VURUGU ARUSHA-Waandishi wa Habari Arusha watoa siku 7 kwa Polisi kuomba radhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VURUGU ARUSHA-Waandishi wa Habari Arusha watoa siku 7 kwa Polisi kuomba radhi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mathias Byabato, Jan 6, 2011.

 1. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Tumetumiwa kwenye email zetu  Ndugu Waandishi wa Habari

  CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), kinalaani,kwa
  nguvu zake zote, matukio ya askari polisi mkoani Arusha kuendeleza
  tabia ya kuwazuia na kuwapiga, waandishi wa habari wakati
  wakitekeleza majukumu yao halali.

  Mfano wa hivi karibuni ni tukio la Januari 5 mwaka huu, ambapo
  waanidishi wa habari habari mkoani Arusha wakiwa katika majukumu yao
  halali ya kufuatilia maandamano na mkutano wa Chama cha Demokrasia na
  Maendeleo(CHADEMA), walikumbana na kipigo kutoka kwa Polisi waliokuwa
  wakijaribu kuzuia vurugu zilizotokea.

  Pamoja na waandishi kujaribu kujitambulisha kwa kuonyesha vitambulisho
  halali,hakuna askari aliyejaribu kuwasikiliza na matokeo yake
  walikumbana na kipigo na wengine kuwekwa ndani kama vile ni wahalifu

  Hatua ya waandishi kufuatilia tukio hilo ilikuwa katika kutimiza
  majukumu yao ya msingi kabisa ya kuwahabatisha wananchi wnegine
  nchini ambao kwa namna moja au nyinbgine wasingeweza kufika au kuwa
  Arusha kwa wakati huo.

  Huo ni wajibu wa kwanza unaotambulika kikatiba na kila chombo
  kinapaswa kuuheshimu kama kweli nchi yetu inataka kujenga demokrasia
  ya kweli katika mfumo wa siasa uliopo nchini.


  Hata hivyo katika hali ambayo APC haikubaliani nayo askari polisi
  waliokuwa katika kulinda amani ikiwa ni pamoja na kuzuia maandamano
  hayo yasifanyike walianza kuwatisha waandishi wa habari wakiwa nje ya
  Hoteli ya Mount Meru. Hali ambayo ilionyesha kana kwamba waandishi wa
  habari nao walikuwa sehemu ya wanachama wa CHADEMA kitendo ambacho si
  kweli.

  Pamoja na maandamano hayo kufanyika kwa takribani kilomita mbili hivi
  waandishi wa habari waliendelea kupiga picha na kukusanya taarifa zao
  ikiwa ni pamoja na kufuatilia kwa karibu nyendo zote za maandamano
  hayo. Lakini katika mazingira ya yaliyoleta utata pamoja na kwamba
  askari polisi walikuwa wakiowana waandishi wa habari mbele ya
  maandamano wakiwa na zana zao za kazi.

  Pamoja na hali hiyo bado askari polisi walidiriki kuanza kuwapiga
  waandishi wa habari huku wakiwatishia kuwanyang’anya kamera na vitabu
  vyao. Hata hivyo hali bado iliendelea kujitokeza kwa waandishi wa
  habari waliokuwa wakisubiria mkutano wa viongozi wa CHADEMA ktaika
  hoteli moja, ambapo bado askari polisi waliwakamata kwa tuhuma za
  kupiga picha wakati Dk. Slaa akiwa anakamatwa.

  Waandishi hao walikamatwa na kufikishwa kituoni na kamera zao
  kuchukuliwa kisha kufutwa picha zote zilizokuwa zimepigwa,

  MSIMAMO WA APC

  Kutoka na mazingira hayo Chama cha Waandishi wa habari mkoani wa
  Arusha kinatambua na kuheshimu kwamba jeshi la polisi ni moja ya
  vyanzo vikubwa vya upatikanaji kwa taarifa kwa waandishi wa habari.

  Pamoja na kutambua hilo APC inaelewa mahusiano mazuri yaliyopo,kwa
  muda mrefu kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa habari mkoani
  Arusha na ushirikiano uliodumu kwa muda mrefu sasa.

  Hata hivyo, kutokana na mazingira hayo ya Januari 5, 2011 ya kuonyesha
  kukamiana yaliyofanywa na baadhi ya askari polisi, APC inatoa muda wa
  wiki moja kwa jeshi hilo mkoani Arusha kuchukua hatua za haraka za
  kurekebisha kasoro zote hizo.

  Hatua ambazo Jeshi hilo linapaswa kuchukua ni pamoja na kuwaomba radhi
  waandishi wa habari kwa usumbufu na maumivu ya kupigwa waliyoyapata
  wakati wakiwa wanafanya kazi zao halali.

  Pili APC, inatoa tamko kuwa endapo msamaha huo hautatolewa katika
  kipindi hicho basi tutalazimika kuangalia upya mahusiano na
  ushirikiano wetu na Jeshi la Polisi na ikiwezekana kusitisha kabisa
  ushirikiano wa aina yoyote mpaka kila upande utakapozingatia umuhimu
  wa mwenzake.

  Tatu,tungependa kuona askari waliohusika kwa makusudi katika
  kuwadhalilisha waandishi wa habari,ambao wanafahamika hata kwa majina,
  wanachukuliwa hatua zinazostahili ikiwa ni pamoja na kulipa fidia
  waandishi waliodhurika na kuharibiwa vifaa vyao vya kazi.

  Ni utamaduni wa APC wa kuepuka kulumbana au kutofautiana kwa namna
  yoyote na wadau wetu Jeshi la Polisi likiwamo, lakini kamwe hatutakaa
  kimya tukiona tunadharauliwa na kunyanyaswa mbela ya jamii wakati
  tunatekeleza majukumu yetu

  tuko tayari kushirikiana na mdau yeyote anayejali kazi zetu
  tunazofanya kwa weledi na kamwe hatutamwogopa mtu, taasisi au mdau
  yoyote mwenye nia ya kutunyamazisha kwa sababu zake binafsi.

  Inawezekana iwapo kila mmoja atatimiza wajibu wake.


  Imetolewa na

  ARUSHA PRESS CLUB

  6th January,2011
   
 2. W

  We can JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wamwulize yule WAZIRI aliyegombana na waandishi wa habari siku za nyuma! Waandishi wa habari wakiamua kuandika tu negatives za askari, watajijimbia. Utakuta picha zao wakikojoa, wakijisaidia, wakifanya ngono, nk. Zingine nzuri hazitaandikwa....

  Mbona POLISI mmefikia/kufikishwa hapo?

  Hii nayo iongezwe kwa OKAMPO
   
 3. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Poleni waandishi.
  Yaliyowapata kwa vyovyote yalifanywa na askari wachache.
  Mnastahili kuombwa radhi.
  Polisi wetu ni wasikivu, watawasikiliza na kumaliza tofauti zilizojitokeza.
  Tuko pamoja nanyi.
   
Loading...