VODACOM wameanza kunyooka

Zantel wangekua na special no ningehamia huko
Mimi mbona nimepata special namba kwa buku tu, nenda pale mikocheni hukosi. Maana bado zantel haina wateja wengi, ukijaribu namba yako utakuta haina mtu jaribu kwa 0779
 
Halotel nimewakataa, unaweza nunua 1GB halafu ukashindwa kuitumia, mtandao wao ni wa Kobe
Bila shaka upo mjini, na hiyo inamaanisha kuna watu wengi wanaotumia mtandao wa Halotel kwa ajili ya internet. Ukitaka kuhakikisha, jaribu kutumia internet yao kuanzia saa 6 hadi saa 12 kamili asubuhi (watu wengi wakiwa wamelala), ikiwa na kasi kwa mida hiyo, jua kuna watumiaji wengi.

Ukifika vijijini kwenye watumiaji wachache, mtandao unakuwa na speed kubwa. Shida Sasa, si kila kijiji kina 3G.
 
Voda kumenoga.
Kwa 1500 unapata dakika 150 (mitandao yote) 1GB na sms kwa siku 7
Bila shaka hiyo ni Dar supa uni, wiki 2 zijazo tu utakuwa umeshaondolewa hiyo ofa, ndio walivyo vodacom, hawana consistency, na hapo bado umeliwa, kwa pesa hiyo hiyo mwenzio napata 1.5 GB na zantel wapo consistency mwezi wa 4 huu toka nimejiunga zantel na sijaona kama kuna badiliko lolote, ww hiyo ofa nakupa zikizidi siku 30 hiyo ofa itakuwa imeondolewa ktk orodha ya vifurushi vyako, na hasa ukiwa unanunua kila siku. Badala waiache ili wapate pesa wao ndio wanaitoa wanakupa ofa ya juu. Voda mie cheap Yao ipo kwenye kiswaswadu
 
Voda walijiona wana monopoly /wanatunyonga sana kwenye mb
Habarini wanajamvi,

Leo nimeamka vema sana hasa baada ya kupata ujumbe kwa njia ya simu ukiniambia nikitia buku napata GB1 kwa siku 3 da, taratibu wanaanza kuongea lugha yetu, tuzidi kukaza hadi watuuzie GB1 kwa buku wiki nzima.

Haikuishia hapo nafungua wasafi nakutana na news vodacom wamejitoa kudhamini ligi kuu ya Tanzania, sababu zao kubwa wanasema asilimia kubwa ya wateja wao wamefutiwa usajili wa line zao kwahiyo mapato yamepungua very silly reason si waseme tu watu wameacha kununua mabando, kwahiyo mapato yamepungua. Tuendelee kuwanyoosha hadi wote warudi njia kuu.

Kwa sasa hivi hamna wa kunitoa Zantel, 1500 napata dakika 160, sms 500 na 1.5 GB wao wakae na data zao ila lazima wataisoma na uchumi huu wa Covid-19.
 
Bila shaka upo mjini, na hiyo inamaanisha kuna watu wengi wanaotumia mtandao wa Halotel kwa ajili ya internet. Ukitaka kuhakikisha, jaribu kutumia internet yao kuanzia saa 6 hadi saa 12 kamili asubuhi (watu wengi wakiwa wamelala), ikiwa na kasi kwa mida hiyo, jua kuna watumiaji wengi.

Ukifika vijijini kwenye watumiaji wachache, mtandao unakuwa na speed kubwa. Shida Sasa, si kila kijiji kina 3G.
Ni kweli mkuu inawezekana ila kama ni hivyo sisi wa dar haloteli haitufai tena
 
Voda walijiona wana monopoly /wanatunyonga sana kwenye mb
Upo sahihi, na ndio faida ya kuwa na ushindani, hiyo monopoly system ingeondolewa hata kwenye huduma za umeme nadhani TANESCO wangejirekebisha sana. Hasa Tanesco mkoa wa pwani ni pasua kichwa, natafuta namna ya kumfikishia mkuu wa mkoa kunenge malalamiko yangu kuhusu watu wa Tanesco mkoa wa pwani.
 
Upo sahihi kiongozi ! tatizo ni sheria iliyotungwa na bunge inayoipa total monopoly hili shirika la TANESCO.Ukiruhusu ushindani katika utoaji wa huduma then gharama kwa mlaji wa mwisho zinapungua,anyway tuone kama itakuwepo tija kwenye bwawa la Nyerere kama tunavyoaminishwa na politicians
Upo sahihi, na ndio faida ya kuwa na ushindani, hiyo monopoly system ingeondolewa hata kwenye huduma za umeme nadhani TANESCO wangejirekebisha sana. Hasa Tanesco mkoa wa pwani ni pasua kichwa, natafuta namna ya kumfikishia mkuu wa mkoa kunenge malalamiko yangu kuhusu watu wa Tanesco mkoa wa pwani.
 
Ukiona hivyo umewekwa kitengo cha matajiri.

Hata ufanyaje huchomoki huko.
... ha ha ha! Eti Ndugu Igombe fisherman umewekwa kwenye kundi la matajiri ndio maana ofa za voda utazisikia tu. Halafu kwenye kundi hilo ni fedheha kujiunga na mabando; unatakiwa kutumia muda wa maongezi direct! Nyie ndio mnatakiwa muibebe kampuni na sisi makapuku tukifaidi humo humo. You know the 80/20 rule?
 
Bila shaka hiyo ni Dar supa uni, wiki 2 zijazo tu utakuwa umeshaondolewa hiyo ofa, ndio walivyo vodacom, hawana consistency, na hapo bado umeliwa, kwa pesa hiyo hiyo mwenzio napata 1.5 GB na zantel wapo consistency mwezi wa 4 huu toka nimejiunga zantel na sijaona kama kuna badiliko lolote, ww hiyo ofa nakupa zikizidi siku 30 hiyo ofa itakuwa imeondolewa ktk orodha ya vifurushi vyako, na hasa ukiwa unanunua kila siku. Badala waiache ili wapate pesa wao ndio wanaitoa wanakupa ofa ya juu. Voda mie cheap Yao ipo kwenye kiswaswadu
Ofa ya kanda ya ziwa hiyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom