Vuai Ali Vuai akalia kuti kavu ccm zanzibar , mipango ya kumng'oa yasukwa .

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,690
239,251
Ama kwa hakika MUOSHA HUOSHWA , Taarifa kutoka kisiwandui zinadokeza kwamba maisha ya uongozi ndani ya ccm kwa Mh Vuai yanaelekea mwisho , mipango ya kumwondosha imekamilika .

Anatuhumiwa kukitelekeza chama hadi kikawa na wakati mgumu kwenye uchaguzi mkuu ( kwa lugha ya watu wazima unaweza kusema anatuhumiwa kusababisha chama kushindwa )

Alipoulizwa Vuai mwenyewe kuhusiana na njama hizo alikiri kuzifahamu na kwamba mizengwe hiyo inasukwa na kikundi cha watu 15.

Alisema kikundi hicho kimekuwa na tabia za kifisadi ndani ya chama na kwenye jumuiya za chama , na kwamba muda ukifika atawataja hadharani .

Chanzo - Mwananchi .

Ushauri , Mh Vuai kama hutakiwi na wenzako ng'atuka usisubiri aibu .

CC - JABIR IDRISSA .
 
aah inatusaidia nini sisi raia wa kawaida ikiwa huyo muheshimiwa gamba ataondoshwa na magamba wenziwe
 
Ama kwa hakika MUOSHA HUOSHWA , Taarifa kutoka kisiwandui zinadokeza kwamba maisha ya uongozi ndani ya ccm kwa Mh Vuai yanaelekea mwisho , mipango ya kumwondosha imekamilika .

Anatuhumiwa kukitelekeza chama hadi kikawa na wakati mgumu kwenye uchaguzi mkuu.

Alipoulizwa Vuai mwenyewe kuhusiana na njama hizo alikiri kuzifahamu na kwamba mizengwe hiyo inasukwa na kikundi cha watu 15.

Alisema kikundi hicho kimekuwa na tabia za kifisadi ndani ya chama na kwenye jumuiya za chama , na kwamba muda ukifika atawataja hadharani .

Chanzo - Mwananchi .

Ushauri , Mh Vuai kama hutakiwi na wenzako ng'atuka usisubiri aibu .

CC - JABIR IDRISSA .
Ccm ina utaratibu wake wa kuteua naibu katibu mkuu
Hata hivyo inatarajiwa Magufuli atapanga sekretariet mpya
 
aah inatusaidia nini sisi raia wa kawaida ikiwa huyo muheshimiwa gamba ataondoshwa na magamba wenziwe

Hili ni jukwaa la siasa na hapa ni mahala pake kuzungumzia hili kama unahitaji kusaidiwa nenda jukwaa la ushauri au jukwaa la uchumi.
 
Aondolewe tu. Kwanza hata CCM yenyewe inalazimisha tu kutawala visiwani. Haitakiwi na wananchi wa huko.
Tatizo kubwa linaloikabili nchi hii ni ccm , sasa hawa vigogo wakishaanza kurogana ndiyo mwanzo wa chama chao kufa .
 
Back
Top Bottom