VUNJA MBAVU: Ali Kiba avunja kikao cha usuluhishi Mondi na Harmonize

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
KUMBE Januari Mosi, 2020, ingeleta bonge la kishindo. Diamond Platnumz na Harmonize, walikubaliana kukutana na kumaliza tofauti zao. Alikiba buana akavunja kikao.

Ilikuwaje? Utamu wote uliletwa na prisenta maarufu TZ wa kuitwa Suti ya Brauni, alipopiga stori na Vunja Mbavu.
VM: Unasema Harmonize na Diamond wangeandika historia Januari Mosi 2020. Historia gani?

SUTI YA BRAUNI: Amkeni amkeni amkeniiii! Diamond aliomba msamaha kwa Harmonize. Kuna mambo ambayo kila upande ulitaka.

VM: Mambo gani hayo?

SUTI YA BRAUNI: Huu ni umbea usioumiza. Diamond alitaka Harmonize arudi WCB kwa sababu tangu Harmonize aondoke imekuwa tena sio WCB, imegeuka “dabliyuu thiii biii”.

VM: Harmonize akajibu nini?

SUTI YA BRAUNI: Harmonize alikubali lakini alitoa masharti.

VM: Enhee, hapo kwenye masharti.

SUTI YA BRAUNI: Amkeni buana! Harmonize kwanza alitaka ile nafasi ya Sallam WCB apewe Sarah. Yaani Sarah wa Harmonize ndiye awe meneja wa WCB wa michongo ya kimataifa. Halafu Harmonize ndiye awe top WCB, Diamond awe chini yake. Kisha Babu Tale na Mkubwa Fella wawe mabaunsa, yule Mwarabu Fighter na Kifesi ndio wawe mameneja.

VM: Hayo masharti hayo, Diamond alijibu nini?

SUTI YA BRAUNI: Diamond alikubali yote. Kwanza alifurahia Sarah kuwa meneja wake, si unajua ni Mzungu? Hata Babu Tale na Fella kuwa mabaunsa hakuwa na kipingamizi. Shida ni Alikiba.
VM: Sasa Alikiba aliingiaje hapo?

SUTI YA BRAUNI: Amkeniiiiii! Harmonize na Diamond baada ya kukubaliana, walitaka msuluhishi ili wakasaini makubaliano mbele yake. Diamond alitaka Juma Lokole ndiye awe msuluhishi wao, Harmonize alimkataa. Harmonize alimpendekeza Mwijaku, Diamond akamkataa. Sarah akamnong’oneza Harmonize kuwa ampendekeze Alikiba.
VM: Ikawaje?

SUTI YA BRAUNI: Harmonize alipompendekeza Alikiba, Diamond alikubali. Wakampigia simu Alikiba. Hakukataa kuwa msuluhishi, ila aliwauliza wapo wapi? Harmonize alikuwa Tandahimba na Diamond Kigoma. Alikiba akawaambia waende nyumbani kwake akawasuluhishe muda huohuo.

VM: Sasa hapo tatizo lilikuwa nini si wangeenda tu?

SUTI YA BRAUNI: Diamond na Harmonize waliomba kikao kifanyike Mwaka Mpya wamalize kwanza shoo za Kigoma na Tandahimba. Alikiba aliwajibu ‘kama hamtaki kuja sasa hivi acheni’.

Credit: Luqman Maloto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom