BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Vumbi kesi ya Dk. Slaa
na Mustafa Leu
Tanzania Daima
UTATA unaotokana na tofauti za takwimu umeibuka mahakamani wakati kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Karatu, Dk. Willbrod Slaa (CHADEMA) ilipokuwa ikiendelea kusikilizwa jana.
Kuibuka kwa utata huo kulikuja baada ya aliyekuwa wakala wa jimbo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Joseph Hayim, kuwasilisha takwimu alizodai kuwa ni za matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 zinazotofautiana na zile za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Katika kesi hiyo ambayo wanachama watatu wa CCM wanapinga ushindi wa Dk. Slaa, wakala huyo anadaiwa kuwasilisha majina ya baadhi ya vituo vya kupigia kura ambavyo havimo katika orodha ya vituo rasmi vya NEC.
Wakala huyo ambaye ni shahidi wa walalamikaji, aliiambia Mahakama Kuu Kanda ya Arusha inayosikiliza kesi hiyo kwamba, matokeo katika kituo cha Shangit B yaliyoandaliwa na CCM yalikuwa hayafanani na matokeo sahihi ya NEC.
Hayim alidai mahakamani hapo kuwa kutokana na tofauti hiyo ya matokeo kati ya yale ya NEC na aliyoletewa na mawakala wa chama hicho kutoka vituoni ni vigumu kujua ni mgombea gani wa ubunge kati ya yule wa CCM au CHADEMA (Slaa) alishinda.
Shahidi huyo alidai pia kuwa, katika kituo kingine cha Mamsai kulikuwa na tofauti katika fomu za CCM na zile za NEC na hivyo kuleta utata wa kutojulikana mshindi halisi.
Katika kituo kingine cha Njia Panda, Hayim alidai hakukuwa na kituo kama hicho, ingawa katika fomu za CCM zimeonyeshwa kilikuwepo na karatasi zake za malalamiko ziliwasilishwa kwa bahati mbaya mahakamani kama kielelezo.
Aliiambia mahakama hiyo kuwa yeye alipokea karatasi za matokeo kutoka kwa mawakala wa Chama chake Cha Mapinduzi ambazo zilionyesha kuwepo kwa kituo cha Njia Panda, lakini ukweli ni kuwa kituo hicho hakikuwepo.
Alipoulizwa na Wakili Tundu Lissu, anayemtetea Dk. Slaa kuhusu taarifa za kituo kimoja kuwa na fomu mbili za matokeo, shahidi huyo alisema kuwa swali hilo hawezi kulijibu na alikuwa anaiachia mahakama, kwani kila kituo kilikuwa na fomu moja ya matokeo na fomu 20 za CCM zilizoongezeka zilipelekwa mahakamani kwa bahati mbaya.
Akiendelea kutoa ushahidi, alisema kuwa katika kituo cha Getamol, matokeo yalibadilishwa na yale ya CCM yakawekwa kama ya CHADEMA na ya CHADEMA yakaandikwa kama ya CCM, na taarifa ya msimamizi wa uchaguzi inaonyesha kuwa CHADEMA ilishinda kwa kura 79 katika kituo hicho.
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi ni fomu zipi basi za matokeo zipokelewe na mahakama kama kielelezo, alisema yeye amezileta mahakamani ili mahakama ndiyo iangalie.
Shahidi huyo alikiri kuwapo kwa fomu ambazo ziliandaliwa na CCM zinazoonyesh matokeo, ingawa hazina majina na sahihi za mawakala, na nyingine zilizowasilishwa mahakamani hapo kwa makosa ambayo yalitokea katika vituo vya kupigia kura wakati wa kuzijaza.
Hayim aliiambia mahakama hiyo kuwa mawakala wote 253 wa CCM hawakujaza fomu za malalamiko ya matokeo, ingawa walikuwa na haki ya kufanya hivyo kupitia fomu namba 16 inayotolewa na msimamizi wa uchaguzi kwa madai kuwa walinyimwa.
Alidai pia kuwa katika matokeo hayo, CCM iliandaa taarifa yenye kuchanganya kura za madiwani na kuzifanya kuwa ndizo za wabunge.
Kuhusu hilo, alieleza kuwa, walalamikaji wenzake walibadilisha herufi moja katika fomu kwenye kituo cha Mango'ra kwa kuongeza herufi A, badala ya ile ya awali, ambapo hakuna herufi hiyo, na taarifa yake aliyoiandaa ilikuwa haina muhuri wa msimamizi na akaiomba mahakama iikubali.
Aliiambia mahakama kuwa alipokea fomu hizo Novemba 25 mwaka 2006, na siku iliyofuata wakafungua kesi. Shahidi huyo ataendelea kutoa ushahidi wake leo.