Vodacom wamenitapeli hela zangu kupitia huduma ya songesha

Ntandaba

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
923
1,465
Habari za jumapili wapendwa!
Nathubutu kutumia neno utapeli au wizi, nikiwa miongoni mwa mamia ya watumiaji wa mtandao wa vodacom kupitia huduma ya mpesa.

Ni takribani wiki tatu nimefuatilia hela zangu ambazo zilikatwa kimakosa kupitia huduma ya songesha kwenye namba yangu, Sijawahi kutumia hiyo huduma na wao baada ya kwenda ofisini kwao wakakiri imekatwa kimakosa.

Niliahidiwa kurudishiwa kwa masaa 48, lakini ni wiki tatu sasa nikienda ofisini kwao wanadai kitengo cha songesha bado kinashughulikia.

Je, ninaweza kuwashtaki ili hela zangu zirudi kwa riba kama wao walivyonikata kwa riba au ni taratibu zipi nizifanye kwa haraka ili nirudishiwe hela zangu.

Msaada wa kimawazo
 
Mkuu kwenye ufuatiliaji wako unawaona watu husika au ndio unaishia receiption..

Hakikisha unaongea na watu potential, WAHUSIKA kabisa ambao wakisema KESHO TUTARUDISHA unaondoka ukiwa na amani..

Fanya hivo au kama umeshafanya hvo basi nenda hatua nyingine
 
Nenda kwenye Baraza la usuluhishi nadhani ni MCC watakupa maelekezo na nina uhakika watakulipa mpaka pesa ya usumbufu na watakulipa pesa ya kueleweka labda uwaonee huruma,maana huo ni wizi wa mtandao japo we unasema wamekukata,hapo hakuna cha kukatwa huo ni wizi wa kimtandao na sheria zake zipo zitakulinda.
Pili inapaswa uwaambie kupitia hiyo pesa uliyoibwa imefelisha mambo yako mengi ambayo yamekwama kwa ajili ya hiyo pesa,japo yaweza kuwa ndogo!!

Kuna mzee aliwahi lipwa na Airtel milioni 28 kwa upuuzi kama huo,mzee alienda kuwashitaki wakamlipa,imagine milioni 28 ya mwaka 2005,si mchezo

CHIFWINOLOGY²
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom