Vote: Viwanda (Magufuli) vs Kilimo (Kambarage)

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,031
2,000
Hebu naomba tutoe maoni juu ya fikra hizi 2 za ukuaji wa Uchumi nchini!

Hapa kuna waasisi wawili wa falsafa 2 mbili za uti wa mgongo wa uchumi wa taifa hili! Nyerere aliasisi kilimo na sasa Magufuli anaasisi viwanda kama ndio tegemeo la juu ktk uchumi wa nchi!

Kwa mtazamo wangu na vote for kilimo! Pia natoa ushauri kwa Mhe Rais Magufuli aachane na mpango wa Uchumi wa Viwanda! CCM na serikali yako mtaanguka 2020 kama hamkuwa makini! Miaka 5 ni mchache mno kwa kujaribu kufanya maendeleo ya mwendokasi! Fanya kazi mbili (2) tu ktk maisha yako ya miaka 5 Watanzania watakukumbuka milele!

Moja ya sifa ya mtu makini ni kuwa precise! Na ili huwe hivyo jaribu kupunguza mikakati as much as possible! Huwezi kuwa taifa lenye priorities 5, zenye strategies 4-5 kwa kila moja!

Hebu tazama hawa wazee wawili watakaokumbakwa ktk historia ya Tanzania! Kumbukumbu ya Mwl katika uchumi inaanzia ktk azimio la Arusha. Kuna sehemu tulifaulu na kuna sehemu tulikwama! Azimio jingine la kukumbukwa ni ka Zanzibar, nalo kuna sehemu tumefaulu na kuna sehemu tumefeli!

Haya maazimio mawili ni matamko ya Sera za uchumi, haya yalibadili mifumo kabisa ya uchumi na maisha, lkn pia yalikuja na mikakati ambayo ndiyo misingi mikuu ya maisha ktk vipindi vyote! Wote bado waliamini ktk Kilimo Ila kwa mbinu tofauti!

Mzee Mwinyi Kilimo chake hakikuenda sawa kwa kuwa soko huria lilishawishi sana. Mabepari kumiliki kila aina ya njia za kiuchumi na hivyo biashara kumeza kila kitu bila ya kujali mtindo rasmi wa kuingizia kipato unatokea wapi!

Wewe so far huna direction, unaonekana kuishi azimio la Arusha lkn unatekeleza mikakati ya azimio la Zanzibar. Huwezi kuwa raisi wa wanyonge kwa uchumi wa Viwanda.

Serikali yako ni ya kinyonge by the way, haiwezi kuhudumia wananchi, sasa huku huwapi huduma huku unawakaba koo, wakupe mtaji wa Viwanda, hawawezi. Rejea SHAMBANI, tumeshawekeza sana huko na siasa ni kilimo, kilimo ndio uti wa mgongo, kilimo kwanza etc!

Hizi lugha za Viwanda ni ngumu sana! Hatuna nishati ya umeme wa kuaminika, hatuna malighafi za kutosha kwa processing industries, lakini kikubwa zaidi hatuna capitals ujue hadi leo unashindwa kulipa boom la shule kwa universities, pesa ya field, afya na madawati tu bado tunaomba.

Ukipoteza hizi juhudi za Mwl, nduguze na CCM za 50 years, na kuanza zako za 5 years. Akija mwenzio naye atatupa kule Viwanda na kuanza vya kwake. Tunahitaji Viwanda yes lkn sio leo, acha tusubiri kwa miaka mingine 20 tutakuwa katika position nzuri zaidi.

So vitu viwili vya kufanya:-
  1. Tujenge Mabwawa ya umwagiliaji ktk Rufiji/Ruaha (Rufiji basin) huko Ruaha, Kilombelo na Rufiji. Mtera - Kibaigwa/Gairo, Wami - Dakawa, Pangani - Pangani/Nyumba ya Mungu na mikoa yote inayozunguka lake Victoria lazima iwe na irrigation schemes.
    • Hii itakuwa chachu kubwa ya uzalishaji wa malighafi za Viwanda kwa raisi wa 2035 - 2050
  2. Boresha upatikanaji wa nishati ya umeme!
    • Mtangulizi wako amejitahidi sana ktk kuongeza tija ktk upatikanaji wa nishati hii! Alipomaliza wote mlimsaidia kuainisha ongezeko from X to y! Hicho ndicho kitakachokuwa evaluated! Lkn pia hiyo itakuwa reflected ktk maisha ya mtanzania na ndio chachu ya uchumi wa Viwanda!
Maendeleo hayana shortcuts, huwa ni process, jibu huja automatically kama tumefanya mchakato vema, short than that failure is guaranteed.

Hebu jikumbushe shairi la darasa la NNE: "KAMA MNATAKA MALI, MATAIPATA SHAMBANI"
 

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,033
2,000
Nishart - Kilimo - Viwanda .

Endapo Hizi awamu zilizopita zingepokezana kwa mfumo huo hapo juu. .. leo tungekua kwnye Viwanda . ..na kazi ingekua nyepesi saana .

Tatizo tulipita hapa

Kilimo - Siasa - siasa - siasa - viwanda .
 

Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
2,000
Sera au mawazo ya kilimo hayakufanikiwa sababu kilimo kilibebwa na jembe la mkono kwenye vijiji vya ujamaa. That was a serious no brainer.

Ili kilimo kiendeshe uchumi wa nchi ni LAZIMA kiwe "commercial agriculture". Kilimo hiki kina mashamba yenye maelfu ya ekari, teknolojia na mashine za kufanyia kila shughuli shambani, wataalamu wa sayansi ya kilimo, miundombinu ya kusaidia usafirishaji wa mazao na malighafi, na masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.

Popote palipo na vitu vyote hivi lazima utakuta viwanda vinavyotegemea kilimo. Sasa kwa sura halisi ya nchi yetu ilivyo sina haja ya kuendelea kuandika.
 

concordile 101

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
1,299
2,000
Sera au mawazo ya kilimo hayakufanikiwa sababu kilimo kilibebwa na jembe la mkono kwenye vijiji vya ujamaa. That was a serious no brainer.
Ili kilimo kiendeshe uchumi wa nchi ni LAZIMA kiwe "commercial agriculture". Kilimo hiki kina mashamba yenye maelfu ya ekari, teknolojia na mashine za kufanyia kila shughuli shambani, wataalamu wa sayansi ya kilimo, miundombinu ya kusaidia usafirishaji wa mazao na malighafi, na masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.
Popote palipo na vitu vyote hivi lazima utakuta viwanda vinavyotegemea kilimo.
Sasa kwa sura halisi ya nchi yetu ilivyo sina haja ya kuendelea kuandika.
Yaan kwa mazingira yaliyopo hamna cha viwanda wala nini, sana sana wanacheza segere tu.

Wenzao kama Dubai ilibidi wafanye free tax kwa nationals ambao walikuwa wanafanya kazi kwa wale waliozid pato la USD 96,000 kwa mwaka. Kwanini walifanya hivi ili kuvutia wageni wengi.

Kuhusu kilimo wala haihitaji kampeni n kuondoa madalali katika soko na kuanzisha masoko ya bidhaa za kilimo pia kuruhusu kuwe na free exportation. Kukiwa scarcity ya chakula bei itakuwa nzuri wakulima wafanyabiashara watavutika kuwekeza kwenye kilimo.

Kwa mazingira yaliyopo bora mfanyabiashara anunue mabasi hata kumi kwa gharama usd 150000 +VAT. Kuliko akanunue Lateral irrigation scheme ambazo China zinapatokana mpaka kwa USD 95,000 before installation kwa ekari 200 Tractor usd 50000 ambazo ukiwekeza kwenye kilimo cha mpunga tu kwa mwaka mmoja tu unapata return yako na faida juu lakin kwenye mabasi return sio pungufu ya mwaka na bado ajali hazitabiriki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom