Vugu vugu la kukamatwa viongozi:Tuondoe na kinga ya Raisi kila mtu abebe msalaba wake

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,682
149,886
Moja ya jambo ambalo uwepo wake haunifurahishi ni hiki kinachoitwa "kinga ya Raisi" awe madarakani na baada ya kustaafu.

Wakati huu viongozi wanakamatwa, wabunge wanafungwa jela, wanawekwa mahabasu,n.k nafikiri ni wakati muafaka wa kuondoa hii kinga ili nao wawajibike iwapo watatuhumiwa na baadae kuthibika kutumia vibaya madaraka yao.

Ninapoona nchi tajiri kama Ufaransa Raisi anashitakiwa alafu huku kwetu katika nchi masikini maraisi tunawapa kinga,kwakweli huwa nashindwa kuelewa kabisa tunawaza nini vichwani mwetu.

Wakati umefika tubadili Katiba na maraisi wanaotumua vibaya madaraka yao washitakiwe wawapo madarakani na hata baada ya kustaafu.

Kila mtu abebe msalaba wake bila kujali cheo chake.
 
Hiyo katiba abadili nani? Na lini!!?
Kama ulimsikia mkubwa wa nchi alisema hiyo suala ya katiba haikuwa ajenda yake.
Mwafwaa!
 
wabadili kweli raisi ashitakiwe na mtu mwemye tuhuma za kifisadi hasiruhusiwe kugombea uraisi na wabunge ili wawe wabunge inabidi wawe na elimu ya juu tuondoe watu kama,,msukuma,sugu,majimarefu,mbowe....watu hata kufanya analysis za mambo ya maana hawajui
 
Fisadi Mkapa anastahili kuwa lupango, fisadi Kikwete anastahili kuwa lupango na fisadi Magufuli anastahili kuwa lupango. Wanaipiga vita rasimu ya Warioba ili isije kuwa katiba ya nchi kwani ina kipengele cha kinachowezesha Rais akiwa bado rais au kastaafu kupandishwa kizimbani kwa makosa aliyofanya kwa Jamhuri wakati akiwa madarakani. Sasa kipengele hicho kinawatia kiwewe sana.

Moja ya jambo ambalo uwepo wake haunifurahishi ni hiki kinachoitwa "kinga ya Raisi" awe madarakani na baada ya kustaafu.

Wakati huu viongozi wanakamatwa, wabunge wanafungwa jela, wanawekwa mahabasu,n.k nafikiri ni wakati muafaka wa kuondoa hii kinga ili nao wawajibike iwapo watatuhumiwa na baadae kuthibika kutumia vibaya madaraka yao.

Ninapoona nchi tajiri kama Ufaransa Raisi anashitakiwa alafu huku kwetu katika nchi masikini maraisi tunawapa kinga,kwakweli huwa nashindwa kuelewa kabisa tunawaza nini vichwani mwetu.

Wakati umefika tubadili Katiba na maraisi wanaotumua vibaya madaraka yao washitakiwe wawapo madarakani na hata baada ya kustaafu.

Kila mtu abebe msalaba wake bila kujali cheo chake.
 
mifumo ya serikali zetu ni mifumo ya kikoloni,kikundi kinachotawala ndio kinapata haki zote na wale wanaopinga utawala ni adhabu tu
saivi tupo kwenye mfumo wa vyama vingi ambao ni bandia,bado unatoa haki kwa upande wa utawala tu na bado unatambua kuwa wapinzanni ni maadui
 
Fisadi Mkapa anastahili kuwa lupango, fisadi Kikwete anastahili kuwa lupango na fisadi Magufuli anastahili kuwa lupango. Wanaipiga vita rasimu ya Warioba ili isije kuwa katiba ya nchi kwani ina kipengele cha kinachowezesha Rais akiwa bado rais au kastaafu kupandishwa kizimbani kwa makosa aliyofanya kwa Jamhuri wakati akiwa madarakani. Sasa kipengele hicho kinawatia kiwewe sana.

Wabunge wa CCM ni waoga sana hawawezi hata kunitetea wao wenyewe actually wa naogopa kukataa kwenye Uchaguzi.Wako kwa maslahi yao wenyewe.

Katiba ukisema.kipindi vitatu vinatosha mtu kuwa Mbunge lakini walikataa Katiba ya Warioba sababu inagusa maslahi yao.

Siyo rahisi,Nilitegemea walipopiga Kelele kuhusu Bunge lenye meno wange piga kura ya kumuondoa Tulia kwenye nafasi yake lakini ni kupiga zeze tu.

Huwezi kutaka Bunge huru wakati una NS anayelififisha Bunge kwa kisingizio cha kunitetea Serikali. Bunge lipo kwa ajili ya kuiwajibisha Serikali lakini Leo Serikali inaiwajibisja Bunge
 
Hapo ndio utaona kuwa bado tupo kwenye ukoloni. Ndio maana wanatawala kama wanamiliki Nchi. Washitakiwe kama wengine ndipo watakapojichunguza vizuri kabla hawajagombea.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Fisadi Mkapa anastahili kuwa lupango, fisadi Kikwete anastahili kuwa lupango na fisadi Magufuli anastahili kuwa lupango. Wanaipiga vita rasimu ya Warioba ili isije kuwa katiba ya nchi kwani ina kipengele cha kinachowezesha Rais akiwa bado rais au kastaafu kupandishwa kizimbani kwa makosa aliyofanya kwa Jamhuri wakati akiwa madarakani. Sasa kipengele hicho kinawatia kiwewe sana.
Nawashangaa sana walivyo mstari wa mbele kuhukumu wenzao wakati wao hawataka Katiba ibadilishwe ili nao wabebe misalaba yao.

Mungu si athumani ipo siku tu haya yatatimia.
 
Back
Top Bottom