Vuai, Kagasheki wapi ktk nchi hii mhalifu/jambazi anauawa serikali inasaidia mazishi na fedha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vuai, Kagasheki wapi ktk nchi hii mhalifu/jambazi anauawa serikali inasaidia mazishi na fedha.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by matongo manawa, May 20, 2011.

 1. m

  matongo manawa JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimeshangazwa na kauli za Mawaziri wa mambo ya ndani kuhusina na mauaji yaliyofanywa
  na dola dhidi ya watanzania waliokuwa wakipigania rasirimali za Taifa zinazoibiwa na wazungu
  wanaolindwa na dola,

  Masikini wanatarime hawa umaskini umewajaa huku wazungu weusi wachache kwa kushirikiana
  na wazungu weupe wanakula mema ya nchi.

  Kwanyakati tofauti mawaziri hawa wametoa kauli zinazotia kichefuchefu,
  kauli moja wapo nikwamba hawa watu waliouawa walikuwa ni wahalifu,aisee!

  Ingetosha NAHODHA KUISHIA hapo na serikali kukaa kimya,lkn kuendelea na jitihada
  nyingine kumeibua maswali mengi

  1.Nilini na wapi dola imeshaua wahalifu then ikashughulikia mazishi yao na kutoa rambirambi
  kwa ndugu za wahalifu?

  2.Kama marehemu walikuwa wahalifu kwanini serikali isitambe kwenye Runinga kama
  anavyofanya kova akiwa na vidhibiti kibao ikiwa ni pamoja na silaha walizotumia majambazi?

  Waheshimiwa damu ya wanatarime itawaandama vichwani mwenu.

  Nawasilisha.
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Warikuwa wanapambana na porisi...
   
 3. l

  lyimoc Senior Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakika damu ya wanatarime haitakwenda bure ukombozi wa nchi unakaribia poleni sana ndugu zetu wanatarime tukopamoja kukata tamaa ni mwiko mapambano yaendelee
   
 4. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wanakuja wanaowajali na kuwatetea wananchi leo tundu na marando soon tutajua ukweli.je wahalifu walipigwa risasi kwa mbele huku wakiwashambulia polisi au walipigwa kwa nyuma ikimaanisha walikuwa wanawakimbia polisi?naomba mwenye jibu kamili achangie
   
 5. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Maswali makubwa majibu mepesi.

  Ndio maana CCM inachukiwa sana na wananchi....wanazunguka kutafuta sababu lakini hizo ndio sababu. CCM haiko kwa maslahi ya nchi wala wananchi na ndio maana bila aibu hao mawazir (sic) wamefanya hivyo.
   
 6. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Nitoe pole zangu za dhati kwa wafiwa na wana Tarime wote kwa uhalifu na mauaji yanayotekelezwa na CCM na Serikali yake kwa ujira uchwara wa Barrick Gold Mine. Iko siku, na itafika tu....na haya mauaji na dhuluma na uonevu tutayakomesha kabisa.
   
 7. F

  FRANK MICHAEL Senior Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sisi huku arusha 2liambia kuwa 2lifanya fujo huko tarime majambazi, mi namuomba kamanda mbowe au amuulize mtoto wa mkulima aka handsome boy hili swali tusikie atasemje hii nchi imeuzwa kama amwamini nendeni loliondo kuna falme za kiarabu ndogo mungu bariki tz
   
 8. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  tunisia raisi alikimbia kwa sababu ya damu ya mtu mmoja aliyejiua kutokana na kukatishwa tamaa na serikali,wanatarime wlikuwa wanapinga utumwa kwenye ardhi yao wanaitwa waharifu,halafu mnagharimia mazishi,maana yke ni kuwa bajeti ya mauaji mlishaipanga na saizi mnataka kufanya matumizi wanaharamu nyie
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Suala zuru sana hili ili kubaini ukweli wa mambo.

  lakini nashauri Tume huru iundwe kuchunguza mauaji hayo kwani kinyume chake hakuta kalika huko. jana kapigwa Mbunge wao, kesho atapigwa kiongozi mwingine na hatimaye wataua viongozi watakaotembelea huko katika kulipiza kisasi
   
 10. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  njia ya muongo ni fupi!

  ukweli wanujua ndiyo maana kama kawaida yao wanahaha kuuzima usijulikane

  ole wao wanaowauwa watanzania wenzao kwa visingizio vya kila aina

  siku moja tutasema basi imetosha!!

  ..you can fool some people for some time but not all the people....

  kila siku ninaposikia mauji ya watanzania kwa style yoyote ile najiuliza hivi huyu aliyeapa

  kulinda maisha ya watanzania yuko wapi na nini maana ya kiapo chake?

  hivi tunamwajibisha vipi ikiwa ameshindwa kuwajibika?

  kila siku tunasikia watanzania wakiuliwa na yeye hasemi chochote labda akisema ni kwa

  wafadhili.

  hivi katika njanja za uwajibikaji kama sehemu ya utawala bora hatuna pa kwenda kuhusu hili?

   
 11. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Serikali ya CCM imetuchoka, wakubwa wachache wanajilimbikizia mali na wanakila kitu...ila wananchi tulio wengi tumechoka na hatuna kitu. Ukimlinganisha Kagasheki au Vuai hakuna hata mwananchi mmoja wa NYAMONGO, wanaelingana nae. Dhahabu ipo kwenye aridhi yetu..kabla ya uwekezaji wachimbaji wadogo wadogo walikua wakichimba na kupata fedha za kuendelezea maisha yao..na hakuna Mnyamongo hata mmoja alie wahi kuchimba na kwenda kuuza dhahabu Marekani na kuendeleza miradi ya Marekani. Sasa wamekuja majangili kwa kisingizio cha uwekezaji, hawalipi kodi, hakuna walichowekeza hapa kwetu cha faida, dhahabu yote wanaipeleka Marekani, fedha zote wanaenda kuendeleza miradi nchini kwao. Mnyamongo anae zungukwa na mdodi anabaki maskini wakutupwa, hakuna kitu cha maana anachopata, wao wakubwa wanagawiwa ten percent wanaishi Dar, ndugu zetu wakiuwa wanasema ni majambazi kwa kuwa tu hawaelewi hali alisi ya maeneo yale. Kauli zilizo tolewa na mawaziri wawili hao ni matusi ya waziwazi kwa Wanyamongo wote na wanatakiwa watuombe radhi na waje wajionee wenyewe hali halisi na si kusubiri report zilizo chakachuliwa. na ningependa kuwauliza Mawaziri husika maswali yafuatayo;

  1. Je, ni kwa kiasi gani wanalijua zoezi zima na ulipaji fidia wa watu walio kuwa na mashamba na nyumba zao kwenye maeneo ya mgodi lilizoendeshwa?
  2. Je, wale waathirika wa kemikali ya zebaki na kemikali nyingine mbaya zitokanazo na mgodi wanalipwaje na wako katika hali gani??
  3. kuna maendeleo gani ya waziwazi ambayo mwekezaji ameyaonesha katika eneo zima la NYAMONGO.

  Rai yangu ni kuwa msitupeleke kwenye hatua ya kupigania UHURU wa pili, ambao utatugarimu sana...ila ikibidi itabidi tu kwasababu ninyi akina Nahodha na serikali yenu hamna tofauti na wakoloni kwasababu mna watetea wawekezaji wasio na faidi kwa taifa letu kwa kuwauwa watanzania. Hii ni aibu kubwa
   
 12. m

  mgao wa umeme Member

  #12
  May 20, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jamini tujiulize, hivi hawa mapolisi wanao wapiga risasi watanzania akili zao ni timamu kweli au ni wavuta bangi, hivi hawa mapolisi wanajua haki za binadamu.
  Labda wanafanya hivyo wakidhani hao si ndigu zao, lakini yale unayo wafanyia familia za watu wengine kuna siku nawe familia yako itafanyiwa.
  Jeshi la polisi imulikwe. Kila siku tuna sema ipo siku tutachoka kuonewa, hiyo siku mbona haifiki. We need revolution, revolution hatuwezi kupata bila damu.
  Saa ya ukombozi ni sasa.
  2015 wakileta ujinga kama kawaida yao, vijana tufanye mapinduzi kama ya Egyt, Tunisia................
   
Loading...