Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,499
- 9,279
Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya robo ya mwaka inayoishia Septemba 2019 zinaonesha kuwa kampuni ya Vodacom Tanzania ndiyo inayoongoza kwa kutoza gharama kubwa zaidi ambapo hutoza TZS 205 kwa megabyte (MB) mteja anayotumia.
Wakati Vodacom ikitoza kiwango hicho, nafasi ya pili inashikwa na Zantel ambayo hutoza TZS 93 kwa kila MB, huku wateja wa Airtel na Tigo wanalipa sawa ambao gharama ya MB moja ni TZS 29.
Wateja wa Halotel wanalipa TZS 22 kwa MB, huku wateja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wanalipa TZS 10, wakati wateja wa Smile ndio wanaotozwa gharama ndogo zaidi ya TZS 5 kwa kila MB moja. Gharama zote hizi ni bila kodi, na zinazotwa endapo mteja hajajiunga kifurushi.
TCRA imeeleza kuwa gharama za vifurushi mitandao ya simu nchini haitofautiani sana, na kwamba vifurushi hivyo ambavyo vimekuwa vikitumiwa sana vimeleta unafuu wa gharama za matumizi ya simu kwa wananchi.
Taarifa hiyo ya TCRA inaonesha kuwa mteja anaweza kupata dakika moja ya kupiga simu, MB moja, na ujumbe mmoja kwa gharama kati ya TZS 21 hadi TZS 62 endapo atajiunga kifurushi.
Chanzo: TBC