Vurugu Embaseni: Rose Chatanda ashambuliwa na wafuasi wa CHADEMA

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Sauti ya Msimamizi wa Uchaguzi inaonekana kuwa CCM wanaleta vurugu katika eneo la Embaseni baada kuona vijana wa CDM wapo ngangari kulinda kura... Imelazimu polisi kuingilia kati.

Alikuja mama ambae alieleza kuwa anakuja kumlipa wakala wa SAU, lakini akaelezwa kuwa hapo kituo cha Uchaguzi hakukuwa na wakala huyo..akatakiwa kuondoka. Jioni hii akaja tena akiwa na Vijana wa Kimasai kwenye gari,akamwita msimamizi wa CCM pembeni na kuongea nae kwa muda. Msimamizi wa Uchaguzi akamtaka aondoke, mara vijana aliokuwa nao kwenye gari wakaanza kuwarushia mawe wenzao wa CDM ambao walikuwa mita mia zaidi toka eneo la kupiga kura..ndipo vurugu za kufa mtu zikaibuka, vijana wale wakakimbia na gari wakamwancha yule mama ambae baadae aliwekwa chini ya ulinzi na polisi..Vijana wa CDM wakamdhibiti vurugu zikaendelea mpaka imelazimika Msimamizi wa Uchaguzi wa Kituo kutoa taarifa kwa OCD kwa msaada.

Kwa mujibu wa ITV (Sauti ya Renatus Mtabuzi)

Ngilisho Sunrise Radio anaripoti:
Kituo Embasema kata Kikatiti:

Hali ni tete kabisa, gari lilokuwa na katibu mkuu wa ccm mkoa wa arusha Rosemery Chatanda lashambuliwa na wafuasi wa cdm gari hilo lilikuwa linalazimisha kuingia ndani ya kituo hicho.
 
Mwaka huu CCM kazi wanayo. Hata hapo nguvu ya UMMA imewashinda, maana walikuwa wanataka kuwatimua vijana walio mita mia mbili mwisho wake wakatimuliwa wao. Achana na Nguvu ya Umma wewe
 
Ccm maji shingo,wameanza vurugu,inaonekana huyo mwenyekiti wa ccm ameripoti kwa magamba wenzio kuwa hawajapata kura yoyote hapo na hivyo waingize feki.
 
Leo tumewabana kila kona. Hata tunguri za Profesa Maji Marefu zimeshindwa kufanya kazi mbele ya kauli mbiu ya CDM 'Tulianza na Mungu, tunamaliza na Mungu'
 
BREAK NWS VIJANA WA CCM WAFANYA VURUGU KITUO CHA EMBASENI VIJANA WA CDM WAWADHIBITI VIKALI SANA

Hayo yametokea katika kituo cha embasseni,ambapo vijana hao Wa CCM walikuwa kwenye gari walipofika tu,wakaanza kuwarushia mawe vijana makini wa CDM wanaolinda kura kituo hicho,vijana hao walikuwa wapo na dada mmoja ambaye alikuwa anataka kuingiza kitu kupitia mmoja wa wasimamizi wa kituo,lakini vijana wa CDM waliwadhibiti vikali mpaka ffu walipofika eneo hilo
 
BREAK NWS VIJANA WA CCM WAFANYA VURUGU KITUO CHA EMBASENI VIJANA WA CDM WAWADHIBITI VIKALI SANA

Hayo yametokea katika kituo cha embasseni,ambapo vijana hao Wa CCM walikuwa kwenye gari walipofika tu,wakaanza kuwarushia mawe vijana makini wa CDM wanaolinda kura kituo hicho,vijana hao walikuwa wapo na dada mmoja ambaye alikuwa anataka kuingiza kitu kupitia mmoja wa wasimamizi wa kituo,lakini vijana wa CDM waliwadhibiti vikali mpaka ffu walipofika eneo hilo

Tunataka kujuwa Huyo dada aliyetaka kupenyeza kura ni nani?
 
Yaani tena hadi Masaku akaamua kupotezea..jamaa alikuwa na stori ya CCM na mikakati ya kuhonga mawakala ili waweke kura za maruhani. Msimamizi mkuu wa kituo akawa ngangari na vijana wa CDM wakawa macho.
CCM bila wizi wa kura haiwezekani!!
 
Ccm
maji shingo,wameanza vurugu,inaonekana huyo mwenyekiti wa ccm ameripoti
kwa magamba wenzio kuwa hawajapata kura yoyote hapo na hivyo waingize
feki.

hizo ni hisia zako tu. atajuaje na hazijaanza kuhesabiwa? au kila anayepiga anatangza kura yake?
 
Back
Top Bottom