Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,045
- 20,408
Walionunua hisa mwaka wa 5 huu hakuna gawio zaidi ya elfu kumi tu, na hisa zao haziuziki.Nimeona wameshindwa kuendelea kudhamini premier league,sababu kubwa ikiwa ni hali mbaya ya kampuni.
Mkataba uliwataka wawe wanatoa bilioni 3 kila mwaka.Hata hivyo kwa msimu huu waliomba eti watoe milioni 500 tu kisha zilizobaki zingetolewa msimu ujao.
Kwa mawazo yangu hawa jamaa kiburi na janja janja yao ndivyo vimewadidimiza sana.Mimi ni mmoja wa niliokuwa wateja wao wakubwa nikitumia zaidi ya laki 3 ya kununua vifurushi mbali mbali kwa mwaka.Mimi ni mtu wa hali ya kawaida sana unaweza kusema ya chini au kati.Lakini mara nyingi hata ukinunua kifurushi cha saa 24 huwa hazifiki.Unakuta bado una dakika,lakini unaambiwa muda wa kifurushi umeisha nunua kifurushi kingine.
Hali hiyo imetukimbiza wengi kwani utapeli huu ulikuwa umekithiri sana kwenye hii kampuni.Wasitarajie msimu ujao watafanya vizuri kwani kipindi cha mpito wa kubadilika huchukua muda mrefu.Hadi wateja wavumilivu waanze kuisemea vizuri tena kampuni.
Binafsi nilitaka kuifufua line yangu ya Voda kwa kununua simu ndogo mwezi ujao ila kwa taarifa hizi inaonekana wateja wengi wanawakimbia.Inawezekana hawajajifunza.Bado wana mambo ya ukaburu hata kwenye biashara
VODA imeuliwa na Rosta