VUNJO: Hii hapa hotuba nzito ya Mwenyekiti wa TLP Taifa Mhe Dk Augustino Lyatonga Mrema kwa Watanzania

HOTUBA YA MHE DK AUGUSTINO LYATONGA MREMA-VUNJO

Ndg Wanavunjo na Watanzania kwa Ujumla, Mimi Augustino Lyatonga Mrema nimehudumu Serikalini kwa awamu zote tano,Leo naomba kusema toka ndani ya moyo wangu kwa hakika Sijawahi ona kiongozi Mchapakazi,Mpenda watu na Mwadilifu kama Dk John Pombe Joseph Magufuli kwani nataka Watanzania hasa vijana waelewe historia hili iliyotukuka,

Ndg Wanavunjo na Watanzania kwa Ujumla, Ni Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli Wa awamu ya tano ndio haswa anatembea kwenye nyayo halisi za Baba Wa Taifa hili Mwl Julius Kambarage Nyerere najua wale wote mliopevuka kiakili enzi za Baba Wa Taifa mtakubaliana na mimi kwamba huyu Mtu habahatishi na najua Watanzania wanajua na Sisi Wapinzani wote tunajua sijui kwanini tunaendelea kumzongazonga,

Ndg Wanavunjo na Watanzania kwa Ujumla, Sisi TLP kwahiari yetu wenyewe tulishaamua kutoa "Chama Chetu Pendwa" ili kitumike kama nyenzo ya kufanikisha na kurahisisha Ushindi Wa Kishindo Wa Mhe Dk John Pombe Magufuli Oct 2020 wanaotaka kumsaidia Rais kupitia Ugombea Wa Udiwani na Ubunge mnakaribisha sana muda bado upo,

Ndg Wanavunjo na Watanzania kwa Ujumla, Sisi TLP tunakwenda kujenga a " Royal Opposition " kwani hatuamini katika Upinzani Wa kupinga kila kitu kama wenzetu,Upinzani Wa Visasi na Kejeli kwa viongozi Wa Serikali na Serikali,Upinzani wakuwatumikia mabeberu Weupe na Weusi,Upinzani Wa kuchafua nchi yetu kitaifa na kimataifa,

Ndg Wanavunjo na Watanzania kwa Ujumla, Sisi TLP bado tunawakaribisha na kuwasubiri wale wote walioshindwa kwenye maoni ndani ya Vyama vyao hasa Chama cha Mapinduzi waje ili kila Jimbo/kata paweko na Wapigadebe Wa Rais Magufuli watakaomuhakikishia Ushindi Wa Kishindo kwa Vitendo,

CCM, Waswahili wanasema "mdharau mwiba mguu huota tende" Msiwadharau wapinzani wenu kwa hakuna anayejua nguvu yao,Hakuna anayejua nchi ngapi ziko nyuma yao,Hakuna anayejua wanaukwasi kiasi gani? Hakuna anayejua mwisho watafanya nini! Njia sahihi ya kukabiliana nao ni kuwa na watu wanne katika kila kata wataohakikisha Ushindi Wa kishindo Wa Rais wetu Dk John Pombe Joseph Magufuli na si vinginevyo kwani umoja ni nguvu,

Ndg Wanavunjo na Watanzania kwa Ujumla,
TLP mpaka sasa tunawagombea waliochukua fomu 72 naamini wote watateuliwa na NEC nakwanamna tulivyojipanga tutashinda na tutaongoza kambi rasmi ya Upinzani Bungeni ya kwanza tangu kuanza kwa vyama vingi mwaka 1992 ambayo itakuwa "Royal" itakayosimamia masilahi ya Taifa letu kwanza na mambo mengine yote baadae,Nawahakikishia TLP inakwenda kuweka historia Oct 2020 ya kuwa Chama kikuu cha Upinzani kilichoshinda bila mabavu wala matusi kwa Serikali na Rais,

Ndg Wanavunjo na Watanzania kwa Ujumla, Urais Wa Rais Magufuli ni zaidi ya Ubunge Wa Mrema hapa Vunjo,Ni ubatili mtupu kama Mimi nitashinda Vunjo huku Rais Magufuli akiangushwa ndio maana Mimi katika Uzee huu niamua kusimama ili nihesabiwe na wanaompigania Rais Magufuli kwa hali na mali,Nawahakikishia Mimi na Chama changu hatarudi nyuma kamwe,

Ndg Wanavunjo na Watanzania kwa Ujumla, Nimesimama tena kuandika historia mpya ya Upinzani Tanzania mkiacha ile ya mwaka 1995,Upinzani utakaofurahiwa na kuheshimiwa zaidi na watoto wetu au watoto Wa watoto wetu,Ndio maana kwa ruhusa yenu nimerudi kugombea tena kwa kuzingatia maombi yenu,Nawahakikishia nitatumia fursa hii kuwajengeeni aina mpya ya Upinzani nchini wakati nikimsindikiza Rais Magufuli kwenye miaka yake hii mitano ( 5 ) ya mwisho nikiwa Mbunge Wa Vunjo kwa umuhimu mkubwa nimalizie yale yote yaliyosimama tangu niyaache mwaka 2015 najua mnafahamu,

Ndg Wanavunjo na Watanzania kwa Ujumla, Nimewasikia baadhi ya wagombea wanachochea vurugu na ghasia nchini kisa tu wao tayari Wa "VISA" na nyumba za kuishi huko ughaibui,Chonde Watanzania msikubali mtego huu Wa kijinga unaolenga kusambaratisha na kuvuruga kabisa Taifa letu tulilolijenga kwa Jasho na damu tangu enzi zile za akina Mkwawa na baadae Sisi akina Mrema mpaka hizi za Rais Magufuli Leo, Katu msikubali nendeni kamchagueni tena Rais wenu shujaa na shupavu Dk John Pombe Joseph Magufuli trh 28/10/2020.

Lyatonga Mrema,
Mkt Wa TLP
Hii taaaasusi bado ipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom