Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
Vurugu za kisiasa zinazotokea Zanzibar kwa sasa na sehemu zingine wakati wa uchaguzi Tanzania bara zinatoa fundisho moja kubwa kuwa vyama vingi havijengi umoja wa kitaifa. Ingawa inaweza kuonekana kama wendawazimu lakini tukubali, tusikubali kuna umuhimu wa kurudisha mfumo wa chama kimoja ili kudumisha umoja wa Watanzania.
Kuna mlolongo wa matukio ya kutoweka kwa amani ambayo yametokea ndani ya vyama vingi. Matukio ya mauaji ya watu wasiopungua 27 huko Zanzibar wakati wa utawala wa Mkapa, uchomaji moto wa nyumba unaoendelea huko Zanzibar sambamba na uandikishaji wa wapiga kura ni mifano inayoonyesha kuwa mfumo wa vyama vingi hautufai Tanzania. Si hayo tu, kule Tarime wakati wa uchaguzi mdogo wa mbunge baada ya kifo cha Mh. Wangwe zilichochewa na kuwepo kwa mfumo wa chama kimoja. Si hayo tu, vurugu zilizotokea kule Kiteto pia wakati wa uchaguzi mdogo zinatufanya Watanzania tufikirie upya demokrasia ya vyama vingi ambayo tumenakili kutoka ulaya. Hata kura za maoni kuhusu kuanzisha vyama vingi zilionyesha asilimia 90% kutaka kuendelea na mfumo wa chama kimoja. Hili linaweza bishaniwa kuwa kura ya maoni haikuwa huru. Lakini haiondoi ukweli wa kutoweka kwa amani tunakoona sasa nchi kwetu.
Ingawa wengine wanaweza kusema kuwa mfumo wa vyama vingi unasaidia kumeza utengano wa aina nyingine kama ukabila, udini, ukanda n.k. lakini siasa za Tanzania zimesaidia sana kumomonyoa umoja wa Watanzania. Ukabila na udini unatumika kama mtaji wa kisiasa. Kwa maoni yangu mfumo wa chama kimoja utarejesha umoja unaotoweka kati yetu Watanzania.
Vinginevyo ili kokomesha vurugu za kisiasa yatupasa sasa kupanua wigo wa Mapambano nchini petu. Wana harakati, wafanyakazi wa sekta binafsi naya umma, wafanyabiashara na wakulima hatuna budi kuishinikiza serikali ipunguze mishahara na marupurupua ya wanasiasa ili Watanzania wasikimbilie kwenye siasa na hivyo kusababisha kutoweka amani katika nchi yetu. Kwa mfano kodi kwa wafanya biashara na wafanyakazi zinatakiwa ziwe za haki. Kama kipato katika sekta mbalimbali za maisha katika nchi yetu kitakuwa na usawa, vurugu za kisiasa hazitakuwepo kwa sababu kila mtu atachagua pa kufanya kazi na kipato hakita pishana. Madaktari watabaki mahospitalini, pia manesi na wafamasia, walimu wataendelea kufundisha shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Pia wakulima wataendelea na kilimo na hawatadanganyika kununuliwa Tshirt na kufia. Pia wafanya biashara watabaki kwenye biashara. Sheria inayosemwa na JK ya kutenganisha biashara na uongozi haitatatua vurugu za kisiasa mpaka sekta zote ziwe na uwiano sawa wa kipato cha fedha. Hiki ndicho kipaumbele kinachotakiwa kwenda sambamba na vita dhidi ya ufisadi, Watanzania tudai kwa nguvu nchini kote kupunguzwa kwa mishahara na marupurupu ya wanasiasa na kuongezwa katika sekta nyingine ili amani idumu Tanzania. Vinginevyo tukishindwa hili turudishe mfumo wa chama kimoja.