa wa vurugu za kisiasa Tanzania
1. Kupunguza marupurupu ya wanasiasa na kuinua kipato kwa watanzania walio wengi katika sekta zingine sambamba na vita dhidi ya ufisadi
2. Chama kimoja bila kutoa roho ya mtu yeyote
Majibu yako FMES ya namna ya kuziba ufa wa vurugu za kisiasa Tanzania
1. Hisia
2. Kuua watu ili kufikia malengo ya maendeleo katika mfumo wa vyama vingi
 
- Sasa hii ndio kesi yako ya taifa letu kurudi kwenye utawala wa chama kimoja?

Respect.

FMEs!
 
Back
Top Bottom