Vurugu hizi ni Mavuno ya U-dini ktk siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vurugu hizi ni Mavuno ya U-dini ktk siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Oct 15, 2012.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kampeni za uchaguzi wa 2010 zilipoanza kwenda kombo kwa upande, CCM waliona ni bora kuwagawa wapiga kura kwa kutumia DINI. Kikwete akaanza kupewa sifa ya Uislamu safi na misikiti ikatumika. CHADEMA kikawa ni chama cha wakristu na baadhi ya makanisa yakatumika!

  Pale Arusha Makamba akaweka nguvu kumusaidia Batilda kwa kuingiza kampeni Msikitini.

  Njama zote hizo ziliitwa eti ni mbinu za kisiasa. Leo hii ni miaka miwili. Mimi muislamu niliyeitikia wito wa kumpa kura muislmu mwenzetu, na akapata kura za kutosha kumuweka ikulu leo hii najisikia mzito na mshindi.

  Ndo haya yanayotokea leo hii. Wanaoitwa waislamu wanaona aliyeko ikulu ni yule mshindi wao. Tena kwa upendeleo kabisa kila wakati mkuu wa mkopa wa Dar lazima awe Muislamu mwenzetu na kuiamlisha vurugu mkoani Dar kuliko mikoa mingine. Dar ni yetu.

  Sasa tujiweke tayari ktk safari hii. Ni kama kule Kenya baada ya wanasiasa kufaidi mahangaiko yalihamia kwa wananchi wa kawaida. Matatizo haya hayataweza kutatuliwa na maelezo laini kama hayo ya Rais kwamba eti muwe watulivu. Nani atulie? wataombwa mara ngapi kuwa watulivu?

  Mukifika eneo la tukio wote ni maombi ya utulivu hata hao Polisi wenye vitu vya ncha kali. Bahati mbaya uongozi mzima ni wa waislamu wakiwatuliza wakristu. Rais, IGP, RC na Kova wetu wote waislamu. Kweli inawatoka rohoni kuwaambia wakristu watulie?
  Hali tunayoiona ni matokeo ya uzembe wa kumnadi mtu dhaifu kwa kumpa sifa kubwa ya U-dini.
   
Loading...