Vodafone k3571-z za vodacom ni vimeo a.k.a feki

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,842
8,231
Jamani kwa yeyote mwenye modem kutoka Vodacom aina ya Vodafone K3571-Z zinauzwa 25,000 atagundua haya yafuatayo

1.Inakula hela hata kama hujatumia hiyo bundle au hata ukitumia kidogo tu utakuta hela kweishney

2.Kupata net ni sawa na ngamia kupita tundu la sindano,wakati wote signal ziko chini sana.

3.Inakatika mara kwa mara Nilipoona hilo Tatizo nilienda kulalamika pale Vodashop Mlimani City lakini hakuna uvumbuzi wowte walionipa zaidi ya ubabaishaji tu,baadaye nilipokuwa kwenye internet cafe niliwasikia watu kama watatu nao wakilalamikia ufanisi wa hiyo modem, na mwisho nikapata tetesi kuwa hata utawala wa Vodacom wanajua tatizo la hizi modem,.

Kuna watu wameleta huo mzigo ambao ni sub standard na Vodacom nao wameamua kuwauzia watu ''mbuzi kwenye gunia'' Angalizo ni kuwa watu msije poteza fedha zenu kwa kununua hizo modem HAZIFAI na kama kuna asiyeamini aende akanunue jibu atalipata mwenyewe. Mwami Makamba kazi kwako ,angalia tutawakimbia kwa kutuletea vitu mbofumbofu
 
Back
Top Bottom