Vurugu St. Mathew's Sekondari

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
2,064
2,301
Mwishoni mwa wiki iliyopita kulitokea vurugu kubwa shule ya Sekondari St. Mathew's kule Kongowe. shule hii inamilikiwa na bwana Mtembei. Sababu ya vurugu hizi ni vijana waliomaliza kidato cha sita waliokuwa wanadai fedha zao za "caution money".

Kiasi cha shilingi 30,000 kila mmoja. Walipoufuata uongozi wa shule (na hatimae mwenye shule) wakanyimwa fedha hizo. Vurugu hizo zilisababisha Polisi kupelekwa pale shuleni na mpaka leo wako pale. Pia masomo ya shule nzima yamesimama kwa maelezo kuwa walimu walichomewa vifaa, vitabu na madaftari yao ya kufundishia.

Baadhi ya wanafunzi wamechukuliwa na wazazi wao kwa kuwa hakuna maji na chakula kinachelewa kupikwa.
Cha, ajabu, sikuona chombo chochote cha habari kikiripoti habari hiyo. Habari leo waliripoti Jumatano ukurasa wa tatu. Najiuliza, ilikuwaje vyombo vingine vya habari visiripoti habari hiyo?

Suala la kurudishiwa "caution money" kwa mwanafunzi aliyemaliza shule ni haki yake ili mradi tu awe hakufanya uharibifu wowote wa vifaa vya shule kabla. Vipi hawa wanyimwe mpaka kutokee mzozo uliosababisha vurugu?
Labda kuna mwenye habari zaidi na majibu mwafaka.
 
Skuli nzuri wanaitia doa, makubaliano ni nini kama hiyo caution money ni refundable basi wanatakiwa warudishiwe kama siyo (non-refundable) basi, waangalie kwanza kwani kudai ndo mpaka vurugu? waache ushamba
 
Mutembei yupi; toa jina kamili kama umeamua kutaja majina bwana kutuepushia ma_uncles usumbufu!
 
cha kusikitisha ni kwamba wazazi na walezi ndio wanatoa hela lakini watoto wanapigania hiyo pesa!! mob psychology inaharibu sana watoto

kwani zililipwa kwa vurugu? there could be a better way to claim the money
 
caution money huwa hazirudishwi hata siku moja hapa kwetu Tanzania.Sijui huwa zinapelekwa wapi?
 
Hivi mnajua bora mmenikumbusha nami nenda dai yangu japo ni miaka lukuki- by that tme sie tulikuwa tunalipa tu bila hata ya kupewa maelezo zaidi ya pesa ya kinga shilingi 5,000/= Laiti ningekuwa nimeiona ile 'refundable'
 
Kama walifanya uharibifu hapo ni "bila-bila" - caution Money imepata matumizi - sidhani kama kuna kudai tena!
 
Back
Top Bottom