VUDEO: Ni uchunguzi gani ili mtu ajue kuwa huu ni wizi mtupu kwa jina la "malipo ya posho ya.....??"

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Hii kitu kama kweli imefanyika Wizara ya fedha - HQ, basi tuna tatizo kubwa sana na usalama wa fedha ya umma chini ya watu hawa...

Waziri wa fedha kwa sasa ni Mwigulu Chemba. Kwa takwimu hizi za wizi huu wakati unafanyika zinazotolewa na PM, Mwigulu alikuwa hajawa Waziri bado...

Wakati huo kati ya March - April, Waziri alikuwa bado ni Dr. Philip Mpango ambaye sasa ni Vice President...

Mtu aweza kujiuliza swali hili, kuwa, Waziri na Katibu Mkuu wake, ambao ndio wenye wizara, walikuwa wapi na wanafanya nini? Je, hii imefanyika kwa baraka zao...?

Ukimsikiliza PM hapa, utagundua kuwa fedha nyingi imeibwa kwa jina la "posho ya......" wakati wa kipindi cha maombolezo ya msiba wa Hayati John Pombe Magufuli... Kwanini?


Duuh, kwa hali yoyote hili wala hata halihitaji uchunguzi ili mtu ajue kuwa huu ni wizi mtupu kwa jina la "malipo ya posho ya...."

Kama in uchunguzi, basi iwe ni nani na nani wanahusika kisha sheria ichukue mkondo wake. Hutuwezi kwenda hivi...!!
 
Kipindi cha katikati cha Mwendazake, ulikaa kimya mkawa mnakula pamoja
Sasa unajifanya Msafi uendane na kasi Mama....
 
Mei mosi, Mwigulu alikuwa bado hajawa waziri? Je Rais anayo mamlaka ya kumfukuza VP
 
Back
Top Bottom