Vurugu: Mkutano wa Mbowe wavamiwa Hai, Green Guard na OCD wahusishwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
104,121
183,966
Lengo kuu ni Chadema ijibu mapigo ili wapate kisingizio cha kuzuia Mikutano ya Mbowe inayoendelea .

======
1583298958488.png
Hai. Mkutano wa Mbunge wa Hai (Chadema) mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe uliokuwa ukifanyika katika kijiji cha Kikafu Chini, Kata ya Weruweru umevurugwa baada ya kuibuka kikundi cha vijana zaidi ya 50 wa kike na kiume kwenye mkutano huo na kuanzisha vurugu.

Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho alipanda jukwaani leo Jumanne Machi 3, 2020 saa 11:12 jioni ambapo alizungumza hadi saa 11:47 jioni ndipo kundi la vijana lilipoibuka na kuanza kupiga kelele, jambo lililomfanya mbunge huyo kunyamaza.

Hata hivyo kabla ya kunyamaza, Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema polisi hili ndilo kundi ambalo tuliwaambia na baada ya kauli hiyo alinyamaza akiangalia vurugu hizo.

Vijana hao wanaodaiwa kutoka maeneo mbalimbali walianza kupiga kelele wakisema "sema ulichofanya, tunataka Magufuli” hali ambayo iliwafanya polisi kuingilia kati kuanza kutuliza vurugu hizo.

Baada vurugu kuendelea, polisi ambao walikuwa na gari moja waliongeza nguvu kwa kuja polisi waliokuwa wamevalia sare na kudhibiti kikundi hicho kusogelea jukwaa alilokuwa amesimama Mbowe.

Alivyonyamaza zaidi ya dakika 20 akiwatizama pasina kuongea chochote polisi nao walisimama ili wasiende kwenye jukwaa alilokuwa Mbowe wananchi walikuwa wakipa kelele. Baadaye waliondoka pasina kukamatwa.

Walipoondoka vijana hao, Mbowe alishuka jukwaani na kupanda gari lake kisha kuondoka.

Awali, kabla ya Mbowe kupanda jukwaani, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Hai, Saimon Mnyampanda alidai kuna vijana zaidi ya 70 wa kike na kiume wametumwa katika mkutano huo ili kufanya vurugu.

"Polisi kama ninyi hamtambui, sisi tunatambua, wapo vijana hapa wametumwa kutoka Kiungi, Bomang'ombe na wengine wa hapa, kufanya vurugu, tunatambua hilo," alisema Mnyampanda.

Mwananchi linaendelea kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro (RPC), Salum Hamuduni kuzungumzia vurugu hizo.

Zaidi, soma: Hai: Mbowe azungumzia tukio la kundi la Vijana waliovamia mkutano wake

https://www.jamiiforums.com/threads/ushahidi-uvccm-ndio-waliofanya-vurugu-kwenye-mkutano-wa-mbowe-jimboni-hai.1697857/Jimboni
 
The coolest jw

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
632
1,021
Mkuu wa wilaya ya hai ni mjinga sana siasa ni ustahimilivu na uvumilivu unakubali kushindwa kwa hoja na wala si uwadui kama jiwe anavyofikilia kuwa kuanzisha vurugu kwenye mikutano ya vyama vya wapinzani ndio atapendwa hapo anajidaganya kwanza ndio kama anaongeza petroli kwenye moto
 
Cliffhanger

JF-Expert Member
May 22, 2018
721
1,288

Kosa kubwa lililofanywa ni kumpa mtu mamlaka makubwa bila "background check" matokeo yake tunaongozwa na wahamiaji haramu ambao wanatuharibia nchi yetu!
 
Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,475
6,666
Mbowe analipia dhambi ya usaliti kwa makosa aliyofanya 2015 baada ya kubadili gia angani,hakuna atakayemuonea huruma ,kwani alimpokea Lowassa pesa akala yeye na wafuasi wake wachache
Thibitisha kwa ushahidi usiotia Shaka haya madai yako! Nani alipewa shilingi ngapi na zilikuwa cash au cheque? Huu ujinga wako wa kuipokea taarifa Tena ya kupikwa bila kuwa na uthibitisho na kuifanya habari ipo siku itakuharibia! Ni ushauri tu wa kujifunza kutokushabikia taarifa usizokuwa na ushahidi nazo kwani teknolojia haijui kuongopa!
 
mwakijembe

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
1,640
2,293
Mkuu wa wilaya ya hai ni mjinga sana siasa ni ustahimilivu na uvumilivu unakubali kushindwa kwa hoja na wala si uwadui kama jiwe anavyofikilia kuwa kuanzisha vurugu kwenye mikutano ya vyama vya wapinzani ndio atapendwa hapo anajidaganya kwanza ndio kama anaongeza petroli kwenye moto

Hiyo mbinu wanayotumia ccm ilikuwa ikitumiwa na kina Mussolini kwenye mikutano ya washindani wao, lengo ni kutisha watu kuhudhuria mikutano ya wapinzani, kisha ccm wakifanya inakuwa salama na inatumika propaganda ya kijinga kuwa ccm inakubalika, na wananchi wamewapuuza wapinzani ndio maana hawaendi kuwasikiliza. Ila ni mbinu ya kizamani kweli kweli maana wananchi sasa hivi wanaufahamu wa kutosha.
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
8,256
12,920

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,475
6,666
Hivi kwa mfano vijana wapumbavu wa green guard wawili watatu wangeuwawa hapo lawama ingeenda kwa Mbowe? Huo ni upumbaf mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ni mpango unaosukwa kutoka Whitehouse ya kumsuffocate Mbowe kwa namna yoyote ili aswekwe rumande Hadi uchaguzi uishe! Haiwezekani mikutano yao waifanye bila vurugu lakini linapokuja suala la chama kingine kufanya mikutano wao wanachefukwa kana kwamba wao ni Bora na special kuliko wengine! Ccm jichungeni Sana kwani mipango ya kuwatoa wajeda makambini kwenda kufanya vurugu upo wazi na wanajulikana kwa majina! Acheni Sasa siasa za kitoto watanzania wamestaarabika siyo wajinga Tena!
 
8 Reactions
Reply
Top Bottom