Elections 2010 Vurugu hizi za wapigakura zinadai mabadilio ya muundo wa NEC...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Wapigakura wanaghadhabu nchi nzima na hawaafiki na kile kinachoendelea na hususani sehemu ambazo CCM imefanya vibaya matokeo kucheleweshwa kusomwa au kugeuzwa ili kuibeba CCM............

Haya ni matunda ya JK na serikali yake ya CCM kuendesha nchi kibabe na kukataa mabadilko ya muundo wa NEC na hivyo kubaki na NEC kama ilivyokuwa kwenye serikali ya chama kimoja.......

Leo gazeti la Majira limebainisha ya kuwa waangalizi wa kimataifa wameonyesha kukerwa ya kuwa inakuaje miaka takribani 15 tangia mfumo wa demokrasia ya vyama vingi urudishwe bado serikali ya CCM inang'ang'ania NEC inayoteuliwa na Raisi mgombeaji na kusaidiwa na watumishi wa serikali za mitaa ambao nao hawawajibiki kwa NEC ila kwa serikali ya CCM kupitia mawaziri wanaogombea.............mgongano wa masilahi hapa upo wazi kabisa........

Hivyo chaguzi hii siyo ya huru wala ya haki....................wapigakura nao siyo wajinga wakati wanaona mgombea wasiyemtaka pale anapopita na kuwa kiongozi wao wanapata ghadhabu kubwa na ndiyo maana kuna hizi rabsha rabsha za kupinga mfumo mzima wa uchaguzi......

Hivyo, kama tunataka chaguzi za 2015 kuwa za amani ni lazima NEC iwe huru na haki na iteuliwe kwa mfumo huu hapa chini:

a) Wawepo wajumbe tisa wa NEC na wachaguliwe kwa utaratibu wa kutoka kwenye maeneo haya:-

i) Chama cha Majaji na Mahakimu ziteue wajumbe wawili kwa kura za wajumbe wake ambazo ni za wazi kwa hakimu mmoja na jaji mmoja. Lazima nafasi moja iende kwa jinsia tofauti ili mwanaumme na mwanamke wapatikane.....

ii) Chama cha wanasheria nchini cha bara na Zanzibar kila kimoja kiteue mjumbe mmoja mmoja na hivyo kuwa na wajumbe wawili. Lazima nafasi moja iende kwa jinsia tofauti ili mwanaumme na mwanamke wapatikane.....

iii) Vyama visivyokuwa vya kiserikali yaani NGOs zote ziteue wajumbe wawili tu kwenye tume hiyo. Lazima nafasi moja iende kwa jinsia tofauti ili mwanaumme na mwanamke wapatikane.....

iv) Vyama vya siasa viteuwe nafasi tatu kulingana na idadi ya kura za uchaguzi wa wabunge zikijumlishwa na zile za Uraisi na hivyo nafasi hizi kupatikana kwa asilimia za majumuisho hayo.

v) Mwenyekiti wa NEC kuchaguliwa na wajumbe hao tisa badala ya kuteuliwa na Raisi.Tume hii ni lazima ithibitishwe na bunge na ajira yake hatma yake kuwa bungeni tu na wala siyo kwa watendaji serikalini

vi) Tume kuajili makamisaa wa majimbo wa kudumu ambao watawajibika moja kwa moja kwao badala ya utaratibu uliopo wa kuazimwa kutoka serikali za mitaa..ambako mgongano wa kimasilahi umejitokeza.......

vii) Tume iwe inatoa ajira za muda mfupi za wasimamizi wa vituo vyote vipato 52, 000 na kuondoa hisia za waalimu kununuliwa na serikali iliyopo madarakani kwa peremende za kuongezwa mishahara nyakati za uchaguzi........

viii) Tume ya uchaguzi iwe inatenga bajeti za kuwalipa mawakala wote wa vyama vya siasa ili kuondoa hisia ya kuwa vyama vya upinzani mawakala wake hurubuniwa na chama tawala kutokana na ukata walionao.....
Wajumbe wa NEC waruhusiwe vipindi viwili vya miaka mitano mitano tu na baada ya hapo wajumbe wengine wateuliwe.............
Haya ni mazingira ya uchaguzi wa huru na wa haki na damu kamwe haiwezi kumwagika.......
 
mmh imekaa vizuri lakini utekelezaji wake sijui kwa mafisadi tulio nao?
 
AMEN....ndiyo hali halisi...
Ushauri wako umetulia na hili ni muhimu sana.
UKWELI UTABAKI DAIMA, ILA UONGO NA WAONGO WATAANGAMIA...
MUNGU IBARIKI TANZANIA...NA WATU WAKE WANAOPORWA HAKI.
 
wapigakura wanaghadhabu nchi nzima na hawaafiki na kile kinachoendelea na hususani sehemu ambazo ccm imefanya vibaya matokeo kucheleweshwa kusomwa au kugeuzwa ili kuibeba ccm............

Haya ni matunda ya jk na serikali yake ya ccm kuendesha nchi kibabe na kukataa mabadilko ya muundo wa nec na hivyo kubaki na nec kama ilivyokuwa kwenye serikali ya chama kimoja.......

Leo gazeti la majira limebainisha ya kuwa waangalizi wa kimataifa wameonyesha kukerwa ya kuwa inakuaje miaka takribani 15 tangia mfumo wa demokrasia ya vyama vingi urudishwe bado serikali ya ccm inang'ang'ania nec inayoteuliwa na raisi mgombeaji na kusaidiwa na watumishi wa serikali za mitaa ambao nao hawawajibiki kwa nec ila kwa serikali ya ccm kupitia mawaziri wanaogombea.............mgongano wa masilahi hapa upo wazi kabisa........

Hivyo chaguzi hii siyo ya huru wala ya haki....................wapigakura nao siyo wajinga wakati wanaona mgombea wasiyemtaka pale anapopita na kuwa kiongozi wao wanapata ghadhabu kubwa na ndiyo maana kuna hizi rabsha rabsha za kupinga mfumo mzima wa uchaguzi......

Hivyo, kama tunataka chaguzi za 2015 kuwa za amani ni lazima nec iwe huru na haki na iteuliwe kwa mfumo huu hapa chini:

A) wawepo wajumbe tisa wa nec na wachaguliwe kwa utaratibu wa kutoka kwenye maeneo haya:-

i) chama cha majaji na mahakimu ziteue wajumbe wawili kwa kura za wajumbe wake ambazo ni za wazi kwa hakimu mmoja na jaji mmoja. Lazima nafasi moja iende kwa jinsia tofauti ili mwanaumme na mwanamke wapatikane.....

Ii) chama cha wanasheria nchini cha bara na zanzibar kila kimoja kiteue mjumbe mmoja mmoja na hivyo kuwa na wajumbe wawili. Lazima nafasi moja iende kwa jinsia tofauti ili mwanaumme na mwanamke wapatikane.....

Iii) vyama visivyokuwa vya kiserikali yaani ngos zote ziteue wajumbe wawili tu kwenye tume hiyo. Lazima nafasi moja iende kwa jinsia tofauti ili mwanaumme na mwanamke wapatikane.....

Iv) vyama vya siasa viteuwe nafasi tatu kulingana na idadi ya kura za uchaguzi wa wabunge zikijumlishwa na zile za uraisi na hivyo nafasi hizi kupatikana kwa asilimia za majumuisho hayo.

V) mwenyekiti wa nec kuchaguliwa na wajumbe hao tisa badala ya kuteuliwa na raisi.tume hii ni lazima ithibitishwe na bunge na ajira yake hatma yake kuwa bungeni tu na wala siyo kwa watendaji serikalini

vi) tume kuajili makamisaa wa majimbo wa kudumu ambao watawajibika moja kwa moja kwao badala ya utaratibu uliopo wa kuazimwa kutoka serikali za mitaa..ambako mgongano wa kimasilahi umejitokeza.......

Vii) tume iwe inatoa ajira za muda mfupi za wasimamizi wa vituo vyote vipato 52, 000 na kuondoa hisia za waalimu kununuliwa na serikali iliyopo madarakani kwa peremende za kuongezwa mishahara nyakati za uchaguzi........

Viii) tume ya uchaguzi iwe inatenga bajeti za kuwalipa mawakala wote wa vyama vya siasa ili kuondoa hisia ya kuwa vyama vya upinzani mawakala wake hurubuniwa na chama tawala kutokana na ukata walionao.....
Wajumbe wa nec waruhusiwe vipindi viwili vya miaka mitano mitano tu na baada ya hapo wajumbe wengine wateuliwe.............
Haya ni mazingira ya uchaguzi wa huru na wa haki na damu kamwe haiwezi kumwagika.......

dr slaa natakiwa kuanzai hapo awahamasishe watanzania kudai katiba mpya itakayozaa tume huru ya uchaguzi. Na sisi wapenda mabadiliko tunatakiwa kutimiza wajibu wetu wa kudai katiba mopya kwa kuhamasishana kushiriki kwa wingi katika mandamano ya kudai katiba mpya. Ili kuwafanya watanzania wengi zaidi washiriki katika harakati za kudai katiba mpya dr slaa anatakiwa kutoa elimu ya uraia nchi nzima kwa kufany linkage between mapangufu ya katiba yeti na kushamiri kwa ufisadi, umaskini n.k.

Katika mikutano ya kampeni hilo alijitahidi kulifanya lakini kwa kuwa kampeni zilikuwa time bound hakuweza kulifany kwa ufanisi mkubwa
.
 
Back
Top Bottom