Vurugu, ufisadi, umafia katika kampeni za CCM: Kweli huu ni mfano wa kuigwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vurugu, ufisadi, umafia katika kampeni za CCM: Kweli huu ni mfano wa kuigwa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Jul 23, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Wana-JF wenzangu, nisaidieni, maana nimechanganyikiwa. Hivi karibuni vyombo vya habari, hususan magazeti, vimekuwa vikiripoti vituko, vurugu, umafia na ufisadi katika kampeni za uchaguzi za CCM zilizoanzia katika uchukuaji fomu za kugombea.

  Aidha mara kwa mara tumekuwa tunasikia akina Makamba, Msekwa, Dr Shein, Pinda na viongozi/makada wengine wakuu wa chama hicho wakisema kwa kuwa CCM ni nambari wani, basi CCM ni chama bora kinachopaswa kuigwa na vyama vya wapinzani katika kufanya kampeni za kistaarabu – zisizokuwa na vurugu.

  Swali langu: Mbona mawili haya hayaendani? Kweli vyama vya upinzani vinapaswa kuiga mfano wa CCM, au CCM wana maana gani hasa wanaposema wao ni mfano bora wa kuigwa? Malaria Sugu, labda tuanze na wewe – ni kweli chama chako ni mfano mzuri wa kuigwa?

  Jibu nisilolitarajia ni kwamba vurugu, umafia na ufisadi wote huu ni ukomavu wa siasa/demokrasia. Siamini iwapo yuko kiongozi wa CCM anaweza kutamka hivyo hadharani.
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hii ni uthibitisho kwamba uongozi ngazi zooote ndani ya CCM ni ufisadi in making.
  Pia watanzania hatuhitashi mshauri mwelekezi kutuelezea kuwa CCM haifai kwa kuwa imejaa majambazi wa kura na mafisadi wenye uchu kuliko fisi.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Zak -- hujachanganyikiwa, ila CCM ndiyo imechanganyikiwa. Kuna tofauti kubwa kati ya yale wasemayo majukwaani na watendayo. Na hali hii itaendelea tu hadi hapo watakapoishiwa kabisa na kutokomea kunakowafaa -- kama jinsi historia inavyotukumbusha siku zote.

  Angalia usanii wa serikali yake: Ime-unleash TAKUKURU kuingilia katika ufisadi ndani ya kampeni zake -- na wametangaza wamewanasa kadha. Lakini naamini kabisa hapo ndipo mwisho, hakuna hatua zozote za mahakama zitazochukuliwa. Mwisho wa yote wahusika watafutiwa mashitaka -- mfano mzuri ni wale wabunge wawili mkoani Arusha walivyokamatwa wakitembeza fedha katika mchakato wa kugombea nafasi katika CCM-NEC mwaka 2007.

  Kwa ufupi CCM SI MFANO MZURI WA KUIGA KATIKA KAMPENI.
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hii ni uthibitisho kwamba uongozi ngazi zooote ndani ya CCM ni ufisadi in making.
  Pia watanzania hatuhitashi mshauri mwelekezi kutuelezea kuwa CCM haifai kwa kuwa imejaa majambazi wa kura na mafisadi wenye uchu kuliko fisi.
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ukipata mchango kutoka kwa MS utakuwa na bahati, huyu yeye ni bingwa wa kutundika threads za "ajabu ajabu" na kutokomea, sijawahi kumuona akichangia hoja hapa jamvini.
   
Loading...